

KAMATI ya Sera ya Fedha (MPC) ya Bodi ya Wakurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania, imeamua Riba ya Benki Kuu (CBR) kuendelea kuwa asilimia 6 kwa robo mwaka itakayoishia Septemba 2024 ambapo Uamuzi huu umefikiwa katika kikao cha Kamati kilichofanyika tarehe 3 Julai 2024.
KAMATI ya Sera ya Fedha (MPC) ya Bodi ya Wakurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania, imeamua Riba ya Benki Kuu (CBR) kuendelea kuwa asilimia 6 kwa robo mwaka itakayoishia Septemba 2024 ambapo Uamuzi huu umefikiwa katika kikao cha Kamati kilichofanyika tarehe 3 Julai 2024.
Akisoma taarifa hiyo leo julai 4 jijini Dar es Salaam Naibu Gavana wa BoT wa sera za uchumi na Fedha, Dk. Yamungu Kayandabila kwa niaba Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania BoT, Emmanuel Totuba ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Sera ya Fedha amesema uamuzi huo umefanikiwa katika kikao kili chokfanyika jJulai,3 2024 tathimini ya kamati kuhusu mwelekeo wa uchumi na vihatarishi mblimbali inaonesha kwamba utekelezaji wa sera ya fedha kwa kipi cha Januari hadi Juni mwaka huu wamefanikiwa kudhibiti mfumuko wa bei na kubaki chini ya lengo la asilimia 5.
"Kamati ya Sera ya Fedha MPC ya Bodi ya Wakurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania imeamua riba ya Benki Kuu CBR kuendelea kuwa asilimia 6 kwa robo mwaka itakayoisha Septemba mwaka huu,"amesema Dk. Kayandabila.
Amesema maamuzi ya kamati yamezingatia mtazamo chanya wa uchumi wa dunia ambapo matarajio ni kuendelea kupungua kwa mfumuko wa bei katika nchi nyingi kuimarika kwa ukwasi katika msoko ya fedha duniani na kushuka kwa bei za bidhaa katika soko la dunia.
Amesema Kamati hiyo inatarajia uchumi wa ndani kuendelea kukua kwa kasi na upatikanji wa chakula cha kutosha na kupungua kwa kasi ya kushuka thamani ya shilingi kufuatia ongezeko la mapato ya fedha za kigeni kutokana na shughuli za utalii,pamoja na mauzo ya dhahabu na mazao ya biashara na chakula.
"Katika kuthamini mwenendo wa uchumi wa dunia kamati imebaini kuimarika kwa shughuli za kiuchumi katika nchi nyingi kwa robo ya kwanza na ya pili ya mwaka 2024.Mfumuko wa bei unaendelea kupungua na kuimrika kwa ukwasi katika masoko ya fedha duniani na Benki Kuu katika nchi nyingi kuanza kupunguza viwango vya riba ikiwemo bei ya mafuta ghafi licha ya kuongezeka kidogo mwishoni mwa mwezi Juni 2024 huku bei ya dhahabu inaendelea kuwa juu ikiashiria dhahabu kuendelea kutumika kama uwekezaji mbadala katika mazingira y kushuka kwa thamani ya sarafu mbalimbali kutokan na migogoro ya kisiasa duniani,"ameeleza.
Amesema kuwa matarajio ni uchumi wa dunia kuendelea kuimarika kwa kipindi kilichobaki cha mwaka 2024/2025 pamoja na kuwepo kwa hatari ya kuongezeka kwa migogoro ya kisiasa na mizozo ya kibiashara.
Aidha Dk. Kayandabala amesema kuhusu mwenendo wa uchumi nchini kamati imeridhishwa na kuendelea na kuimarika kwa shuguli za kiuchumi kutokana na utekelezaji wa sera thabiti na maboresho mbalimbali yenye lengo la kukuza uchumi.
TUNALAANI WOTE WANAOHAMASISHA MAANDAMANO- MALAIGWANAN K'NJARO
RC MAKALLA AZINDUA MSIMU WA SHEREHE ZA MILA ZA KIMASAI
KAMATI YA ULINZI NA USALAMA TANGA YATOA ONYO KWA WATU WANAOPANGA KUVUNJA AMANI SIKU YA UCHAGUZI
JIJI LA DAR ES SALAAM NI SHWARI,JITOKEZENI KUPIGA KURA:RC CHALAMILA.
VIONGOZI WA DINI WAHIMIZA WATANZANIA KUPIGA KURA KWA AMANI.
PADRI NIKATA ALIJIPOTEZA KUTOKANA NA MSONGO WA MAWAZO NA KUACHWA NA MPENZI WAKE- POLISI
DOWOSA Yawaokoa Wanawake Dodoma Kutoka Mikononi mwa “Kausha Damu”
Vijana sasa kujifunza ufundi kwa urahisi kupitia programu ya VSOMO ya VETA
CHALAMILA: WATAKAOJIZIMA DATA OKTOBA 29, TUTAWAFANYA NETWORK ZISOME
RC MAKALLA AWAHAKIKISHIA USALAMA WAZEE WA MKOA WA ARUSHA SIKU YA UPIGAJI KURA OKTOBA 29.