BANKI YA TCB YAZINDUA KIKOBA KIDIGITALI. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Biashara

BANKI YA TCB YAZINDUA KIKOBA KIDIGITALI.

Kufuatia kukua na kuimarika kwa Maendeleo ya Teknolojia nchini kumewezesha wananchi wengi kupata huduma za kibenki kwa njia salama na kuwa na uhakika wa usalama wa fedha zao.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
09 May 2024
BANKI YA TCB YAZINDUA KIKOBA KIDIGITALI.

Kufuatia kukua na kuimarika kwa Maendeleo ya Teknolojia nchini kumewezesha wananchi wengi kupata huduma za kibenki kwa njia salama na kuwa na uhakika wa usalama wa fedha zao.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Commercial Bank (TCB), Adam Mihayo, wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa Kikoba Kidigitali uliofanyika leo Mei 9,2024 Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa uzinduzi huo umelenga kusogeza huduma ya usajili wa kujiunga na Kikoba kupitia mtandao wake wa simu anaoutumia.

Ameongeza kuwa hapo awali huduma hiyo iliwapa fursa wateja wa mtandao mmoja pekee jambo ambalo liliwanyima fursa wateja wa mitandao mingine.

"TCB Benki, imeshirikiana na Kampuni zote za simu nchini zikiwemo, Tigo, Airtel, Halotel na Vodacom, ili kurahisisha namna ya kusajili na kujiunga na Kikoba mtandaoni.

"Ukiwa na Kikoba mtandaoni ni salama zaidi, kwani nirahisi kuona miamala yao, na kuleta uwazi kati ya wanachama"amesema Mihayo.

Amefafanua kuwa hatua hiyo imewezesha kuwa na aina mbili za vikoba, ambapo aina ya kwanza ni kumwezesha mteja kusajili au kujiunga na kikoba kupitia mtandao wake wa simu anaoutumia, na aina ya pili ni M-Koba inayomwezesha mteja kusajili Kikoba na kikundi cha watu wanaotumia mtandao mmoja wa Vodacom.

Awali akitoa neno la utangulizi katika sherehe hizo, Mkurugenzi wa Masoko wa Benki hiyo, Deo Kweyunga amesema kuwa uzinduzi huo utakwenda nchi nzima kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi na kuwahamisha Kuchangamkia fursa hiyo.

RC SENYAMULE ATAMANI DODOMA KUWA JIJI LA KIBIASHARA.

RC SENYAMULE ATAMANI DODOMA KUWA JIJI LA KIBIASHARA.

WAMILIKI wa viwanda watakiwa kuhakikisha wanalipa madeni ya wakulima.

WAMILIKI wa viwanda watakiwa kuhakikisha wanalipa madeni ya wakulima.

Wananchi 'wafunguka' barabara za TARURA zinavyowaongezea kipato na kukuza uchumi wao - Kilolo

Wananchi 'wafunguka' barabara za TARURA zinavyowaongezea kipato na kukuza uchumi wao - Kilolo

TADB WAINGIA MAKUBALIANO NA BENKI YA EXIM KUTOA DHAMANA YA MIKOPO KWA MINYORORO YA THAMANI KATIKA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI.

TADB WAINGIA MAKUBALIANO NA BENKI YA EXIM KUTOA DHAMANA YA MIKOPO KWA MINYORORO YA THAMANI KATIKA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI.