Septemba 7, 2023 Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mathew Mwaimu (Jaji Mstaafu) amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Balozi wa Marekani nchini Tanzania, ulipotembelea Makao Makuu ya Ofisi za Tume zilizopo mtaa wa Kilimani jijini Dodoma.
Ujumbe huo wa watu watatu uliongozwa na Mshauri wa masuala ya Siasa na Uchumi katika Ubalozi huo, Bwana Jonathan Howard aliyeambatana na Bwana Andy Allen na Bi. Beatrice.
Katika mazungumzo yao Ujumbe huo ulipata fursa ya kuifahamu zaidi Tume na majukumu yake na Mpango Kazi wa Kitaifa wa Haki za Binadamu.
Pia, katika mazungumzo yao viongozi hao walijadili maeneo mbalimbali ya mashirikiano kwa lengo la kukuza na kulinda haki za binadamu nchini.
Mkurugenzi wa Malalamiko na Uchunguzi, Bi. Suzana Pascal aliambatana na Mwenyekiti wa Tume katika mazungumzo hayo.
KOREA KASKAZINI YAWANASA ‘SNIPER’ UKRAINE, YADAI RUSSIA INAWAUA MAJERUHI
MAREKANI HALI TETE, MOTO WAUA 16 LOS ANGELES, UPEPO WATARAJIWA KUONGEZEKA
Ajali ya gari yajeruhi mamia ya watu Ufaransa
Maria Sarungi atekwa Kenya wasiojulikana watajwa
BENKI KUU YAWAGEUKIA WATENGENEZAJI, WAUZAJI ‘PUTTY’