

WAZIRI wa Viwanda na biashara Dkt.Ashatu Kijaji anatarajiwa kuwa mgeni rasmi siku ya maadhimisho ya siku ya miliki ubunifu Duniani yanayotarajiwa kufanyika Mei 9,2024 jijini Dar es salaam ambapo maazimisho hayo yataenda sambamba na utaiji saini wa hati ya makubaliano katika eneo la miliki ubunifu baina ya BRELA na COSOTA.
WAZIRI wa Viwanda na biashara Dkt.Ashatu Kijaji anatarajiwa kuwa mgeni rasmi siku ya maadhimisho ya siku ya miliki ubunifu Duniani yanayotarajiwa kufanyika Mei 9,2024 jijini Dar es salaam ambapo maazimisho hayo yataenda sambamba na utaiji saini wa hati ya makubaliano katika eneo la miliki ubunifu baina ya BRELA na COSOTA.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Mei 8,2024 Jijini Dar es salaam. Mkurugenzi wa Miliki Bunifu Loy Mhando Amesema maadhimisho hayo yalianzishwa na Shirika la miliki ubunifu Duniani (WIPO) Ambapo yatafanyika katika Hotel ya Johari rotana huku kauli mbiu ikiwa "Miliki Ubunifu na malengo ya Maendeleo endelevu Kujenga mustakabali wa pamoja kwa kutumia Ubunifu".
"Maadhimisho ya siku ya Miliki Bunifu Duniani huadhimishwa Aprili 26 kila mwaka lakini kwa hapa kwetu kutokana na Tarehe hiyo kuwa na jambo muhimu la kitaifa la kuazimisha muungano sisi tunaazimisha siku tofauti ambapo mwaka huu tunaadhimishia tarehe 09/05/2024,"Amesema.
Ameongeza kuwa katika maadhimisho hayo kutakuwa na matukio mbalimbali yatakayoambatana nayo ikiwemo mijadala kuhusu Miliki Ubunifu ambayo itahusu fursa,mafanikio na changamoto wanazokutana nazo katika nyanja nzima ya miliki ubunifu.
"Vile vile, hati za makubaliano ya ushirikiano katika eneo la Miliki Ubunifu baina ya BRELA,COSOTA na Taasisi nyingine zitasainiwa ikiwa ni njia ya kurasimisha ushirikiano uliopo baina ya Taasisi hizo katika kuhakikisha Miliki Ubunifu inaleta manufaa katika maendeleo ya kiuchumi na teknolojia nchini".
Aidha amesema Miliki Ubunifu inatija kubwa kwa wabunifu kwani inawapa ulinzi wa kumiliki bunifu zao na kuwasaidia katika kupata haki zao endapo mtu yoyote ataingilia ama kutumia bunifu yake pasipo makubaliano na mmiliki.
Mashirika ya kimataifa na kikanda ya Miliki Ubunifu yameongeza wigo wa ulinzi wa bunifu za wabunifu katika maeneo mbalimbali Duniani hususani kwa wabunifu wa kazi zinazovuka mipaka.
Waziri Mkuu Azindua Mfumo wa Kubadilishana Taarifa Serikalini GovESB.
LUKUVI AWASILISHA BUNGENI TAARIFA YA HALI YA DAWA ZA KULEVYA
UDSM YASAINI MAKUBALIANO NA KAMPUNI ZA CHINA KUTOA MAFUNZO KWA VITENDO KWA WANAFUNZI WA CHUO HICHO.
WATENDAJI WA UBORESHAJI WA DAFTARI MAGEREZA NA VYUO VYA MAFUNZO WANOLEWA
MAONESHO YA UTALII NA UWEKEZAJI ZANZIBAR; FURSA KWA WANANCHI KUJUA VIVUTIO VYA UTALII VILIVYOPO NGORONGORO
GRAND BUNGE BONANZA KUFANYIKA JUNI 21 2025 HUKU MGENI RASMI AKITARAJIWA KUWA RAIS SAMIA.
CDE SALUM ATANGAZA NIA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KAHAMA MJINI.
KIHENZILE:WIKI YA UTUMISHI WA UMMA NI FURSA MUHIMU KWA WANANCHI
NISHATI YA GESI ASILIA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA NCHI.
MOI YASEMA WAGONJWA WENGI WANAOWAHUDUMIA WANA MATATIZO SUGU.