TARURA KUTUMIA TEKNOLOJIA MBADALA KUIMARISHA MTANDAO WA BARABARA. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Tanzania

TARURA KUTUMIA TEKNOLOJIA MBADALA KUIMARISHA MTANDAO WA BARABARA.

Wakala wa barabara Vijijini na mijini (TARURA) inaendelea kutumia Teknolojia mbadala katika kuimarisha mtandao wa barabara ikiwemo ujenzi wa madaraja imara na madhubuti kwa kutumia mawe.

Sophia kingimali
By Sophia kingimali
28 May 2024
TARURA KUTUMIA TEKNOLOJIA MBADALA KUIMARISHA MTANDAO WA BARABARA.

Wakala wa barabara  Vijijini na mijini (TARURA) inaendelea kutumia Teknolojia mbadala katika  kuimarisha mtandao wa barabara ikiwemo ujenzi wa madaraja imara na madhubuti kwa kutumia mawe.

Akizungumza na waandishi wa habari Mei 27,2024 jijini Dar es salaam katika banda la maonesho la TARURA kwenye mkutano wa 30 wa wahandisi Afrika.Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhandisi Rogatus Mativila amesema Teknolojia ya mawe imeweza kuwa mkombozi kwa kusaidi kupunguza gharama za ujenzi.

“TARURA wanaonesha utaalamu wanafanya ikiwemo ujenzi wa ‘structure’ mbalimbali za kupitishia maji, wanajenga kwa mawe teknolojia hii inasaidia inapunguza gharama za ujenzi lakini pia miundombinu hiyo inadumu kwa muda mrefu,” amesema.

Akizungumzia namna Serikali ilivyojipanga kurejesha miundombinu iliyoharibiwa na mvua zilizoanza kunyesha tangu Oktoba, 2023 na kuendelea hadi sasa, Mativila amebainisha kuwa bado kuna sehemu nyingi mvua  zinaendelea kunyesha, miundombinu mingi imeharibika, mvua zilizokuja hazikuwa za kawaida kama miaka mingine hivyo pindi mazingira yatakapokauka urejeshaji utaanza mara moja.

Amesema kufuatia tathimini iliyofanyika  kiasi cha Tsh. Bil.  2 zinahitajika kurejeresha miundombinu iliyoharibiwa na mvua na Serikali ipo tayari kutoa fedha hizo

Kwa upande wake Msimamizi wa Teknolojia Mbadala TARURA – Makao Makuu Mhandisi Mshauri Pharels Ngeleja amesema tayari wamejenga madaraja 256 kwa teknolojia ya mawe yaliyogharimu Tsh. Bil. 13.

I “Hii Teknolojia ya mawe tunaitumia pia kujenga barabarani, kuna Km. 26.18 zimekamilika Mkoani Mwanza, Kigoma na Rukwa, pia kwenye barabara zetu zingine tunatumia teknolojia za Ecoroad, Ecozyme na Polymer”.

“Tumejenga barabara ya Sawala Km. 13 Mkoani Iringa, Chamwino - Dodoma pia tunaendelea na hizi teknolojia, Dodoma  barabara ya daraja dogo tumekamilisha na Miradi hii ipo maeneo mbalimbali nchi na tunaendelea nayo” amesema Mhandisi Ngereja.

Aidha ameongeza kuwa  kupitia kitengo cha mambo ya mazingira wanaendelea pia kufuatilia kwa ukaribu athari za mabadiliko ya tabia nchi ili kujiimarisha zaidi katika ujenzi wa miundombinu yake.

TARURA imeweza kujenga barabara kwa kutumia teknolojia ya Ecoroad, Ecozyme na Polymer katika barabara ya Chamwino Km. 7,Itilima Km. 5, Sawala-Mkonge Km. 10 na Daraja dogo -Dodoma Km.1.

UBORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA KUANZA TAREHE 20 JULAI, 2024 KIGOMA

UBORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA KUANZA TAREHE 20 JULAI, 2024 KIGOMA