DKT.TULIA AMUAPISHA BALOZI KOMBO AMTAKA KUCHAPA KAZI. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

DKT.TULIA AMUAPISHA BALOZI KOMBO AMTAKA KUCHAPA KAZI.

Spika wa bunge Dkt Tulia Ackson amemuapisha balozi Mahamoud Thabit Kombo huku akimtaka kwenda kufanyakazi aliyokusudiwa kuifanya ili kukamilisha mipango mingi ya maendeleo iliyoanzishwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Sophia Kingimali.
By Sophia Kingimali.
25 Jul 2024
DKT.TULIA AMUAPISHA BALOZI KOMBO AMTAKA KUCHAPA KAZI.

Spika wa bunge Dkt Tulia Ackson amemuapisha balozi Mohamed Thabit Kombo huku akimtaka kwenda kufanyakazi aliyokusudiwa kuifanya ili kukamilisha mipango mingi ya maendeleo iliyoanzishwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza mara baada ya kumuapisha leo Julai 25,2014 katika ofisi ndogo za bunge jijini Dar es salaam Dkt Tulia amesema kuteuliwa kwa barozi Kombo kuwa mbunge na waziri wa mambo ya nje na uhusiano wa Afrika Mashariki ili kutumikia wananchi lakini pia kuendeleza mipango mingi ya maendeleo iliyowekwa na Rais.

"Rais anamipango mingi na mingi ameiweka wazi hivyo anawategemea ninyi ili kuweza kuitekeleza kwa ustawi wa Taifa",Amesema Dkt Tulia.

Amesema uapisho aliofunya ni kwa mujibu wa kanuni ya 30(2)(b) ya kanuni za kudumu za bunge toleo la februari 2023 ambapo inatamka kuwa mbunge kabla ya kuanza kazi ataapishwa na spika.

Amesema pia sheria hiyo imempa mamlaka spika kuchangua eneo la kumuapishia kama hakuna mkutano wa bunge unaoendelea na baadae spika kutoa taarifa bungeni kwenye kikao cha kwanza.

Kombo aliteuliwa na Rais kuwa mbunge na waziri Julai 21,2024 mara baada ya kutenguliwa aliyekuwa waziri wa mambo ya nje na ushirikiano Afrika mashiriki Januari Makamba.

Baadhi ya wabunge walioshiriki katika hafla hiyo ni Stegomena Tax Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Londo ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki.

EKARI 1,165 za mashamba ya bangi zateketezwa Morogoro

EKARI 1,165 za mashamba ya bangi zateketezwa Morogoro

DCEA YAFANYA OPARESHENI MAALUM YA SIKU TISA MKOANI MOROGORO.

DCEA YAFANYA OPARESHENI MAALUM YA SIKU TISA MKOANI MOROGORO.

FCS KUADHIMISHA WIKI YA AZAKI SEPTEMBA 9,ARUSHA.

FCS KUADHIMISHA WIKI YA AZAKI SEPTEMBA 9,ARUSHA.

JAMII YA KIMASAI IMEANZA KUENDANA NA KASI YA UTANDAWAZI.

JAMII YA KIMASAI IMEANZA KUENDANA NA KASI YA UTANDAWAZI.

TBS YAFUNGUA MASHINDANO YA TUZO ZA UBORA KITAIFA.

TBS YAFUNGUA MASHINDANO YA TUZO ZA UBORA KITAIFA.