BENKI KUU YAWAGEUKIA WATENGENEZAJI, WAUZAJI ‘PUTTY’ | The Dodoma Post
The Dodoma Post Tanzania

BENKI KUU YAWAGEUKIA WATENGENEZAJI, WAUZAJI ‘PUTTY’

Benki kuu ya Tanzania imewataka wadau wanaojishughulisha na utengenezaji na usambazaji wa saruji ya ukuta ‘wall putty’ nchini kuacha kuweka fedha taslimu katika mifuko ya saruji kama sehemu ya kuwavutia wateja.

The Dododma Post
By The Dododma Post
10 Jan 2025
BENKI KUU YAWAGEUKIA WATENGENEZAJI, WAUZAJI ‘PUTTY’

Benki Kuu imetoa katazo hilo ilipokutana na wadau hao katika ofisi za Makao Makuu Ndogo ya Benki Kuu, Dar es Salaam, Januari 10, 2024 na kuwapa elimu ya utunzaji wa fedha na alama za usalama katika noti za Tanzania.

Wadau hao wamehimizwa kutunza vizuri sarafu na noti ili ziweze kukaa muda mrefu katika mzunguko na kuipunguzia serikali gharama kubwa inayotumia kutengenza na kuzichapisha.

Ili kutunza vizuri noti, wananchi wametakiwa kuepuka kuzikunja, kuzitoboa na kuziweka katika maeneo yenye unyevunyevu kwani kufanya hivyo kunachangia kwa kiasi kikubwa kuchakaza fedha kwa haraka.

Namna sahihi ya kutunza noti hizo ni kwa kuzihifadhi sehemu ambayo zinanyoka, haswa katika pochi (wallet) kwani kwa kufanya hivyo, noti zitaweza kudumu kwa muda mrefu katika mzunguko, amesema Bw. Erick John wakati akitoa mafunzo hayo ya alama za usalama katika fedha zetu.

Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo wameishukuru Benki Kuu kwa kuwapa elimu hiyo na kuomba wadau zaidi waweze kufikiwa.

Aidha, kuhusu zoezi la uondoaji wa matoleo ya zamani ya fedha katika mzunguko, Bw. Erick amewahimiza wananchi wote wenye fedha zilizoainishwa katika tangazo la serikali kuzipeleka Benki Kuu au benki za biashara ili waweze kubadilishiwa na kupewa fedha zinazoendelea kuwa katika mzunguko, kwa thamani ya fedha watakazopeleka.

Zoezi la ukusanyaji wa fedha za zamani limeanza Januari 6, 2025 na litatamatika Aprili 5, 2025. Baada ya hapo, fedha zote zilizotangazwa kuondolewa katika mzunguko zitakosa uhalali wa kutambulika katika matumizi.

PBPA  YASHAURI UJENZI WA MATENKI YA MAFUTA BANDARI YA MBAMBA BAY

PBPA YASHAURI UJENZI WA MATENKI YA MAFUTA BANDARI YA MBAMBA BAY

WATU WENYE ULEMAVU WAMEPATA UFADHILI KWA AJILI YA KUWAWEZESHA KATIKA MASWALA YA UONGOZI NA KUKUZA DEMOKRASIA.

WATU WENYE ULEMAVU WAMEPATA UFADHILI KWA AJILI YA KUWAWEZESHA KATIKA MASWALA YA UONGOZI NA KUKUZA DEMOKRASIA.

RAIS SAMIA APELEKA KICHEKO KWA WANANCHI WA SONGWE

RAIS SAMIA APELEKA KICHEKO KWA WANANCHI WA SONGWE

SERIKALI YATAKA MAFANIKIO SEKTA YA MAJI YALINDWE

SERIKALI YATAKA MAFANIKIO SEKTA YA MAJI YALINDWE

CCM YASHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA.

CCM YASHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA.