HARUSI YA KIHISTORIA YAFUNGWA KRETA YA NGORONGORO | The Dodoma Post
The Dodoma Post Utalii

HARUSI YA KIHISTORIA YAFUNGWA KRETA YA NGORONGORO

Tarehe 15 Desemba 2024 Kreta ya Ngorongoro imepambwa na tukio adhimu na la kihistoria la maharusi wa Kitanzania kufunga ndoa ndani ya Hifadhi huku hao wakipunga upepo mwanana kwenye mazingira asilia yaliyozungukwa na wanyama mbalimbali wakiwemo Big 5.

Na Kassim Nyaki, Ngorongoro Kreta.
By Na Kassim Nyaki, Ngorongoro Kreta.
16 Dec 2024
HARUSI YA KIHISTORIA YAFUNGWA KRETA YA NGORONGORO

Bw. Kelvin Mwakaleke na mkewe
Jackline Nyalu wamefunga Ndoa ndani ya Kreta ya Ngorongoro wakisindikizwa na wazazi, ndugu, jamaa na marafiki huku wakishuhudiwa na macho ya Wanyama mbalimbali wakiwemo Simba, Faru, Tembo, Nyati, Chui, Pundamilia, Nyumbu, Thomson Gazelle, ambao wamekuwa mashuhuda  wa tukio hilo lililofanyika pembeni mwa bwawa maarufu la Ngoitoktok wakati huo Viboko  wakinogesha shughuli kwa kuogelea.

Akielezea tukio hilo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Mariam Kobelo anayesimamia huduma za Utalii na Masoko NCAA ameeleza kuwa "Leo ni siku ya furaha na ya  kipekee isiyosahaulika, tumeshuhudia tukio adhimu na akramu lenye baraka za Mungu kwa maharusi hawa kufunga ndoa kwenye bustani ya Eden (Ngorongoro Crater).

Hili ni jambo jipya na la kwanza katika historia ya NCA na limechagizwa na juhudi za Utangazaji wa vivutio vya utalii vinavyopatikana ndani ya  NCA huku vimeendelea kuibua chachu kwa watanzania wengi, ndio maana unaona leo tumeona zao jipya la utalii. Tunaendelea kuwakaribisha wananchi wengine kuja hifadhi ya Ngorongoro kwa matukio kama haya" alifafanua Kamishna Kobelo.

Kufunga ndoa ndani ya hifadhi ni fursa muhimu katika kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo Ngorongoro hali inayoamsha ari kwa watalii wa ndani kuongezeka na kuchangia mapato ya Serikali.

Akielezea tukio hilo huku akiwa na nuru ya tabasamu na fursa Bwana harusi Kelvin Mwakaleke akiwa na mkewe Jackline ameeleza kuwa kufunga ndoa ndani ya hifadhi ilikiwa ndoto yake ambayo hatimae imetimia.

"Nilimuomba Mungu kuniongoza kufanikisha tukio hili, kufunga ndoa kreta ni uzoefu ambao siwezi kuusahau, ni eneo lenye vivutio vya kila aina kwa mtu yoyote kutembelea, lina uzuri wa asili wanyama wengi na uoto wa asili uliohifadhiwa vema,  mimi, mke wangu na ndugu wachache tuliounganika hapa tutakuwa mabalozi wa kuitangaza hifadhi ya Ngorongoro" alisema Bw. Mwakaleke.

Aidha, alishukuru kwa huduma nzuri iliyotolewa na wahifadhi wote waliokuwa bega kwa bega kuhakikisha wanakuwa salama na kufurahia mandhari na kukamilisha ndoa yao.

#WedinWild
#merryandwild
#Ngorongoroawaits
#visitngorongoro
#unforgettableexperiences

NYUMBA 2,500 ZAKAMILIKA MSOMERA, USAMBAZAJI WA UMEME WAFIKIA ASILIMIA 98, MIUNDOMBINU MINGINE MBIONI KUKAMILIKA.

NYUMBA 2,500 ZAKAMILIKA MSOMERA, USAMBAZAJI WA UMEME WAFIKIA ASILIMIA 98, MIUNDOMBINU MINGINE MBIONI KUKAMILIKA.

TANZANIA NA UTURUKI KUSHIRIKIANA SEKTA YA MALIASILI NA UTALII

TANZANIA NA UTURUKI KUSHIRIKIANA SEKTA YA MALIASILI NA UTALII

TUKIFANYA KAZI KWA PAMOJA TUTAPATA WATALII WA KUTOSHA UKANDA WA KARIBE NA MAENEO JIRANI - BALOZI POLEPOLE

TUKIFANYA KAZI KWA PAMOJA TUTAPATA WATALII WA KUTOSHA UKANDA WA KARIBE NA MAENEO JIRANI - BALOZI POLEPOLE

WACUBA WAVUTIWA NA HIFADHI YA NGORONGORO

WACUBA WAVUTIWA NA HIFADHI YA NGORONGORO

BAROZI DKT CHANA AFUNGA ONESHO LA S!TE ASIFU MAFANIKIO YALIYOPATIKANA.

BAROZI DKT CHANA AFUNGA ONESHO LA S!TE ASIFU MAFANIKIO YALIYOPATIKANA.