MSD KUISAIDIA SIERRA LEON KUIMARISHA BOHARI YAO YA DAWA. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Tanzania

MSD KUISAIDIA SIERRA LEON KUIMARISHA BOHARI YAO YA DAWA.

BOHARI kuu ya dawa nchini MSD wamekubaliana kushirikiana na Bohari ya Dawa ya Sierra leone kubadilishana taarifa za utendaji ili kuwasaidia bohari hiyo kuweza kukua na kufikia ukubwa wa MSD.

Sophia Kingimali
By Sophia Kingimali
29 Apr 2024
MSD KUISAIDIA SIERRA LEON KUIMARISHA BOHARI YAO YA DAWA.

BOHARI kuu ya dawa nchini MSD wamekubaliana kushirikiana na Bohari ya Dawa ya Sierra leone kubadilishana taarifa za utendaji ili kuwasaidia bohari hiyo kuweza kukua na kufikia ukubwa wa MSD.

Akizungumza leo Aprili 29,2024 wakati wa mazungumzo na ugeni kutoka Sierra Leon uliokuja nchini kujifunza shughuli zinazofanywa na MSD Mkurugenzi Mkuu wa MSD Mavere Tukai amesema kutokana na utendajikazi wa bohari hiyo umeendelea kuvutia wengi kuja kujifunza.

"Tunakumbuka Sierra Leon ni nchi ambayo ilikubwa na matatizo ya amani ambao ulivunja vunja mfumo mzima wa afya sasa wameamka na kujikung'uta na kuanza upya mfumo wao wa afya na sasa wamekuja huku kujifunza namna ya sisi tunavyofanya kazi zetu.

Amesema moja ya kitu kilichowavutia zaidi ni ubunifu ambao MSD wamekuwa nao katika kufanya shughuli zao za kununua na kusambaza dawa lakini pia uhimilivu wa fedha lakini na matumizi ya Tehama.

Aidha amesema watawasaidia taasisi yao jinsi ya kuweza kushirikiana na wadau wengine ndani ya serikali na nje ya  serikali ikiwemo kuunganisha mifumo yao na idara mbalimbali,  kama watu wa fedha, utumishi, wateja na wizara ya afya.

Kwa upande wake,Mfamasia Mkuu wa serikali na Mkurugenzi wa huduma za dawa Daud Msasi amesema  ujio wa wageni hao ni kuona wanaboresha bohari yao ya dawa inaboreshwa na kuimarika katika kutoa huduma.

Amesema nchi ipo tayari kuwapa ushirikiano wa kutosha kwa maslahi mapana ya wananchi wa Afrika.

"Ukiona mtu amechambua akaja akaswma akajifunze Tanzania inamaanisha tunafanya vizuri na ndio maana ndugu zetu hawa wakachagua kuja hapa kujifunza ni ugeni mzito ambao umeongozwa na Mganga mkuu wa nchi yao",Amesema.

Naye,Mfamasia Mkuu na Mkurugenzi wa huduma za dawa Sierra Leon Moses Batema amesema wamefanya utafiti wa kutosha na kuona sehemu ya kwenda kujifunza ni Tanzania hivyo wameridhishwa na majadiliano walioyafanya lakini pia wamejifunza vitu vingi vitakavyowasaidia kuboresha Bohari yao.

MAHAKAMA YAMWACHIA HURU ALIYEKUA DED MAFIA KASSIM NDUMBO

MAHAKAMA YAMWACHIA HURU ALIYEKUA DED MAFIA KASSIM NDUMBO

MHANDISI SEFF AMTAKA MKANDARASI UJENZI WA BARABARA YA KASULU-KABANGA-MUYAMA KUMALIZA KAZI KWA WAKATI

MHANDISI SEFF AMTAKA MKANDARASI UJENZI WA BARABARA YA KASULU-KABANGA-MUYAMA KUMALIZA KAZI KWA WAKATI

Serikali ya Tanzania kuendelea kushirikiana na Serikali ya Zanzibar

Serikali ya Tanzania kuendelea kushirikiana na Serikali ya Zanzibar

RC MTWARA AIPONGEZA WIZARA YA FEDHA KWA KUTOA ELIMU YA FEDHA KWA WANANCHI.

RC MTWARA AIPONGEZA WIZARA YA FEDHA KWA KUTOA ELIMU YA FEDHA KWA WANANCHI.