FCC YAWATAKA WADAU KUSHIRIKIANA KUTOKOMEZA BIDHAA BANDIA. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Biashara

FCC YAWATAKA WADAU KUSHIRIKIANA KUTOKOMEZA BIDHAA BANDIA.

TUME ya Taifa ya ushindani FCC imetoa rai kwa kampuni,taasisi za kifedha,wawekezaji na wazalishaji wa bidhaa,pamoja na wafanyabiashara kuhakikisha wanashirikiana ili kutokomeza uingizwaji na utengenezaji wa bidhaa bandia nchini ili kuchochea ukuaji wa uchumi lakini pia kuendelea kutoa elimu ya kudumu kuhusu matumizi ya bidhaa feki ilikuendeleza na kukuza uchumi wa nchi.

Sophia Kingimali.
By Sophia Kingimali.
17 Jul 2024
FCC YAWATAKA WADAU KUSHIRIKIANA KUTOKOMEZA BIDHAA BANDIA.

TUME ya Taifa ya ushindani  FCC imetoa rai kwa kampuni,taasisi za kifedha,wawekezaji na wazalishaji wa bidhaa,pamoja na wafanyabiashara  kuhakikisha wanashirikiana ili kutokomeza uingizwaji na utengenezaji wa bidhaa bandia nchini ili kuchochea ukuaji wa uchumi lakini pia kuendelea kutoa elimu ya kudumu kuhusu matumizi ya bidhaa feki ilikuendeleza na kukuza uchumi wa nchi.

wito huo umetolewa leo Julai 17,2024  jijini Dar es salaam na Mkurugenzi mkuu ambaye pia ni mkaguzi wa alama za bidhaa FCC William Erio  ikiwa ni wiki ya maadhimisho kudhibiti bidhaa bandia duniani yanayotarajiwa kuhitimishwa Julai 18,2024 huku yakiwa na kauli mbiu isemayo Kudumisha uhalisia katika kulinda ubunifu kwa ajili ya maendeleo ya uchumi. 

Amesema kuwa takwimu zinaonyesha kuwa kati ya asilimia 2 mpaka 5 ya biashara zinazofanyika duniani zinahusisha bidhaa bandia hivyo ni wajibu wa kila mwanamaendeleo kuhakikisha anakua mstari wa mbele kupinga na kuzuia matumizi ya bidhaa bandia.

Erio ameongeza kuwa bidhaa bandia kwenye biashara inazorotesha uchumi kwani inawafanya wanaofanya biashara ya bidhaa halisi kukosa soko lakini pia wawekezaji kuogopa kuingia kwenye soko kwani wanakosa nguvu ya kumiliki soko,ila kama serikali na wadau wote watashiriki kutokomeza bidhaa hizo bandia itasaidia kukuza soko.

Ameongeza kuwa kati ya asilimia 2.5 na 3.5 ya biashara zinayofanyika ulimwenguni zinahusisha bidhaa bandia ambapo amebainisha baadhi ya madhara ya bidhaa hizo kuwa ni kutopata thamani halisi ya fedha pamoja na madhara mbalimbali ya kiafya kwa watumiaji

“Wiki ya kudhibiti bidhaa bandia duniani , wiki hii inaadhimishwa sehemu zote duniani kati ya mwezi wa 6 na 7 na sababu yake ni kwamba bidhaa bandia zina matatizo mengi lakini katika biashara zinazoendelea sehemu mbalimbali duniani kati ya asilimia 2.5 na 3.5 ya biashara yote inayofanyika duniani inahusisha bidhaa bandia”,amesema.

Aidha Erio amezitaja athari zinazotokana na  bidhaa bandia ikiwemo kudhorotesha biashara, uchumi na kukosekana kwa ajira nchini.

“ Bidhaa bandia zina matatizo hata katika maeneo ya kiuchumi kwanza zinaathiri ubunifu kwasababu katika kushindana unatakiwa kila kitu uje na kitu kipya, Kuwa  na bidhaa katika uchumi kunadhorotesha biashara kwasababu pamoja na mambo mengine biashara ya bidhaa bandia inafanyika katika mifumo isiyo rasmi haifuati mifumo ya rasmi ya serikali kwahiyo kuna kodi, ubora wake ni wa chini”

Erio amewataka wadau kuendelea kuungana nao katika kuendelea kutoa elimu kuhudu matumizi ya bidhaa feki ili kuendelea kukuza uchumi nchini

Kilele cha maadhimisho hayo yaliyobebwa na Kauli mbiu isemayo “Kudumisha uhalisia kwa kulinda ubunifu kwa maendeleo ya kiuchumi nchini” kinatarajiwa kuwa julai 18 katika ukumbi wa mikutano ya mlimani city jijini dar es salaam ambapo kutaambatana na maonyesho mbalimbali ya wajasiriamali na wamiliki wa viwanda vidogovidogo pamoja na majadiliano ya jopo.

BODI YA MKONGE TANZANIA YATANGAZA FURSA  KWA WATANZANIA.

BODI YA MKONGE TANZANIA YATANGAZA FURSA KWA WATANZANIA.

DCEA:SERIKALI IMEPUNGUZA KASI YA WALAIBU WA DAWA ZA KULEVYA.

DCEA:SERIKALI IMEPUNGUZA KASI YA WALAIBU WA DAWA ZA KULEVYA.

VITONGOJI VYOTE 64,359 VITAKUWA NA UMEME IFIKAPO 2030

VITONGOJI VYOTE 64,359 VITAKUWA NA UMEME IFIKAPO 2030

FCC YATOA ELIMU YA UTAMBUZI BIDHAA FEKI SABASABA.

FCC YATOA ELIMU YA UTAMBUZI BIDHAA FEKI SABASABA.