FCS YAIOMBA SERIKALI KUWAWEZESHA MAKUNDI MAALUM MIUNDOMBINU YA KIDIGITAL | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

FCS YAIOMBA SERIKALI KUWAWEZESHA MAKUNDI MAALUM MIUNDOMBINU YA KIDIGITAL

Asasi za Kiraia nchini kupitia Shirika la The Foundation for Civil Society (FCS), imeiomba Serikali iangazie katika kuhakikisha makundi maalum yanawezeshwa kufikia miundombinu ya kidigitali ili waweze kushiriki katika michakato ya maendeleo na kujiimarisha kiuchumi.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
13 Aug 2024
FCS YAIOMBA SERIKALI KUWAWEZESHA MAKUNDI MAALUM MIUNDOMBINU YA KIDIGITAL

Hayo yamesemwa na Meneja Programu wa FCS Nasim Losai katika mkutano wa kitaifa wa watu wenye ulemavu, madiwani na wadau, uliofanyika Agosti 12, 2024 Jijini Dar es salaam.

Losai amesema kuwa mkutano huo umejikita katika kuangazia ushiriki wa watu wenye ulemavu  katika maendeleo, uchumi na kijamii, huku ukiangazia matumizi ya takwimu za sensa katika kuboresha  mipango ya halmashauri za wilaya na ngazi za kata.

Aidha, ameeleza kuwa Serikali imekuwa Sikivu katika kuhakikisha makundi maalum yanafikiwa na kuwezeshwa katika shughuli za kiuchumi na kujiongezea kipato, nakwamba FCS wamekuwa wakIisadia serikali katika kuunga mkono juhudi hizo kutokana na zoefu wao wa zaidi ya miaka 20 ya kufanya kazi na jamii.

"FCS tuna zaidi ya miak 20 tumekuwa tukisaidia serikali hasa katika shughuli za jamii na kutetea watu wenye ulemavu na michakato ya kiserikali, hasa kwenye majengo mengi mioundombinu imebadilika na kazi kubwa imefanywa na FCS pamoja na makundi haya" amsema Losai.

Kwa upande wake Mshauri wakitalam masuala ya watu wenye ulemavu Tanzania  Peter charlse, amesema mkutano huo umejumuisha watu  mwenye ulemavu  zaidi ya 600 kutoka ndani ya Jiji la Dar es salaam wakiwepo madiwani 60 wa viti maalimu na wale wakuteuliwa.

Amesema kuwa malengo ya mkutano huo ni kuwajengea uelewa watu wenye ulemavu katika masuala mbalimbali na kuangazia zaidi eneo la uchumi na kuona  fursa zipi  walemavu wameweza kushirikishwa na ambazo wanaziweza.

"Ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu bado ni mdogo ndio maana tumewaalika madiwani ili  kuangalia changamoto zilizopo na kuwajengea ili kuyaingiza katika mipango yao ya maendeleo kupitia Mabaraza yao ndani ya halmashauri" amesema.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu Tanzania  Hamadi Abdallah komboza, amesema  changamoto kubwa kwa watu wenye ulemavu ni masuala ya ajira, huku akimuomba kamshina wa kazi  na vyama vyenye ulemavu kufanya ukaguzi kwenye mashirika na taasisi ambazo zinapaswa kuajiri watu wenye ulemavu lakini bado hazijatekeleza nakwamba msukumo zaidi unahitajika.

Katibu  Mkuu Shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania, Jonas Lubalo ameishukuru taasis ya Ikupa Trust Fund kwa kuendelea  kuchangia na kutoa huduma kwa watu  wenye ulemavu katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

(LHRC) chatoa maelekezo kwa vyombo vya ulinzi na usalama Kufuatia mauaji ya watoto watatu wa familia moja

(LHRC) chatoa maelekezo kwa vyombo vya ulinzi na usalama Kufuatia mauaji ya watoto watatu wa familia moja

FURAHIKA WAJIVUNIA MAFANIKIO ASILIMIA 75 YA WAHITIMU WAKE KAPATA AJIRA.

FURAHIKA WAJIVUNIA MAFANIKIO ASILIMIA 75 YA WAHITIMU WAKE KAPATA AJIRA.

EKARI 1,165 za mashamba ya bangi zateketezwa Morogoro

EKARI 1,165 za mashamba ya bangi zateketezwa Morogoro

DCEA YAFANYA OPARESHENI MAALUM YA SIKU TISA MKOANI MOROGORO.

DCEA YAFANYA OPARESHENI MAALUM YA SIKU TISA MKOANI MOROGORO.

FCS KUADHIMISHA WIKI YA AZAKI SEPTEMBA 9,ARUSHA.

FCS KUADHIMISHA WIKI YA AZAKI SEPTEMBA 9,ARUSHA.