

MAMLAKA ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), imepongezwa kwa kasi kikubwa cha urejeshaji wa miundombinu ya reli iliyoharibiwa.
MAMLAKA ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), imepongezwa kwa kasi kikubwa cha urejeshaji wa miundombinu ya reli iliyoharibiwa.
Pongezi hizo zimetolewa na Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile, katika ziara yake ya ya kukagua urejeshwaji wa miundombinu na huduma za usafiri wa treni ya Tazara kwa kipande cha Ifakara mpaka Lumumwe.
Amesema shughuli hizo zilisimama kupisha urekebishaji wa miundombinu iliyoharibiwa kutokana na mvua zilizonyesha nchini.
"Nitumie nafasi hii kuwapongeza kwa kazi kubwa mliyoifanya, wakati ule nilikuja kwa helikopta miundombinu haikuruhusu kufika hapa ila safari hii nimekuja na kiberenge nimejionea tayari panafikika na kazi kubwa imeshafanyika na changamoto zote mlizosema nimezichukua,”amesema.
Kihenzile ameeleza lengo la ziara hiyo ni kuona maendeleo yaliyofikiwa na kitu kinachotakiwa kuongezwa nguvu kuhakikisha usafiri wa reli hiyo ya kihistoria ya Tazara unarejea kama ilivyokuwa awali kutoka Dar es Salaam hadi Kapiri Mposhi nchini Zambia.
"Pamoja na kufurahia kazi nzuri iliyofanyika hapa, nimeona treni za mizigo zimeanza kupita, ninatoa maelekezo tena kwa Tazara simamieni maeneo yote yaliyobakia kuhakikisha reli yote inarudi katika hali yake huku tukizingatia usalama wa abiria na mizigo ili usafirishaji wa abiria uanze mara moja,” amesisitiza.
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Dunstan Kyobya amemshukuru Kihenzile kwa ufuatiliaji wa maendeleo ya urejeshwaji wa miundombinu ya reli hiyo.
Amesema wilaya hiyo itahakikisha miundombinu inakamilika kwa wakati na huduma zinarejea kwa wananchi.
Akizungumzia maendeleo ya urejeshaji wa miundombinu kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Tazara, Kelvin Kyara ameishukuru Wizara ya Uchukuzi kwa kuendelea kutoa fedha na kusimamia kwa karibu utekelezaji wa ukarabati huo ambao uko mwishoni kukamilika, kurejesha huduma zilizosimama kwa zaidi ya mwezi mmoja
Sio Lazima Kila Mhitimu Aajiriwe na Serikali: Waziri Simbachawene.
Waziri Simbachawene "Sio Lazima Kila Mhitimu Aajiriwe na Serikali"
TASAC YAWAJENGEA UWEZO MAWAKALA WA MELI, FORODHA NA WAKUSANYAJI NA WATAWANYAJI WA MIZIGO MWANZA.
Awamu ya pili uboreshaji, uwekaji wazi wa dafatri la wapiga kura kuanza mei.
NYONGO: SEKTA BINAFSI INA MCHANGO MKUBWA KWA TAIFA.
NIDA KUSITISHA MATUMIZI YA NAMBA ZA UTAMBULISHO (NINs) KWA WASIOCHUKUA VITAMBULISHO VYAO.
Shule mpya ya wavulana kugharimu zaidi ya bilioni tatu
Chama Cha Mawakili wa Serikali kufanya mkutano Aprili 14-15 jijini Dodoma
WADAU WA UNUNUZI WAASWA KUZINGATIA MAADILI KAZINI
Watumishi wa Bodi ya maziwa waaswa kuzingatia weledi katika kazi zao.