RC MAKALLA AZINDUA MSIMU WA SHEREHE ZA MILA ZA KIMASAI | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

RC MAKALLA AZINDUA MSIMU WA SHEREHE ZA MILA ZA KIMASAI

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla leo Jumatatu Oktoba 20, 2025, amezindua sherehe za msimu wa tohara kwa jamii ya Kimasai nchini Tanzania, akiishukuru Jamii hiyo kwa kuheshimu sheria na Miongozo ya nchi kwa kusimamisha shughuli za Tohara Oktoba 29, 2025 ili kuruhusu Makundi rika mbalimbali kwenda kupiga kura kuwachagua Viongozi wanaowataka kuwaongoza kwa miaka mitano ijayo.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
20 Oct 2025

Sherehe hizo maarufu kama Enkipaata zimezinduliwa kwenye Kijiji cha Oldonyosapuk Wilaya ya Arumeru zikitarajiwa kuhusisha zaidi ya Vijana 2,000 wa kundi rika la Irmegoliki litakalodumu mpaka Oktoba 2032, akiwahakikishia usalama na amani wakati wote kuanzia sasa, siku ya upigaji wa kura na baada ya upigaji kura pamoja na kuwahimiza wananchi wote kushiriki kuchagua Viongozi wanaowataka katika uchaguzi huo.

"Ninawashukuru kwanza kwa kunipa heshima ya kuzindua sherehe hizi na zaidi ni kwamba pamoja na kuwa na mila zenu bado mmeheshimu taratibu na ratiba nyingine za serikali niwaombe tarehe 29 Viongozi wote mpaze sauti katika maeneo yote watu wapate haki ya kupiga kura na sisi kama Serikali tuwahakikishie kuwa uchaguzi utakuwa salama na wenye amani." Amesema Mhe. Makalla.

Kwa upande wake Kiongozi Mkuu wa Jamii ya Kimasai Isack Meijo Ole Kisongo na Mlezi wa kundi rika hilo linaloingia kwenye msimu wa tohara wamesema sababu ya kuiheshimu Oktoba 29, 2025 ni kutokana na Jamii hiyo kutambua umuhimu wa upigaji wa kura, wakiahidi kuwa Jamii kinara katika kumpa kura nyingi zaidi Mgombea wa nafasi ya Urais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na mapenzi yao kwake na maendeleo mengi aliyowatendea jamii ya Kimasai nchini katika sekta ya jamii na ufugaji.

JIJI LA DAR ES SALAAM NI SHWARI,JITOKEZENI KUPIGA KURA:RC CHALAMILA.

JIJI LA DAR ES SALAAM NI SHWARI,JITOKEZENI KUPIGA KURA:RC CHALAMILA.

VIONGOZI WA DINI WAHIMIZA WATANZANIA KUPIGA KURA KWA AMANI.

VIONGOZI WA DINI WAHIMIZA WATANZANIA KUPIGA KURA KWA AMANI.

BODABODA NA MACHINGA HATUTAKUWA CHANZO KUVUNJA AMANI YETU

BODABODA NA MACHINGA HATUTAKUWA CHANZO KUVUNJA AMANI YETU

CWT YATOA WITO KWA WALIMU KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU NA KUELEIMISHA JAMII KUHUSU UMUHIMU WA KUPIGA KURA

CWT YATOA WITO KWA WALIMU KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU NA KUELEIMISHA JAMII KUHUSU UMUHIMU WA KUPIGA KURA

Hakuna Maendeleo Bila Amani, Hakuna Taifa Imara Bila Mshikamano - Dkt. Judith

Hakuna Maendeleo Bila Amani, Hakuna Taifa Imara Bila Mshikamano - Dkt. Judith