

Mwenyekiti wa bodi Shirika la uwakala wa meli Tanzania(TASAC) Nahodha Mussa Mandia amesema usafiri wa bahari umezidi kuimarika kiulinzi na usalama hali iliyopelekea kuendelea kuchangia katika ukuaji wa uchumi nchini.
Mwenyekiti wa bodi Shirika la uwakala wa meli Tanzania(TASAC) Nahodha Mussa Mandia amesema usafiri wa bahari umezidi kuimarika kiulinzi na usalama hali iliyopelekea kuendelea kuchangia katika ukuaji wa uchumi nchini.
Pia,ametoa rai kwa wananchi kutembelea kwenye banda lao lililopo kwenye maonesho ya sabasaba ili waweze kujifunza namna shirika hilo linavyofanya kazi katika kuhakikisha linalinda usalama katika bahari.
Akizungumza na waandishi wa habari leo julai 5,2025 jijini Dar es salaam kwenye maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba mara baada ya kutembelea banda hilo amesema vitu vingi karibu asilimia 90 vinasafirishwa kwa kutumia bahari.
"TASAC tunajukumu la kuchajiisha watu kushiriki ulinzi na usalama lakini pia usafiri na usafirishaji katika bahari hivyo tupo hapa kwa ajili ya kuelimisha watu kujua ni kiasi gani usafiri wa bahari unachangia katika uchumi wa nchi",Amesema Nahodha Mandia.
Amesema uwepo wa mazingira mazuri katika bahari umepelekea utalii kwa njia ya bahari unakua lakini pia miradi ya mafuta na gesi inaimarika.
"Tunajukumu la kuhakikisha mazingira ya bahari yanatuzwa kwani yasipotuzwa uchumi utaharibika na utalii kwa njia ya bahari pia utaharibika lakini pia miradi ya mafuta na gesi ndani ya bahari itaharibika",amesema.
Ameongeza kuwa usalama wa bahari kwa kiasi kikubwa umeimarika kwani hata matukio ya maharamia yameisha
"Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vinafanyakazi kubwa kuhakikisha usalama katika bahari unaendelea kuimarika hivyo tunavipongeza kwa kazi kubwa wanayoifanya".Ameongeza Nahodha Mandia.
CCM Yatangaza Wagombea Nafasi Ya Ubunge Waliopenya Kwenye Mchujo:Mpina,Makamba Waenguliwa.
KATIBU BAWACHA AJIUNGA CHAUMA ATAJA SABABU YA KUONDOKA KWAKE.
MASLAHI MAPANA YA NCHI YANAZINGATIWA UTEKELEZAJI WA MRADI WA EACOP-DKT. MATARAGIO.
VYAMA VYA SIASA VYAHAKIKISHIWA UWANJA SAWA UCHAGUZI MKUU 2025
INEC YATANGAZA RASMI TAREHE YA UCHAGUZI MKUU 2025.
CCM Yatangaza Wagombea Nafasi Ya Ubunge Waliopenya Kwenye Mchujo:Mpina,Makamba Waenguliwa.
SHUJAA ALIYEPIGANA VITA ASISITIZA AMANI.
VITUO VIWILI VYA KUPUNGUZA KASI YA MAFUTA GHAFI EACOP KUJENGWA NCHINI.
TBC KUAZIMISHA MIAKA 26 YA KUMBUKUMBU YA KIFO CHA HAYATI MWALIMU NYERERE KWA KUENDESHA MASHINDANO YA INSHA KWA WANAFUNZI.
SERIKALI YASIKIA KILIO CHA WANANCHI YAINGIZA SEKTA BINAFSI KUENDESHA MRADI WA MWENDOKASI.