FCS KUADHIMISHA WIKI YA AZAKI SEPTEMBA 9,ARUSHA. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

FCS KUADHIMISHA WIKI YA AZAKI SEPTEMBA 9,ARUSHA.

TAASISI isiyo ya Kiserikali ya Foundation For Civil Society (FCS) inatarajia kuanza maadhimisho ya wiki ya azaki Septemba 9 hadi 13 mwaka huu jijini Arusha ambapo mashirika zaidi ya 20 yatashiriki na washiriki 500 wanatarajiwa kushiriki.

Sophia Kingimali.
By Sophia Kingimali.
23 Aug 2024
FCS KUADHIMISHA WIKI YA AZAKI SEPTEMBA 9,ARUSHA.

Hayo yamebainishwa leo, Agosti 23, 2024 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa FCS, Justice Rutenge wakati akizungumza na Waandishi wa Habari.

"Maadhimisho ya Wiki ya Azaki yanafanyika Kwa wakati mahususi katika taifa letu tukiwa na mambo kadhaa tutakayojadili ikiwemo Uchaguzi wa mwaka huu wa Serikali za Mitaa, Uchaguzi Mkuu ujao utakaofanyika mwakani na Uzinduzi wa Dira ya Taifa ya 2025- 2050.

Amefafanua kuwa mchakato wa Dira ya Taifa ufanyika kila baada ya miongo mitatu hivyo Kwa kuwa inazinduliwa mwakani, fursa ambayo imepatikana ni muhimu kuijadili ili kutengeneza michakato ya Maendeleo kupitia sauti za wananchi tofauti na ilivyozoeleka miaka ya nyuma kutengenezwa na jopo la wataalam pekee ambayo wakati mwingine inakuwa ngumu kutekelezeka.

"Wanalinganisha na nchi nyingine kutengeneza Dira ya Taifa ingawaje inapaswa itokane na sauti,mawazo,mtazamo na maoni ya wananchi ndiyo maana tunasema sauti ni kipengele muhimu kwenye Kauli mbiu ya Wiki ya Azaki,"amesema.

Amefafanua kuwa dira ya taifa, ifike wakati itokane na maoni ya watanzania namna wanavyotaka licha ya uwepo wa tofauti wa  dini, umri na kijinsia na ni vema ikatangazwa Katika tukio hilo la mwaka huu.

Ameongeza kuwa kauli mbiu ya mwaka huu imeelekea kwenye kipindi muhimu wa  Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Uchaguzi Mkuu mwakani na Uzinduzi wa Dira ya Taifa.

Ameweka wazi kuwa Kauli Mbiu hiyo inasema Sauti, Dira, Thamani ambapo akizungumzia kuhusu thamani amasema kwamba ni namna itakavyotengenezwa kupitia  Sauti za  wananchi na utekelezaji wake itakuwa jambo la msingi.

"Nasisitiza kwamba Wiki ya Azaki thamani itapatikana kwa ushirikiano wa makundi mbalimbali hivyo ni vema kila mtu ashiriki katika mchakato huo wa maendeleo," amesema.

Naye Mwenyekiti  wa Kamati ya maandalizi ya Wiki ya Azaki, Nesia Mahenge, amesema  Wiki ya Azaki imekuwa utamaduni wa kawaida kwa asasi hizo kukutana kila mwaka kwa lengo la kujifunza kama sehemu ya sekta za Asasi za kiraia (Azaki)

Pia wanaangalia changamoto wanazokutana nazo na vitu gani wanaweza kuvifanya kushirikiana pamoja ili kuleta maendeleo kwa pamoja.

"Ushirikiano katika sekta zote kuangalia sekta ya Azaki asasi za kiraia na upande wa Serikali,sekta binafsi na wadau wa maendeleo kwa ujumla namna gani tutashirikiana kuleta maendeleo nchini Tanzania.

“Katika Wiki ya Azaki tupo zaidi ya Mashirika 20 na tumetengeneza Kamati ya Maandalizi na mwaka huu ni wa sita na  tunajivunia kuendelezaa huu utamaduni Kila mwaka na itafanyika Septemba 9 hadi 13,2024 watafanyia mkoani Arusha na washiriki zaidi ya 500 watakuwepo”, amesema.

EKARI 1,165 za mashamba ya bangi zateketezwa Morogoro

EKARI 1,165 za mashamba ya bangi zateketezwa Morogoro

DCEA YAFANYA OPARESHENI MAALUM YA SIKU TISA MKOANI MOROGORO.

DCEA YAFANYA OPARESHENI MAALUM YA SIKU TISA MKOANI MOROGORO.

JAMII YA KIMASAI IMEANZA KUENDANA NA KASI YA UTANDAWAZI.

JAMII YA KIMASAI IMEANZA KUENDANA NA KASI YA UTANDAWAZI.

TBS YAFUNGUA MASHINDANO YA TUZO ZA UBORA KITAIFA.

TBS YAFUNGUA MASHINDANO YA TUZO ZA UBORA KITAIFA.

FCS YAIOMBA SERIKALI KUWAWEZESHA MAKUNDI MAALUM MIUNDOMBINU YA KIDIGITAL

FCS YAIOMBA SERIKALI KUWAWEZESHA MAKUNDI MAALUM MIUNDOMBINU YA KIDIGITAL