

Watumishi wa Bodi ya maziwa Tanzania (TDB) waaswa kuzingatia weledi katika kazi zao Kwa kuzingatia usiri Kwa wateja na kufanyia kazi yale yote yenye mapungufu ili kuwa bora zaidi.
Hayo yameelezwa na Kaimu katibu Mkuu Wizara ya mifugo na Uvuvi Dkt.Charles Mhina akizungumza Kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof.Riziki Shemdoe wakati akizungumza na watumishi wa Bodi ya maziwa katika kikao kazi Cha kuboresha ufanyaji kazi kwa watumishi hao.
Aidha amesema Kuna umuhimu wa kila mtumishi kutekeleza majukumu yake kutokana na mpango mkakati wa taasisi,kutaka kujua kanuni za utumishi na misingi ya utawala Bora.
"Kwa kufanya hivyo tutapunguza malalamiko kwa wateja wetu maana watu wanadhani watumishi ndio huwa wanalalamika lakini ukweli ni kwamba wadau wetu ndio watoa taarifa kulingana na huduma zetu"
"Tunapaswa kuwa waaminifu kwa mteja pamoja na kuwajibika ipasavyo ili kuwaridhisha wateja au wadau tunaowahudumia, Kila mtumishi anapaswa kujiuliza je anafanya kazi yake vizuri na ni Kwa namna gani umetoa huduma bora kwa wateja wako na watumishi wenzio"
Aidha ameongeza kuwa Kila mtu Kwa nafasi yake ana umuhimu mkubwa sana,na wao kama Wizara wanathamini jitihada za watumishi kukutana na kujadili changamoto zote na kuzitafutia ufumbuzi.
"Niwapongeze kwa kitendo hichi Cha kukutana pamoja kwani itawajengea uzoefu mkubwa na kufanya kazi Kwa weledi unaotakiwa na kutoa huduma Kwa wakati,kama huduma inapaswa kutolewa ndani ya siku 3 basi iwe ivyo ili Kujenga uaminifu kwa mteja wako sababu usipofanya kwa wakati tayari unapoteza uaminifu,hivyo nitoe Rai kila mmoja kufanya majukumu yake kwa wakati"
Sanjari na hayo amesema si vizuri kutoa huduma Kwa upendeleo,sio unatoa upendeleo kwa taasisi nyingine na kuacha nyingine upendeleo wa aina yoyote hautaruhisiwa kwani ni ukiukwaji wa maadili na misingi ya utumishi wa Umma.
"Niwaombe kuacha kutoa Siri za taasisi kama wewe sio msemaji wa taasisi sio vizuri kutoa taarifa ambazo sio sahihi maana saivi watu wanapenda kusambaza na kupotosha taarifa ambazo sio sahihi na zinaleta taharuki kwenye jamii jambo ambalo sio sawaa na unakuwa mtumishi ambaye sio mwadilifu"
Kwa upande wake Msajili wa Bodi ya maziwa Tanzania Prof.George Msalya amesema wana mpango wa Kuanzisha Baa za maziwa ili ziweze kusaidia watu ambao hawako huru kwenda sehemu zingine ambapo zitajulikana kama(milk zone).
Aidha amesema Bodi ya maziwa inafanya kazi kama taasisi huru kwani bado haijaungana na bodi ya nyama hivyo bado wanaendelea kujinoa na kuhakikisha wanakuwa bora zaidi kama taasisi.
Sio Lazima Kila Mhitimu Aajiriwe na Serikali: Waziri Simbachawene.
Waziri Simbachawene "Sio Lazima Kila Mhitimu Aajiriwe na Serikali"
TASAC YAWAJENGEA UWEZO MAWAKALA WA MELI, FORODHA NA WAKUSANYAJI NA WATAWANYAJI WA MIZIGO MWANZA.
Awamu ya pili uboreshaji, uwekaji wazi wa dafatri la wapiga kura kuanza mei.
NYONGO: SEKTA BINAFSI INA MCHANGO MKUBWA KWA TAIFA.
PPAA yawanoa wazabuni Kanda ya Kaskazini
NIDA KUSITISHA MATUMIZI YA NAMBA ZA UTAMBULISHO (NINs) KWA WASIOCHUKUA VITAMBULISHO VYAO.
DrKumbuka Afunguka Kuhusu Kuvunjika kwa Ndoa ya Haji Manara na Zaiylissa
Shule mpya ya wavulana kugharimu zaidi ya bilioni tatu
WADAU WA UNUNUZI WAASWA KUZINGATIA MAADILI KAZINI