KOREA KASKAZINI YAWANASA ‘SNIPER’ UKRAINE, YADAI RUSSIA INAWAUA MAJERUHI | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kimataifa

KOREA KASKAZINI YAWANASA ‘SNIPER’ UKRAINE, YADAI RUSSIA INAWAUA MAJERUHI

Kyiv. Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amesema dunia inapaswa kufahamu kuwa Shirika la Ujasusi la Ukraine (SBU) limewakamata na linawafanyia mahojiano wanajeshi wawili raia wa Korea Kaskazini.

The Dododma Post
By The Dododma Post
12 Jan 2025
KOREA KASKAZINI YAWANASA ‘SNIPER’ UKRAINE, YADAI RUSSIA INAWAUA MAJERUHI

Zelenskyy alitoa taarifa hiyo jana Jumamosi kupitia akaunti yake ya Telegram kuwa wanajeshi hao wa Korea Kaskazini wenye majeraha makubwa mwilini walikamatwa na vikosi vya Ukraine wakiwa wamejificha eneo la Mkoa wa Kursk.

“Wanajeshi wawili wanaendelea kupatiwa msaada wa matibabu ya msingi na wako chini ya Ulinzi wa Shirika la Ujasusi la Ukraine (SBU) jijini Kyiv,” alisema Zelenskyy.

Rais huyo alisema anajisikia furaha na kujivunia wanajeshi wake wanaoendelea na Operesheni katika eneo la Kursk sambamba na kufanikisha kukamatwa kwa wanajeshi hao wa Korea Kaskazini kwa kile alichodai ndiyo njia pekee ya kuifanya dunia ifahamu kinachoendelea eneo la mapigano.

Aliongeza kuwa "Haikuwa kazi nyepesi kuifanya kuwatia mbaroni wanajeshi hawa,”  huku akisema vikosi vya Russia vimekuwa vikiwaua wanajeshi waliojeruhiwa ili kufuta ushahidi wa uwepo wa wanajeshi kutoka nchini Korea Kaskazini wanaopigana dhida ya Ukraine.

SBU ilisema katika taarifa yake kuwa wafungwa hao wa kivita walikamatwa Januari 9, mwaka huu, baada ya kukamatwa walipatiwa huduma zote za Msingi ikiwemo matibabu kwa Mkataba wa Geneva.

"Wanashikiliwa na wanaendelea kupatiwa huduma za msingi huku wakihojiwa chini ya sheria za Kimataifa,” imesema taarifa ya Shirika hilo la Ujasusi nchini Ukraine.

SBU ilisema mahojiano ya wanajeshi hao wasiyojua kuzungumza lugha ya Ukraine, Kingereza wa Kurussia, yanafanyika chini ya msaada wa wakalimani wanaozungumza Kikorea kwa ushirikiano na Shirika la Ujasusi la Korea Kusini (NIS).

Katika taarifa yake aliyoichapisha kwneye mtandao wa Telegram na X, Zelensky alisema wanajeshi hao walikuwa wakifanyiwa mahojiano na SBU na ameagiza vyombo hivyo vya ujasusi kuwaruhusu waandishi wa habari kuwaona na kuandika habari kuhusiana na wanajeshi hao.

"Dunia inapaswa kufahamu ukweli wa nini kinaendelea,” alisema Zelenskyy akiambatanisha chapisho lake na picha za wanajeshi wawili wenye majeraha, huku picha nyingine ikionyesha Kitambulisho cha Jeshi la Russia.

Kwa mujibu wa Kitambulisho hicho cha mmoja wa wanajeshi hao, kinaonyesha amezaliwa Turan, Jamhuri ya iliyoko karibu na taifa la Mongolia.

SBU ilisema kuwa baada ya kuwakamata, mwanajeshi mmoja alikutwa na Kitambulisho cha Jeshi la Russia kilichotolewa kwa jina la mtu mwingine ambaye ni mzaliwa wa taifa la Tuva huku mwingine akikutwa hana kitambulisho chochote.

MABADILIKO YA SERA YA ELIMU KUAKISI MABADILIKO YA KITAIFA NA KIMATAIFA.

MABADILIKO YA SERA YA ELIMU KUAKISI MABADILIKO YA KITAIFA NA KIMATAIFA.

MAREKANI HALI TETE, MOTO WAUA 16 LOS ANGELES, UPEPO WATARAJIWA KUONGEZEKA

MAREKANI HALI TETE, MOTO WAUA 16 LOS ANGELES, UPEPO WATARAJIWA KUONGEZEKA

Maria Sarungi atekwa Kenya wasiojulikana watajwa

Maria Sarungi atekwa Kenya wasiojulikana watajwa

Moto watekeza mitaa, makazi Los Angeles, Marekani

Moto watekeza mitaa, makazi Los Angeles, Marekani