DKT NCHIMBI AITIKISA KAHAMA AELEZA SABABU YA DKT SAMIA KUCHAGULIWA TENA | The Dodoma Post
The Dodoma Post Siasa

DKT NCHIMBI AITIKISA KAHAMA AELEZA SABABU YA DKT SAMIA KUCHAGULIWA TENA

Mgombea Mwenza wa Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwahutubia Wananchi wa Kahama mjini, jimbo la Kahama, leo Alhamis Septemba 4,2025,mkoani Shinyanga.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
04 Sep 2025
DKT NCHIMBI AITIKISA KAHAMA AELEZA SABABU YA DKT SAMIA KUCHAGULIWA TENA

Mgombea Mwenza wa Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi  akiwahutubia Wananchi wa Kahama mjini, jimbo la Kahama, leo Alhamis Septemba 4,2025,mkoani Shinyanga.

Dkt Nchimbi akihutubia Maelfu ya Wana kahama amesema Dkt Samia anayo kila Sababu ya kupigiwa kura ya ndio katika Uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, kwa Sababu amejipambanua katika Kushughulikia kero na Changamoto mbalimbali za Wananchi, pamoja na kufungua fursa kwa Watanzania.

Pamoja na mambo mengine Dkt Nchimbi pia aliwanadi wagombea Ubunge,akiwemo Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kahama mjini,Benjamin Lukubha Ngayiwa ,pamoja na Madiwani.

Balozi Dkt.Emmanuel Nchimbi anaendelea na mikutano yake ya Kampeni Mkoani Shinyanga ya kuinadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030, ambayo inalenga kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa Maendeleo katika miaka mitano ijayo huku akitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa CCM, Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan, Wabunge na Madiwani wa Chama hicho kwa kura za kishindo ifikapo Oktoba 29,2025.

Doyo Aendelea na Kampeni Muheza, Aahidi Kutatua Changamoto za Wananchi.

Doyo Aendelea na Kampeni Muheza, Aahidi Kutatua Changamoto za Wananchi.

MWAGO ATEMA CHECHE AHAIDI MAKUBWA AKIPEWA RIDHAA NA WANANCHI JIMBO LA MBAGALA.

MWAGO ATEMA CHECHE AHAIDI MAKUBWA AKIPEWA RIDHAA NA WANANCHI JIMBO LA MBAGALA.

UZINDUZI MKUBWA WA KAMPENI JIMBO LA MCHINGA

UZINDUZI MKUBWA WA KAMPENI JIMBO LA MCHINGA

Mavunde: Nitahakikisha Mtumba Inang’aa Kwa Huduma na Maendeleo

Mavunde: Nitahakikisha Mtumba Inang’aa Kwa Huduma na Maendeleo

WAZIRI MKUU AWATAKA MADEREVA WA SERIKALI KUFANYAKAZI KWA WELEDI

WAZIRI MKUU AWATAKA MADEREVA WA SERIKALI KUFANYAKAZI KWA WELEDI