

Mamlaka ya kuthibiti na kupambana na madawa ya kulevya imewakamata watu 16 waliohusika na kilimo cha madawa ya kulevya aina ya bangi.
Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na madawa ya kulevya imewakamata watu 16 waliohusika na kilimo cha madawa ya kulevya aina ya bangi.
Hayo yameelezwa na Kamishna msaidizi kanda ya kati Mzee Kasuwi wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu taarifa ya operesheni ya dawa za kulevya kanda ya kati Dodoma na kukabidhi silaha mbili kwa RPC Dodoma zilizopatikana kwenye operesheni tarehe 24 hadi 28 Aprili,2024.
Aidha amesema kuwa katika operesheni hiyo walifanikiwa kukamata silaha mbili za moto aina ya gobore zilizokuwa zinamilikiwa na Hamisi chambo mzigua mwenye umri wa miaka 46 pamoja na Abdilah Juma Mgogo mwenye umri wa miaka 45 wakazi wa kata ya segera ambao walikuwa wanamiliki kinyume cha sheria na kwamba zilikuwa zinatumiwa na watuhumiwa kulinda mashamba ya bangi."Tarehe 24 hadi 28 Aprili 2024,mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya kanda ya kati Dodoma imefanya operesheni katika maeneo ya wilaya ya Chamwino na Dodoma mjini na kufanikiwa kuteketeza ekari 9.5 za mashamba ya bangi,kukamata jumla ya kilogramu 156.23 za bangi na misokoto 127 ya bangi,watu 16 wamekamatwa kuhusika na dawa hizo na watafikishwa mahakamani baada ya taratibu za kisheria kukamilika" Ameongeza Kasuwi.
Amesema kuwa kwa niaba ya kamishna Jenerali wa mamlaka ya kudhibibiti na kupambana na dawa za kulevya anakabidhi silaha hizo kwa kamanda wa polisi wa Mkoa wa Dodoma kwa hatua zaidi za kisheria.
Aidha amewaomba wananchi kuendelea kutoa taarifa za watu wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya kwa kupiga simu kupitia namba yao ya bure 199.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma(RPC) Theopista Mallya ameishukuru Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya kwa kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi kutokomeza uhalifu na kutoa rai kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi kwa kumiliki silaha hatarishi na badala yake kufuata sheria za nchi na taratibu zake kwani Jeshi la polisi lipo na litaendelea kutokomeza matumizi mabaya ya dawa za kulevya.
“Kuna maeneo ambayo tumeelekezwa na tutaenda kuwakamata sababu hawa watu wanalinda haya mashamba kwa kutumia silaha za moto kwa hiyo wananchi waone uhatari uliopo wa hawa watu ambao wanajihusisha dawa ya kulevya,”amesema.
Amewataka wananchi kuwafichua watu wanaojihusisha na biashara hizo kwani wamekuwa hatari kwa jamii na kwa taifa kwa ujumla.
Sio Lazima Kila Mhitimu Aajiriwe na Serikali: Waziri Simbachawene.
Waziri Simbachawene "Sio Lazima Kila Mhitimu Aajiriwe na Serikali"
TASAC YAWAJENGEA UWEZO MAWAKALA WA MELI, FORODHA NA WAKUSANYAJI NA WATAWANYAJI WA MIZIGO MWANZA.
Awamu ya pili uboreshaji, uwekaji wazi wa dafatri la wapiga kura kuanza mei.
NYONGO: SEKTA BINAFSI INA MCHANGO MKUBWA KWA TAIFA.
NIDA KUSITISHA MATUMIZI YA NAMBA ZA UTAMBULISHO (NINs) KWA WASIOCHUKUA VITAMBULISHO VYAO.
Shule mpya ya wavulana kugharimu zaidi ya bilioni tatu
Chama Cha Mawakili wa Serikali kufanya mkutano Aprili 14-15 jijini Dodoma
WADAU WA UNUNUZI WAASWA KUZINGATIA MAADILI KAZINI
Watumishi wa Bodi ya maziwa waaswa kuzingatia weledi katika kazi zao.