Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa ametatua mgogoro wa wachimbaji wadogo wa Madini ya Ruby Wilaya ya Longido Mkoani Arusha uliodumu kwa zaidi ya miaka mitano kati ya Kampuni ya Paradiso Mineral (T) Limited na Mzee Malulu Ole.
Makubaliano hayo yameafikiwa jana Desemba 6, 2025 wakati Dkt. Kiruswa alipofanya ziara ya kutatua mgogoro huo katika Kata ya Mundarara Wilaya ya Longido Mkoani Arusha.
Mhe. Dkt. Kiruswa ameielekeza kampuni ya Paradiso kutekeleza makubaliano walioafikiana na Mzee Malulu Ole Moringo ya kulipa fidia hiyo kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza wanatakiwa kulipa milioni 100 ifikapo Januari 30, 2025 na milioni 50 ifikapo Machi 30, 2025.
Aidha, Dkt. Kiruswa amesisitiza makubaliano hayo kutekelezwa kwa wakati na endapo kampuni ya Paradiso itakiuka makubaliano hayo Serikali itachukua hatua za kisheria ikiwemo kusimamisha shughuli za uchimbaji katika eneo hilo.
Sambamba na hayo, Dkt. Kiruswa amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan haitaki migogoro katika sekta ya Madini ili sekta hiyo kuwa na maendeleo.
Pamoja na mambo mengine, Dkt. Kiruswa amewataka wachimbaji wa madini kuendelea kulipa kodi za Serikali ambapo fedha hizo zitakwenda kuboresha huduma za kijamii kama vile kujenga shule na usambazaji wa umeme maeneo mbalimbali hapa nchini.Awali, Ofisi ya Madini Arusha ilifanya utafiti na kugundua Malulu Ole Moringo ana haki katika eneo hilo ambalo familia ya Jango Master inafanya shughuli za uchimbaji Madini.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha (CCM) Papaanakuta Moleli amempongeza Dkt. Kiruswa kwa kazi nzuri anazozifanya za kutatua migogoro mbalimbali ya wachimbaji wa Madini hapa nchini.
Nayo, Familia ya Jango Master ikiwakilishwa na Victor Jango imekubali kulipa fidia hiyo kwa wakati, huku Malulu Ole Moringo naye akiridhia kupokea fidia hiyo kama Serikali ilivyoelekeza.
PBPA YASHAURI UJENZI WA MATENKI YA MAFUTA BANDARI YA MBAMBA BAY
BoT KUJA NA MFUMO WA KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO YA KIFEDHA KIDIGITAL.
MPANGO KAZI KUKOMESHA MAUAJI YA WATU WENYE UALBINO WADAU WAIPONGEZA SERIKALI.
JAFO AWATAKA WATUMISHI WA WIZARA NA FCC KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZA UWEKEZAJI.
JAMII YAASWA KUTUMIA NISHATI SAFI ILI KUUNGA MKONO JITIHADA ZA MHE.RAIS
JAMII YAASWA KUTUMIA NISHATI SAFI ILI KUUNGA MKONO JITIHADA ZA RAIS SAMIA
FDH YAIPONGEZA UNEP KUENDELEZA AGENDA YA MAZINGIRA KWA WENYE ULEMAVU
MPANGO KAZI KUKOMESHA MAUAJI YA WATU WENYE UALBINO WADAU WAIPONGEZA SERIKALI.
JAFO AWATAKA WATUMISHI WA WIZARA NA FCC KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZA UWEKEZAJI.
BoT KUJA NA MFUMO WA KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO YA KIFEDHA KIDIGITAL.