

Baraza la mitihani nchini(NECTA) limetangaza rasmi kuanza kwa mtihani wa kumaliza elimu ya msingi huku likitoa rai kwa jamii na wadau mbalimbali wa mtihani huo kuhakikisha mtihani huo unafanyika kwa amani na utulivu bila ya kuwepo na udanganyifu.
Baraza la mitihani nchini(NECTA) limetangaza rasmi kuanza kwa mtihani wa kumaliza elimu ya msingi huku likitoa rai kwa jamii na wadau mbalimbali wa mtihani huo kuhakikisha mtihani huo unafanyika kwa amani na utulivu bila ya kuwepo na udanganyifu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 9,2025 jijini Dar es salaam Katibu mtendaji wa NECTA Prof.Said Mohamed amesema jumla ya watahiniwa waliosajiliwa 1,172,279 wanatarajiwa kufanya mtihani huo.
"Jumla ya watahiniwa 1,172,279 wamesajiliwa ambapo kati yao wavulana ni 535,138 sawa na asilimia 45.65 na wasichana ni 637,141 sawa na asilimia 54.35 kati ya hao watahiniwa asilimia 93.35 watafanya mtihani huo kwa lugha ya kiswahili lakini asilimia 6.65 watafanya mtihani huo kwa lugha ya Kiingereza kwani ndio lugha walizokuwa wanajifunzia",Amesema.
Aidha ameongeza kuwa watahiniwa wenye mahitaji maaluum waliosajiliwa kufanya mtihani huo ni 4,679 ambapo kati yao 92 wasioona 1551 wenye uoni hafifu,1079 wenye uziwi,448 wenye ulemavu wa akili na 1,509 wenye ulemavu wa viungo.
"Maandalizi yote kwa ajili ya mtihani huo yamekamilika ikiwa ni pamoja na usambazaji wa karatasi za mitihani pamoja na nyaraka zote muhimu zinazohusu mtihani huo pamoja na maandalizi yote kwa ajili ya watahiniwa wenye mahitaji maalum yamefanyika ipasavyo",Amesema.
Sambamba na hayo Katibu Mtendaji huyo ametoa wito kwa kamati za mitihani,wasimamizi,wamiliki wa shule na jamii kuhakikisha usalama wa vituo vyote vya mitihani unaimarishwa na vituo hivyo vinatumika kwa kuzingatia muongozo uliotolewa na Baraza la Mitihani nchini.
Pia amewataka wamiliki wa shule na wakuu wa shule kutoingilia majukumu ya wasimamizi wa mtihani katika kipindi chote cha mtihani kwani baraza halitasita kukifutia kituo chochote cha mtihani endapo litajiridhisha pasipo shaka kuwa uwepo wake unahatarisha usalama wa mtihani wa Taifa.
TANESCO YAENDELEA KUBORESHA HUDUMA KWA WATEJA KWA KUNUNUA VITENDEA KAZI VYA USAFIRI
Doyo Aendelea na Kampeni Muheza, Aahidi Kutatua Changamoto za Wananchi.
MWAGO ATEMA CHECHE AHAIDI MAKUBWA AKIPEWA RIDHAA NA WANANCHI JIMBO LA MBAGALA.
UZINDUZI MKUBWA WA KAMPENI JIMBO LA MCHINGA
WATEJA WAKUBWA WA HOTELI MOROGORO WAKAMATWA KWA WIZI WA UMEME.
Mavunde: Nitahakikisha Mtumba Inang’aa Kwa Huduma na Maendeleo
Matumizi ya Nishati Safi Kupikia Yapata Msukumo Mpya
WAZIRI MKUU AWATAKA MADEREVA WA SERIKALI KUFANYAKAZI KWA WELEDI
Mbeya Yafurika Kumuaga Mwanahabari Kadala Komba
BRELA YAFANYA KAZI NZURI YA URASIMISHAJI BIASHARA MWANZA