

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amewaagiza Waziri wa Viwanda na Biashara Dk.Ashatu Kijaji na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo kuhakikisha mradi wa chuma wa liganga unaanza uzalishaji na malighafi hiyo itumike kwenye viwanda vya hapa nchini.
RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amewaagiza Waziri wa Viwanda na Biashara Dk.Ashatu Kijaji na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo kuhakikisha mradi wa chuma wa liganga unaanza uzalishaji na malighafi hiyo itumike kwenye viwanda vya hapa nchini.
Akizungumza leo Mei, 9,2024 jijini Dar es Salaam Dk. Samia wakati akizindua kiwanda cha kuunganisha malori na matipa cha Surtun kilichopo Kisarawe II Wilaya ya Kigamboni uliohudhuliwa na viongozi mbalimbali wa Serikali,Taasisi na Dini.
Amesema Malighafi zinazopatikana katika mradi wa chuma wa liganga utasaidia utengenezaji wa vipuri na bidhaa nyingine zinazozalishwa na viwanda vya ndani.
"Mradi huu ni muhimu kwa uchumi wa viwanda vya chuma na amewataka mawaziri hawa kuhakikisha wanapata muwekezaji mzuri atakayechimba chuma hicho na kisha kitumike kwenye viwanda vingine,"amesema Dk.Samia.
Amesema serikali itaendelea kujenga uchumi wa kisasa funganishi na jumuishi na shindani katika msingi wa Viwanda, huduma za kiuchumi na miundombinu wezeshi.
Amesema sekta ya viwanda inaongoza uzalishaji na kutoa ajira kwa wananchi jambo ambalo ni muhimu katika kukuza kusaidia katika mapambano ta kuondoa umaskini
Dk. Samia amesema serikali imepunguza kodi ya makapuni kutoka asilimia 30 hadi asilimia 10 kwa kipindi cha miaka mitano ya mwanzo ili kuchochea uwekezaji zaidi kwenye sekta ya viwanda.
"Kiwanda hiki ni chachu ya ukuaji wa viwanda na sekta nyingine kwa kuwa kutumia vioo vinavyozalishwa na kiwanda kingine ambacho zaidi ya asilimia 89 ya malighafi zake zinapatikana hapa nchini,"amesema.
Pia Dk. Samia amesema matumizi ya bidhaa zinazozalishwa nchini zinapunguza gharama kwa kampuni zenyewe zinazotengeneza magari na inaongeza manufaa ya uwepo wa kampuni hiyo kwa uchumi wa nchi.
Ameongeza kuwa kiwanda hicho kimetoa ajira za moja kwa moja 250 na zisizo rasmi 1800 kuongeza mzunguko wa fedha, mapato ya serikali na kuhaulisha teknolojia.
Naye Waziri wa Viwanda na Biashara Dk.Ashatu Kijaji, amesema uamuzi wa serikali wa kulipa fidia wananchi wanaozunguka mradi wa madini ya vioo wa Engaruka uliopo Wilaya ya Monduli mkoani Arusha.
Amesema malighafi zitapatikana katika mradi huo zitatosheleza kwa zaidi ya asilimia 99 viwanda vya vioo hapa nchini.
" Mradi huu ni muhimu kwa uchumi wa viwanda vya vioo na kwamba hatakuwa na haja ya kuagiza malighafi nje ya nchi,"amesema Dk. Kijaji.
Amesema hatua hiyo ya serikali ni ushindi mkubwa kwa uwekezaji na uzalishaji wa bidhaa za vioo hasa viwanda vilivyopo nchini.
Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mpango na Uwekezaji , Profesa Kitila Mkumbo amesema katika miaka mitatu iliyopita uchumi wa Tanzania umekua na kuimarika na ukuaji kwa asilimia sita
Amesema uchumi wa Tanzania umeimarika kutokana na uwekezaji uliofanywa na serikali katika kilimo na ujenzi wa miundombinu.
"Sekta ya viwanda imekuwa na mchango chiki ya asilimia 10 katika miongo mitatu iliyopita lakini kwa sasa changamoto nyingi zimetatuliwa na ndio maana uwekezaji katika sekta hii unazidi kukua,"amesema Profesa Kitila.
Amesema kati miradi 526 iliyosajiliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania kwa mwaka jana, pekee na miradi 237 iliikuwa ni ya uzalishaji viwandani.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Surtun Corporation Limited,Rehmtullah Habib amesemakiwanda hicho ni cha kuunganisha magari aina ya malori na matipa na kwa siku kinauwezo wa kuzalisha malori 30 na matipa tisa.
Amesema hadi sasa wamezalisha magari 150 na wanazalisha aina kuu mbili ambazo trucki na tippa kwaajili ya shughuli. Mbalimbali katika sekta ya ujenzi na madini.
" kiwanda hiki kimeajiri watu 250 na ajira zisizo rasmi 1800 wakati tunaanza kuuza magari walikuwa 20 tangu kiwanda kianze ajira zimeongeza,"amesema Habib.
Sio Lazima Kila Mhitimu Aajiriwe na Serikali: Waziri Simbachawene.
Waziri Simbachawene "Sio Lazima Kila Mhitimu Aajiriwe na Serikali"
TASAC YAWAJENGEA UWEZO MAWAKALA WA MELI, FORODHA NA WAKUSANYAJI NA WATAWANYAJI WA MIZIGO MWANZA.
Awamu ya pili uboreshaji, uwekaji wazi wa dafatri la wapiga kura kuanza mei.
NYONGO: SEKTA BINAFSI INA MCHANGO MKUBWA KWA TAIFA.
NIDA KUSITISHA MATUMIZI YA NAMBA ZA UTAMBULISHO (NINs) KWA WASIOCHUKUA VITAMBULISHO VYAO.
Shule mpya ya wavulana kugharimu zaidi ya bilioni tatu
Chama Cha Mawakili wa Serikali kufanya mkutano Aprili 14-15 jijini Dodoma
WADAU WA UNUNUZI WAASWA KUZINGATIA MAADILI KAZINI
Watumishi wa Bodi ya maziwa waaswa kuzingatia weledi katika kazi zao.