WAZIRI CHANA ATETA NA UJUMBE WA BENKI YA DUNIA | The Dodoma Post
The Dodoma Post Utalii

WAZIRI CHANA ATETA NA UJUMBE WA BENKI YA DUNIA

Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi, Dkt. Pindi Chana amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka Benki ya Dunia ukiongozwa na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bw. Nathan Belete katika Ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii, jijini Dodoma leo Septemba 5, 2024.

The Dododma Post
By The Dododma Post
05 Sep 2024
WAZIRI CHANA ATETA NA UJUMBE WA BENKI YA DUNIA

Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi, Dkt. Pindi Chana amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka Benki ya Dunia ukiongozwa na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bw. Nathan Belete katika Ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii, jijini Dodoma leo Septemba 5, 2024.

Ujumbe huo umekuja kumpatia mrejesho wa ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Benki ya Dunia hasa katika uhifadhi wa maliasili na utekelezaji wa mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW)ikizingatiwa kwamba Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) ameteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Samia Suluhu Hassan kuiongoza Wizara hiyo.

Akizungumza katika kikao hicho, Chana ameishukuru Benki ya Dunia kwa namna ambavyo imeendelea kuiwezesha Tanzania kwenye juhudi zake za uhifadhi na kuahidi kuendeleza ushirikiano huo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii anayeshugulikia maliasili, Kamishna Benedict Wakulyamba na  Mratibu wa Mradi wa REGROW, Aenea Saanya.

SERIKALI- HAKUNA MWANANCHI ANAYEONDOLEWA NGORONGORO KWA AJILI YA UTALII BALI UHIFADHI

WAZIRI MKUU MAJALIWA AWAPONGEZA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII MAONESHO YA NANENANE

WAZIRI KAIRUKI AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KUSHIRIKI MKUTANO WA PILI WA SHIRIKA LA UTALII DUNIANI KUHUSU UTANGAZAJI UTALII- KANDA YA AFRIKA NCHINI ZAMBIA

TANZANIA YAUNGA MKONO AGENDA ZA SHIRIKA LA UTALII DUNIANI ZA UWEKEZAJI WA KIMKAKATI NA USALAMA WA MAENEO YA UTALII.

UNDERSTANDING THE REASONS BEHIND THE VOLUNTARY RESETTLEMENT OF NGORONGORO RESIDENTS WITHIN THE RESERVE.