

Sekta ya Uvuvi ni miongoni mwa Sekta za uzalishaji ambayo inatoa ajira za moja kwa moja kwa wavuvi 201,661, wakuzaji viumbe maji 49,084 na takriban watanzania milioni 6 wanajishughulisha na kazi mbalimbali zinazohusiana na uvuvi katika mnyororo wa thamani.
Hayo yameelezwa Mei 6 2025 jijini hapa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Dkt, Ashatu Kijaji wakati akieleza mafanikio ya Miaka minne ya Rais Samia Suluhu Hassan katika ukumbi wa Idara Maelezo.
Hali ya uzalishaji wa mazao ya uvuvi umeongezeka kutoka tani 477,018.84,zenye thamani ya shilingi2,775,798,531.30 katika mwaka 2021, hadi kufikia tani 522,788.33,zenye thamani ya shilingi4,352,735,640.54,katika mwaka 2024.
Aidha, katika kipindi cha kuanzia mwaka 2021 hadi 2024, jumla ya tani 1,951,296.33 za mazao ya uvuvi, zenye thamani ya shilingi 13,647,504,498.08, zilizalishwa kutoka katika maji ya asili.
Serikali imeendelea kuimarisha biashara ya mazao ya uvuvi katika soko la ndani na nje ya nchi ambapo, mauzo ya mazao ya uvuvi na samaki hai wa mapambo yameongezeka kutoka tani 42,302.03za mazao ya uvuvi na samaki hai wa mapambo 181,268zenye thamani ya dola za Marekani 457,817,845,082 kwa mwaka 2021 hadi kufikia tani 59,746.41 za mazao ya uvuvi na samaki hai wa mapambo 148,041zenye thamani ya shilingi 752,969,498,996 mwaka 2024.
"Hivyo, Ongezeko hili limetokana na kuboreshwa kwa mazingira ya biashara ikiwa ni pamoja kufanya mauzo ya mazao ya uvuvi kuongezeka hadi kufikia tani 181,655.7 na samaki hai wa mapambo 729,413 yenye thamani ya shilingi 2,282,092,677,530. na kupungua kwa baadhi ya tozo na kuimarika kwa masoko ya mazao nje ya nchi"
Aidha, ongezeko la thamani ya samaki hai wa mapambo limetokana na kuimarika kwa soko la samaki hai nchi za nje zikiwemo nchi za Poland, Denmark, Ujerumani, Marekani na Uswisi.
Serikali imeendelea na ujenzi wa Bandari ya Uvuvi Kilwa Masoko ambapo hadi kufikia Aprili, 2025 ujenzi huo umefikia asilimia 81.9 na unatarajiwa kukamilika Mwezi Juni mwaka 2025. Mradi huu una thamani ya shilingi bilioni 279.5
Ujenzi huo umejumuishaJengo la kuzalishia barafu, kuhifadhia, kuandalia samaki pamoja na soko la kuuzia samaki; Kituo cha kusambazia maji safi; Kituo cha zimamoto; Kituo cha kupoozea umejumuisha:Ujenzi wa gati lenye urefu wa mita za mraba 315;Jengo la utawala; umeme; Kituo cha kuzalishia gesi ya naitrojeni; Sehemu ya kuegesha magari;Tanki za kuhifadhia mafuta;na karakana ya kutengenezea meli.
Aidha, kukamilika kwa kuchochea uwekezaji katika ujenzi wa viwanda vya kuchakata samaki na miundombinu ya uhifadhi wa mazao ya uvuvi,Pia, meli hizo zitatia nanga kupata na kushusha samaki wanaolengwa na wale wasiolengwa hivyo,Bandari hiyo,pamoja na masuala mengine kutawezesha meli za uvuvi zinazovua mazao ya uvuvi katika Ukanda wa Uchumi wa Bahari yaTanzania (EEZ) na Bahari huduma mbalimbali za kijamii kutoka kwa wafanyabiasha wa ndani ya nchi,Vile vile, jumla ya wananchi 570 wamepata ajira ya moja kwa moja kupitia mradi huu.
Aidha Mwenendo wa uzalishaji wa samaki na viumbe maji wengine katika maji ya asili duniani unaonesha kupungua ukilinganisha na mwenendo wa kuongezeka kwa mahitaji ya samaki na mazao mengine ya ukuzaji viumbe maji.
Washirika wa Maendeleo na Sekta Binafsi umewezesha uzalishaji wa mazao ya ukuzaji viumbe maji kuongezeka kutoka tani 44,735.32
mwaka 2020/2021 hadi tani 124,024.224 mwaka 2024/2025
Vilevile, uzalishaji wa chakula Cha samakikutoka tani 1,182.47 mwaka 2020/2021na kufanya jumla ya tani 123,346.86 ya chakula cha samaki nchini umeongezeka hadi tani 13,859kwa mwaka 2024/2025zilizozalishwa kwa kipindi husika.
EVANCE KAMENGE AJITOLEA KUSAIDIA JAMII KAGERA
SERIKALI KUTEKELEZA MFUKO WA UBUNIFU WA SAMIA “SAMIA INNOVATION FUND” WENYE THAMANI YA BIL 2.3
SERIKALI YAENDELEA KUTOA MAFUNZO KWA WALIMU 70,657 UTEKELEZAJI MITAALA ILIYOBORESHWA, YAANZA MAPITIO SHERIA YA ELIMU
DKT. DORIYE AVISHA VYEO VYA KIJESHI MAAFISA 145 NA ASKARI 476 WA NCAA NA KUSISITIZA UCHAPAKAZI, NIDHAMU, MAADILI NA UZALENDO KATIKA ULINZI WA RASILIMALI.
WAHUKUMIWA MIAKA 20 GEREZANI KWA KUHUJUMU MRADI WA ETDCO
Ibraah Afunguka: "Nilifukuzwa Konde Gang na Harmonize"
Watu Wenye Ulemavu Waomba Kuangaliwa kwa Jicho la Kipekee Katika Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote.
BODI YA ITHIBATI YATAMBULISHWA RASMI BUNGENI
SERIKALI Imeendelea Kujenga na Kuboresha Miundombinu ya Viwanja vya Ndege
MKURUGENZI WA MASOKO TTB AELEZA FURSA INAYOWEZA KUPATA TANZANIA KUTOKA JAPAN KATIKA ELIMU YA UTALII NA UHIFADHI