

Gavana wa zamani wa Lagos, Bola Ahmed Tinubu ameapishwa leo kuwa rais mpya wa Nigeria
Gavana wa zamani wa Lagos, Bola Ahmed Tinubu ameapishwa Mei 29, 2029 kuwa rais mpya wa Nigeria, hatua hiyo inakuja kufuatia uchaguzi uliofanyika Februari 25, mwaka huu uliompa ushindi Rais huyo ambao pia ulikumbwa na utata na kusababisha kupingwa na vyama vya upinzani mahakamani.
Tinubu ameapishwa kuwa Rais mpya katika hafla iliyofanyika kwenye uwanja wa Eagle Square Mjini Abuja ambapo alishangiliwa na umati na mkewe, Oluremi Tinubu, alisimama kando yake alipokuwa akila kiapo chake na kutia sahihi nyaraka.
Muda mchache tu hapo awali, Makamu wake wa Rais Kashim Shettima aliapishwa kuwa Makamu wa Rais mpya wa Nigeria katika hafla hiyo.
Huu ndio wakati Tinubu amekuwa akiusubiri katika kipindi chake chote cha maisha ya siasa na hatimaye ameapishwa kuwa Kiongozi wa nchi hiyo yenye uchumi mkubwa zaidi barani Afrika, huku akirithi changamoto mbalimbali kutoka kwa Rais anayemaliza muda wake, ikiwemo ukosefu wa usalama, uchumi unaoyumba na wapiga kura waliogawanyika pamoja na ukosefu wa ajira huku vijana wakizidi kuongezeka.
Maelfu ya watu wameondoka nchini humo kutokana na hali ya ukosefu wa usalama na kwa mujibu wa takwimu za uhamiaji zilizochapishwa wiki iliyopita, raia wa Nigeria sasa ni miongoni mwa wapokeaji wakubwa wa viza nchini Uingereza.
Hata hivyo, Rais anayeondoka madarakani Muhammadu Buhari ametetea miaka minane ya uongozi wake, wakati wa hotuba iliyorekodiwa kwenye televisheni Jumapili iliyopita, Buhari alidai kuwa anaondoka madarakani huku nchi hiyo ikiwa katika hali nzuri kuliko alipoingia madarakani kwa mara ya kwanza.
Hotuba hiyo imekabiliwa na ukosoaji mkubwa kutoka kwa raia wa Nigeria, ambao wanalalamika juu ya ongezeko la gharama za maisha, pamoja na ukosefu wa usalama chini ya utawala wake.
Baadhi ya watu wana wasiwasi kuwa huenda kipindi cha uongozi cha Rais Tinubu kisiwe cha kuleta mabadiliko nchini humo, kutokana na kile wanachodai kuwa alikuwa na mchango mkubwa katika kumfanya Buhari achaguliwe, hivyo Tinubu atakabiliwa na shinikizo la kuonesha kwamba anaweza kutatua changamoto zilizopo mbele yake kwa haraka zaidi kuliko ilivyokuwa kwa mtangulizi wake.
Hata hivyo, gumzo limekuwa ni kuhusu uimara wa afya yake baadhi wakisema hana uimara kulinganisha na nguvu yake wakati alipokuwa gavana wa jiji la Lagos.
Tangu kufanyika kwa uchaguzi uliompa ushindi februari mwaka huu, amesafiri nje ya nchi mara mbili na kuzua maswali kuhusu afya yake, mnamo mwaka 2021 alitumia miezi kadhaa akiwa Uingereza akitibiwa ugonjwa ambao haukutajwa hadharani.
Tinubu amekuwa akipuuzilia mbali ukosoaji huo akisema kazi yake akiwa mkuu wa nchi haihitaji uimara kama wa mwanariadha wa olimpiki huku wafuasi wake wakimlinganisha na Rais wa Marekani Joe Biden mwenye miaka 80 kwa kumtaja kama mzee mwenzake.
Wanigeria wamekuwa na vuguvugu mitandaoni wakionesha kuchoshwa kuona marais wa nchi hiyo wakitumia muda mrefu kwenye hospitali za nje ya nchi na kusababisha nchi kukosa udhibiti wake kikamilifu.
Sherehe hiyo ya kuapishwa Rais Tinubu imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Afrika akiwemo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Rwanda Paul Kagame, Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa na Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune.
MTIHANI WA DARASA LA SABA KUFANYIKA SEPTEMBA 10,WADAU WAASWA KULINDA AMANI NA UTULIVU KIPINDI CHA MITIHANI.
TANESCO YAENDELEA KUBORESHA HUDUMA KWA WATEJA KWA KUNUNUA VITENDEA KAZI VYA USAFIRI
Doyo Aendelea na Kampeni Muheza, Aahidi Kutatua Changamoto za Wananchi.
MWAGO ATEMA CHECHE AHAIDI MAKUBWA AKIPEWA RIDHAA NA WANANCHI JIMBO LA MBAGALA.
UZINDUZI MKUBWA WA KAMPENI JIMBO LA MCHINGA
Mavunde: Nitahakikisha Mtumba Inang’aa Kwa Huduma na Maendeleo
DKT NCHIMBI AITEKA RORYA | WANANCHI WATHIBITISHA KUTIKI OKTOBA 29 KWA KISHINDO.
VIKAO VYA KUANDAA MKUTANO WA 35 WA BARAZA LA KISEKTA LA MAWAZIRI LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI VYAANZA JIJINI ARUSHA.
MZEE JOSEPH BUTIKU ALIVYOIBUKIA KATIKA MKUTANO WA KAMPENI WA DK.EMMANUEL NCHIMBI RORYA
Matumizi ya Nishati Safi Kupikia Yapata Msukumo Mpya