JAFO AWATAKA WATUMISHI WA WIZARA NA FCC KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZA UWEKEZAJI. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

JAFO AWATAKA WATUMISHI WA WIZARA NA FCC KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZA UWEKEZAJI.

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dk.Seleman Jafo,Pia, amewataka watumishi wa Wizara ya viwanda na biashara kuhakikisha wanashughulikia changamoto zilizopo za uwekezaji huku akiitaka FCC kuharakisha miungano sahihi ya Taasisi za kibiashara ili kukuza uchumi nchini.

Sophia Kingimali.
By Sophia Kingimali.
05 Dec 2024
JAFO AWATAKA WATUMISHI WA WIZARA NA FCC KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZA UWEKEZAJI.

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dk.Seleman Jafo,Pia, amewataka watumishi wa Wizara ya viwanda na biashara   kuhakikisha wanashughulikia changamoto zilizopo za uwekezaji huku akiitaka FCC kuharakisha miungano sahihi ya Taasisi za kibiashara ili kukuza uchumi nchini.

Waziri Jafo ameyasema hayo leo Disemba 5,2024 jijini Dar es Salaam, wakati akifungua maadhimisho ya kitaifa ya siku ya ushindani Duniani, yaliyoandaliwa Kitaifa na Tume ya Ushindani (FCC).

Amesema serikali ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan imeendelea kuweka fursa mbalimbali za uwekezaji nchini kuhakikisha wafanyabiashara wanakuza uchumi wao na Taifa.

"Serikali ya Rais Dk.Samia imeendelea kufanya maboresho mbalimbali ya Taasisi ikiwemo  ya uwekezaji (TIC) kwa lengo la kukuza uwekezaji nchini.

"Kama hiyo haitoshi, katika kuboresha mazingira ya biashara nchini  Rais Dk.Samia  ameunda tume ya maboresho ya kodi, kuhakikisha biashara zinashamiri na kufanyika kwa wepesi zaidi," amesema.

Ameongeza kuwa, sh.trilioni 6.5  ilitolewa kujenga Bwawa la Julius Nyerere kuchochea upatikanaji wa gharama za bidhaa Kwa kuwepo nishati ya kutosha, ujenzi wa reli ya kisasa, kurahisisha usafirishaji, uboreshaji wa bandari, kuhakikisha kuwa biashara zinafanyika kwa wepesi kupakia na kushusha mizigo ikiwa ni jitihada za kuimarisha na uwekezaji nchini.

Akotoa maagizo, kwa Katibu Mkuuu Viwanda na Biashara, amemtaka kuangalia changamoto zilizopo za kisheria na kuziwasilisha, Mkurugenzi wa FCC kuimarisha mifumo ya kushaghihisha biashara na kuharakisha miunganiko ya makampuni, wafanyabiashara kuchangamkia masoko ya biashara yaliyopo nje ya nchi.

"Wataalamu wa Wizara na FCC, kuhakikisha wanashughulikia maoni yote yanayotolewa ndani ya mjadala wa maadhimio hayo na yaweze kunifikia ndani ya siku 14",Amesema.

Aidha amewasisitiza vijana kuhakikisha wanafanya kazi kwa juhudi kubwa, ubunifu na jadilifu, huku watumishi wa serikali kuhakikisha wanashughulikia kwa haraka ushindani nchini.

Katika hatua nyingine, amewataka wafanyabiashara kutumia vyema masoko yaliyopo ikiwemo soko huru la Biashara Afrika na lile la ulimwenguni huku akisisitiza kutengeneza bidhaa bora zenye ushindani.

Amesema lengo la maadhimisho hayo ni kuhakikisha wafanya biashara wanashindana kwa haki, na usawa bila kuingiliana katika maslahi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Hashil Abdallah, amesema FCC ni miongoni mwa Taasisi zinazofanya vizuri katika Wizara ya viwanda na biashara katika kuendelea kuimarisha biashara na ushindani.

Amesema kuwa FCC imeendelea kuimarisha ushindani sokoni kwa kuhakikisha inasimamia vyema suala hilo nchini, na kuwepo mafanikio makubwa.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi FCC, Aggrey Mlimuka amesema Tume hiyo imeendelea kutekeleza sheria ya ushindani huku ikiwa katika hatua za kupatiwa cheti cha ushindani

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa FCC, William Erio, amemshukuru Waziri Jafo na wageni mbalimbali waliofika katika maadhimisho hayo, yenye lengo ya kudumisha ushindani nchi.

MPANGO KAZI KUKOMESHA MAUAJI YA WATU WENYE UALBINO WADAU WAIPONGEZA SERIKALI.

MPANGO KAZI KUKOMESHA MAUAJI YA WATU WENYE UALBINO WADAU WAIPONGEZA SERIKALI.

Wachimbaji wa Madini wahimizwa kulipa kodi ya Serikali.

Wachimbaji wa Madini wahimizwa kulipa kodi ya Serikali.

FDH YAIPONGEZA UNEP KUENDELEZA AGENDA YA MAZINGIRA KWA WENYE ULEMAVU

FDH YAIPONGEZA UNEP KUENDELEZA AGENDA YA MAZINGIRA KWA WENYE ULEMAVU

JAMII YAASWA KUTUMIA NISHATI SAFI ILI KUUNGA MKONO JITIHADA ZA RAIS SAMIA

JAMII YAASWA KUTUMIA NISHATI SAFI ILI KUUNGA MKONO JITIHADA ZA RAIS SAMIA

SERIKALI YA SAMIA KUZALISHA AJIRA MPYA MILIONI 1.2 KILA MWAKA

SERIKALI YA SAMIA KUZALISHA AJIRA MPYA MILIONI 1.2 KILA MWAKA