TANESCO YAENDELEA KUBORESHA HUDUMA KWA WATEJA KWA KUNUNUA VITENDEA KAZI VYA USAFIRI | The Dodoma Post
The Dodoma Post Nishati

TANESCO YAENDELEA KUBORESHA HUDUMA KWA WATEJA KWA KUNUNUA VITENDEA KAZI VYA USAFIRI

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limezindua mpango mpya wa kuboresha huduma kwa wateja kwa kununua vitendea kazi ikiwemo magari 100, bajaji 100 na pikipiki 284, hatua inayolenga kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma bila kujali jiografia ya maeneo wanayoishi wateja wake.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
09 Sep 2025
TANESCO YAENDELEA KUBORESHA HUDUMA KWA WATEJA KWA KUNUNUA VITENDEA KAZI VYA USAFIRI

* Imenunua magari 100, bajaji 100 na pikipiki 284 ili kumfikia mteja kwa haraka na kwa wakati
*Takribani shilingi bilioni 1.3 yaokolewa gharama za kukodisha usafiri

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limezindua mpango mpya wa kuboresha huduma kwa wateja kwa kununua vitendea kazi ikiwemo magari 100, bajaji 100 na pikipiki 284, hatua inayolenga kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma bila kujali jiografia ya maeneo wanayoishi wateja wake.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Septemba 09, 2025, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO, Bi. Irene Gowelle, alisema uamuzi huo umefuatia ziara ya Mkurugenzi Mtendaji Bw. Lazaro Twange ambaye alibaini uhitaji mkubwa wa vitendea kazi katika mikoa mbalimbali nchini.

“Shirika limenunua vifaa hivi ili kuongeza ufanisi ambapo magari, bajaji na pikipiki tayari vimesambazwa katika mikoa mbalimbali. Lengo letu ni kumfikia mteja kwa haraka na kwa wakati, bila kujali jiografia ya eneo husika.

Aidha, hatua hii imepunguza gharama kwa kiasi kikubwa, kwani awali tulikuwa tukitumia shilingi bilioni 1.3 kila mwezi kukodisha magari,” alisema Bi. Gowelle.

Aliongeza kuwa mbali na kurahisisha upatikanaji wa huduma, uwepo wa vitendea kazi hivyo utaboresha pia mazingira ya kazi kwa wafanyakazi wa TANESCO, ambao ni nguzo muhimu katika kuhakikisha wateja wanapata huduma bora.

Pia aliwataka watendaji wa shirika hilo kuvihifadhi na kuvitumia kwa malengo yaliyokusudiwa.

Vitendea kazi hivyo vinatarajiwa kutumika hususan katika maeneo yenye madawati ya dharura yanayotoa huduma saa 24, ili kuhakikisha changamoto za wateja zinatatuliwa kwa haraka na kwa wakati.

Matumizi ya Nishati Safi Kupikia Yapata Msukumo Mpya

Matumizi ya Nishati Safi Kupikia Yapata Msukumo Mpya

AHADI YA SERIKALI KUFIKISHA UMEME WA GRIDI KAGERA YATEKELEZWA

AHADI YA SERIKALI KUFIKISHA UMEME WA GRIDI KAGERA YATEKELEZWA

DKT. BITEKO ATAKA WATUMISHI WIZARA YA NISHATI NA TAASISI ZAKE KUWA MFANO WA MATUMIZI NISHATI SAFI YA KUPIKIA.

DKT. BITEKO ATAKA WATUMISHI WIZARA YA NISHATI NA TAASISI ZAKE KUWA MFANO WA MATUMIZI NISHATI SAFI YA KUPIKIA.

WANANCHI WATAKIWA KUTUNZA AFYA ZAO KWA KUTUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA.

WANANCHI WATAKIWA KUTUNZA AFYA ZAO KWA KUTUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA.

AGIZO LA MINADA YOTE NCHINI KUTUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA LAANZA KUTEKELEZWA.

AGIZO LA MINADA YOTE NCHINI KUTUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA LAANZA KUTEKELEZWA.