VIKAO VYA KUANDAA MKUTANO WA 35 WA BARAZA LA KISEKTA LA MAWAZIRI LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI VYAANZA JIJINI ARUSHA. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Tanzania

VIKAO VYA KUANDAA MKUTANO WA 35 WA BARAZA LA KISEKTA LA MAWAZIRI LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI VYAANZA JIJINI ARUSHA.

Vikao vya maandalizi ya Mkutano wa 35 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango na Mkutano Maalum wa 58 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ngazi ya Wataalamu, vimeanza rasmi jana tarehe 31 Agosti, 2025 jijini Arusha.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
01 Sep 2025
VIKAO VYA KUANDAA MKUTANO WA 35 WA BARAZA LA KISEKTA LA MAWAZIRI LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI VYAANZA JIJINI ARUSHA.

Vikao vya maandalizi ya Mkutano wa 35 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango na Mkutano Maalum wa 58 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ngazi ya Wataalamu, vimeanza rasmi jana tarehe 31 Agosti, 2025 jijini Arusha.

Mkutano wa Ngazi ya Wataalam umefunguliwa na kuongozwa na Dkt.Alice Yalla, Katibu wa Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambapo amesisitizia umuhimu wa kutekeleza kwa wakati majukumu watakayojiwekea ili kuweza kufikia malengo ya Jumuiya.

Pamoja na mambo mengine, mkutano huu wa wataalam, unajadili agenda mbalimbali muhimu kuhusu masuala ya mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambazo baadaye ajenda hizo zitawasilishwa kwenye Mkutano wa ngazi ya Makatibu Wakuu kwa majadiliano na hatimaye zitawasilishwa kwenye Mkutano ngazi ya  Mawaziri.

Taarifa zilizopokelewa na kuanza kujadiliwa ni pamoja na mapendekezo na taarifa mbalimbali za Jumuiya, ikiwemo Utekelezaji wa Maamuzi na Maelekezo yaliyopita ya Baraza la Kisekta la Mawaziri wanaoshugnulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango.

Pia mkutano huo utajadili Rasimu ya Mkakati wa Saba (7) wa Maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dira ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Mwaka 2050, Mkakati wa Mageuzi ya Kidigitali wa Mwaka 2025 - 2030, Maandalizi ya Sera ya Lugha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Pamoja na Kalenda ya Majukumu ya Jumuiya kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Desemba, 2025 na hatua iliyofikiwa katika uondoaji wa vikwazo visivyo vya kiforodha Katika Jumuiya.

Mambo mengine yatakayojadiliwa kwa kina katika mkutano huo ni pamoja na hatua iliyofikiwa katika masuala ya Kisiasa ya Nchi Wanachama wa Jumuiya hiyo ya Afrika Mashariki.

Mkutano huu wa ngazi ya wataalam umeanza tarehe 31 Agosti hadi 02 Septemba, 2025, ukifuatiwa na mkutano wa ngazi ya Makatibu Wakuu utakaofanyika tarehe 03 hadi 04 Septemba, 2025 na kisha kuhitimishwa tarehe 05 hadi 06 Septemba, 2025 kwa Mkutano wa 35 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri linaloshughulikia Masuala ya Afrika Mashariki na Mipango.

WAZIRI MKUU AWATAKA TRAMPA KUZINGATIA MAADILI YA KAZI KATIKA UTUNZAJI WA NYARAKA.

WAZIRI MKUU AWATAKA TRAMPA KUZINGATIA MAADILI YA KAZI KATIKA UTUNZAJI WA NYARAKA.

BODI YA BIMA YA AMANA YAPATA MKURUGENZI MKUU

BODI YA BIMA YA AMANA YAPATA MKURUGENZI MKUU

SERIKALI IMEJIPANGA KUIFANYA SEKTA YA USAFIRISHAJI NA UCHUKUZI KISASA ILI KUKUZA UCHUMI WA NCHI.

SERIKALI IMEJIPANGA KUIFANYA SEKTA YA USAFIRISHAJI NA UCHUKUZI KISASA ILI KUKUZA UCHUMI WA NCHI.

WATANZANIA WAASWA KUJITAFAKARI KABLA YA KUCHUKUA MIKOPO.

WATANZANIA WAASWA KUJITAFAKARI KABLA YA KUCHUKUA MIKOPO.

PPAA YASHIRIKI MAONESHO YA NANENANE, KUTOA ELIMU KWA WAZABUNI NA UMMA

PPAA YASHIRIKI MAONESHO YA NANENANE, KUTOA ELIMU KWA WAZABUNI NA UMMA