VIJANA NCHINI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA YA UFUGAJI SUNGURA KIBIASHARA. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

VIJANA NCHINI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA YA UFUGAJI SUNGURA KIBIASHARA.

JAMII imeshauriwa kujihusisha na ufugaji wa sungura kibiashara kwani soko lake limeendelea kukua nchini lakini pia imekuwa fursa katika kujikwamua kiuchumi.

Sophia Kingimali
By Sophia Kingimali
03 Sep 2025
VIJANA NCHINI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA YA UFUGAJI SUNGURA KIBIASHARA.

JAMII imeshauriwa kujihusisha na ufugaji wa sungura kibiashara kwani soko lake limeendelea kukua nchini lakini pia imekuwa fursa katika kujikwamua kiuchumi.

Pia,nyama ya sungura imetajwa kuwa na faida kubwa kwa watumiaji ikiwa ni pamoja na kuimarisha ubongo wa mtoto na misuli kwa watu wazima lakini pia husaidia changamoto ya uzazi.

Hayo yamebainishwa leo Septemba 3,2025 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa kampuni ya Saore inayojishughulisha na ufugaji wa sungura, Suleyman Rugarabamu wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu fursa walizokuja nazo katika kuwasaidia wananchi kujikwamua kiuchumi.

Amesema wanatoa mtaji kwa watu watakaochangamkia fursa hiyo ambapo mtu mwenye eneo atajengewa banda la kufuguia na sungura ambao atakaoanza kuwafuga na pindi watakapotimiza kuanzia kilo moja wao kama kampuni watawanunua tena.

"Sisi kama Saore tumejipanga kuhakikisha tunawasaidia watanzania wenzetu wanajikwamua kiuchumi ikiwa ni pamoja na kuweza kusomesha watoto wao kupitia biashara hii ya ufugaji wa sungura sisi tunafanyakazi na makundi matatu ambao wasio na mtaji,walio na mtaji na ambao wanataka kufuga lakini wamebanwa na majukumu sisi tutawafugia na wao watapata faida yao",Amesema.

Aidha amebainishwa kuwa Sungura hao ambao wanatoa kwa wafugaji tayari wamekatiwa bima hivyo mfugaji pindi atakapopewa na ikatokea amekufa atapewa tena sungura mwingine bila malipo yoyote.

Akizungumzia kuhusu faida za sungura hao amesema sungura anauweza wa kuzaa watoto 6 mpaka 16 kwa wakati mmoja na wanauwezo wa kuza a kila mwezi lakini pia mkojo na kinyesu chake kina faida kwani navyo huuzwa.

Kwa upande wake bondia wa ngumi nchini Karim Mandogo ambae ni sehemu ya hamasa kwa vijana amesema vijana wanapaswa kutumia vyema fursa hiyo kwa kujitokeza kwa wingi kuanza kufuga sungura hao kibiashara.

Pia ameongeza kuwa baada ya kujua faida ya ulaji wa nyama hiyo ameahidi kuanza kuitumia japo mara moja kwa wiki ili kuimarisha afya yake pindi atakapopanda ulingoni aweze kuwa imara zaidi.

"Vijana wenzangu jitokezeni kwa wingi Saore mje kuchukua fursa hii unapewa sungura kama mtaji unajengewa banda alafu wakikua wanakuja tena kuwanunua wao wenyewe aisee tusibaki nyuma lakini kuanzia sasa hakuna tena bondia wa kunipiga nitakuwa nawapiga tu nitakula nyama ya Sungura mara kwa mara ili misuli yangu izidi kuwa imara",Amesema Mandoga

Kampuni ya Saore wameanza kufanya kazi hiyo ya ufugaji tangu mwaka 2018 na wameweza kuwafikia watu 6000 ila watu hao walikuwa wanapeana fursa kifamilia na kirafiki lakini sasa wamefungua fursa hiyo kwa jamii yote ya Kitanzania.

MTIHANI WA DARASA LA SABA KUFANYIKA SEPTEMBA 10,WADAU WAASWA KULINDA AMANI NA UTULIVU KIPINDI CHA MITIHANI.

MTIHANI WA DARASA LA SABA KUFANYIKA SEPTEMBA 10,WADAU WAASWA KULINDA AMANI NA UTULIVU KIPINDI CHA MITIHANI.

WATEJA WAKUBWA WA HOTELI MOROGORO WAKAMATWA KWA WIZI WA UMEME.

WATEJA WAKUBWA WA HOTELI MOROGORO WAKAMATWA KWA WIZI WA UMEME.

Mbeya Yafurika Kumuaga Mwanahabari Kadala Komba

Mbeya Yafurika Kumuaga Mwanahabari Kadala Komba

MRADI WA TACTIC KUBADILISHA MANDHARI YA JIJI LA DODOMA

MRADI WA TACTIC KUBADILISHA MANDHARI YA JIJI LA DODOMA

SERIKALI KUGHARAMIA MAZISHI YA WALIOFARIKI KATIKA AJALI YA MGODI NYANDOLWA.

SERIKALI KUGHARAMIA MAZISHI YA WALIOFARIKI KATIKA AJALI YA MGODI NYANDOLWA.