

MAMIA ya wakazi wa Mbeya wamejitokeza kwenye mazishi ya mwanahabari Kadala Komba (35) aliyefariki jumatatu wiki iliyopita wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma.
MAMIA ya wakazi wa Mbeya wamejitokeza kwenye mazishi ya mwanahabari Kadala Komba (35) aliyefariki jumatano tarehe 03 septemba 2025 wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma.
Akihubiri katika ibada iliyofanyika kabla ya mazishi nyumbani kwao Nzovwe Jijinii Mbeya, Mchungaji wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) kutoka Bahi mkoa wa Dodoma, Emmanuel Chibwana alisema kuwa kila mwanadamu anatakiwa kuishi maisha ya kumpendeza Mungu.
"Maisha ya duniani yana mwisho kwa kila mtu,mtu anapokufa mwisho wake unakuwa umefika mwisho,lakini baada ya kifo kuna ukaguzi wa mbinguni, ndio maana duniani kuna nyumba za ibada,"alisema
Alisema kuwa kila mmoja anatakiwa kufanya matendo nema ili apate kuurithi ufalme wa mbinguni.
Alisema kuwa wakati marehemu (Kadala) akiumwa aliomba aongozwe sala ya toba.
"Aliniomba nimuongoze sala ya toba japo alikuwa ameokoka,baada ya maombi alisema wakati wake wa kuondoka umefika,' alisema
Mchungaji Chibwana alisema kuwa jambo hilo hakulielewa na alianza kufunga na kuomba kwa ajili yake,lakini kauli yake ilikuwa wakati wake wa kuondoka umefika.
Kadala alizikwa katika makaburi ya Iwambi yaliyopo kwa Jijini Mbeya.
Akisoma wasifu wa marehemu Mwakilishi wa familia Vicent Mapunda, alisema kuwa marehemu alizaliwa Desemba 23,1990 akiwa mtoto wa kwanza kwenye familia ya watoto saba.
Alipata elimu ya msingi na sekondari mkoani Mbeya kabla ya kujiunga na Chuo cha Uandishi wa habari cha Royal.
Alifanya kazi katika maeneo mbalimbali ikiwemo Dodoma Televisheni.
Marehemu ameacha mume na watoto wawili
MTIHANI WA DARASA LA SABA KUFANYIKA SEPTEMBA 10,WADAU WAASWA KULINDA AMANI NA UTULIVU KIPINDI CHA MITIHANI.
TANESCO YAENDELEA KUBORESHA HUDUMA KWA WATEJA KWA KUNUNUA VITENDEA KAZI VYA USAFIRI
Doyo Aendelea na Kampeni Muheza, Aahidi Kutatua Changamoto za Wananchi.
MWAGO ATEMA CHECHE AHAIDI MAKUBWA AKIPEWA RIDHAA NA WANANCHI JIMBO LA MBAGALA.
UZINDUZI MKUBWA WA KAMPENI JIMBO LA MCHINGA
Mavunde: Nitahakikisha Mtumba Inang’aa Kwa Huduma na Maendeleo
Matumizi ya Nishati Safi Kupikia Yapata Msukumo Mpya
WAZIRI MKUU AWATAKA MADEREVA WA SERIKALI KUFANYAKAZI KWA WELEDI
BRELA YAFANYA KAZI NZURI YA URASIMISHAJI BIASHARA MWANZA
VIJANA NCHINI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA YA UFUGAJI SUNGURA KIBIASHARA.