

Wajumbe zaidi ya 137 kutoka nchi mbalimbali barani Afrika waliokuwa wakihudhuria mkutano mkuu wa 73 wa Baraza la Viwanja vya Ndege Afrika leo Aprili 30, 2025, wamefanya ziara katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro na kufurahia vivutio vya utalii vilivyoko katika hifadhi hiyo
Ziara hiyo ambayo imefanyika baada ya kumalizika kwa Mkutano mkuu wa Baraza hilo uliofanyika jijini Arusha kuanzia Aprili 24 hadi 30, 2025 imelenga kuunga mkono jitihada za Serikali na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kuhamasisha utalii na kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo Ngorongoro na maeneo mengine ya nchi.
Akizungumza wakati wa kupokea ugeni huo, Afisa uhifadhi Mkuu kutoka Idara ya Huduma za Utalii na Masako Peter Makutian, amesema kuwa kutokana na jitihada zinazofanywa na Mamlaka za kuhamasisha utalii ndani na nje ya nchi wamekuwa wakipokea makundi makubwa ya watalii ambao wamekuwa wakivutiwa kutembelea vivutio mbalimbali ikiwemo kreta ya Ngorongoro inayotajwa kuwepo kwenye maajabu saba ya Asili barani Afrika.
“Leo tumepokea wageni kutoka baraza la viwanja vya ndege ambao wamevutiwa kuja kutembelea vivutio vya utalii Hifadhi ya Ngorongoro, tunaamini ujio wa ugeni huu utaendelea kuhamasisha utalii kutoka kwa wageni wa ndani na nje nchi, wametembelea kreta ya Ngorongoro na maeneo mengine ambapo wamejionea Wanyama mbalimbali, vivutio vya malikale, uoto wa asili na mandhari mbalimbali ” Alisema Makutian
Kwa upande Bi. Violeth Mfuko ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Viola Tours & Travel limited iliyoratibu ziara hiyo alieleza kuwa, vivutio ambavyo vinapatikana ndani ya Eneo la Ngorongoro hasa Bonde la Kreta na maeneo mengine ambayo yamekuwa kivutio cha kipekee kwa watalii wengi kuwa na shauku kubwa ya kutembelea maeneo hayo kutokana na uzuri wake wa asili na kuwa eneo la urithi wa dunia lenye uhifadhi endelevu.
Katika hatua nyingine, NCAA imetumia fursa hiyo kuhamasisha wageni wa baraza hilo kulipigia kura eneo la Hifadhi ya Ngorongoro linalowania tuzo ya kuwa Kivutio Bora cha Utalii Barani Afrika kupitia tuzo ambazo zinaratibiwa na mtandao wa World Travel Awards.
Maiko Salali Arejesha Fomu ya Kugombea Ubunge Jimbo la Mpwapwa, Apongeza CCM kwa Ujumuishwaji wa Makundi Maalum
DIB YAHIMIZA WANANCHI KUDAI FIDIA ZAO KUTOKA BENKI ZILIZOFILISIKA
USHIRIKI WA TAWA KATIKA MAONESHO YA 49 YA BIASHARA YA KIMATAIFA
DWIGHT DANDA KIJANA MDOGO NA MHITIMU WA CHUO KIKUU ATIA NIA UBUNGE KIBAMBA
BoT YAWATAKA TAMFI NA TAMIU KUBORESHA UPATIKANAJI WA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA.
Aliyeongoza kura maoni Vunjo 2020, kumkabili tena Dkt. Kimei
Maiko Salali achukua fomu ya ubunge Jimbo la Mpwapwa
Serikali kufanya mageuzi ya kimtazamo katika nafasi za uongozi kwa wanawake
Dkt.Tulia Aweka Jiwe La Msingi Ujenzi wa Shule ya Wavulana Bunge.
Mavunde Akabidhi Jengo la kupumzikia Wananchi Hospitali ya Rufaa ya Dodoma