

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama ametoa shime kwa Baraza la Uwekezaji wa Wananchi Kiuchumi kwa kushirikiana na sekta binafsi na wadau mbalimbali kutambua mawanda makubwa ya uwekezaji yaliyo katika nchi yetu.
Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza katika Kongamano la Nne la Kitaifa la Ushiriki wa Watanzania katika Miradi ya kimkakati na uwekezaji lilofanyika leo tarehe 27 Aprili, 2024 katika ukumbi wa Benki kuu ya Tanzania (BOT) Jijini Dar es salaam.
Waziri Mhagama amesema kuwa sekta binafsi na wadau mbalimbali waendelee kutoa mapendekezo kwenye fursa mbalimbali zinazojitokeza za kiuchumi ili kuwezesha utekelezaji wa miradi ya kiuchumi kufikia malengo yaliyopo.
Ameongeza kusema wananchi wa Tanzania wako tayari wakiongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameonesha kwa vitendo kwamba yuko tayari hivyo ni vyema kumuunga mkono kwa kufanya kazi ili kujenga uchumi wa Taifa.
Aidha jukwaa hilo litasaidia kujenga uelewa wa pamoja juu ya mafanikio yaliyopatikana na katika uwekezaji na ustawi wake wa kiuchumi.
Waziri aliongezea dhana ya kongamano hilo lenye kauli Mbiu ya “Wekeza Tanzania kuongeza thamani ya ziada” linatumika kujenga uchumi imara ambao umeshirikisha Watanzania wengi.
“Na itatutengenezea mazingira mazuri ya biashara ambayo yatachochea wananchi wengi katika uwekezaji na ushiriki wao katika kujenga uchumi,"alisema Waziri Mhagama
Baraza la Uwekezaji wa Wananchi Kiuchumi limeingia makubaliano na taasisi ya serikali inayosimamia manunuzi ya umma, katika moja ya kipengele katika sheria ya manunuzi ya umma kinachosisitiza kila asilimia 30 ya manunuzi ya umma ya kila mradi yaende kwa vijana, wanawake wazee na watu wenye ulemavu ambayo ni sehemu ya uwezeshaji wa wananchi kiuchumi.
Kwa upande wake Bibi, Beng’i Issa Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi wa Kiuchumi (NEEC) amesema moja ya mambo wanayosimamia ni kuangalia kampuni zinazopata kazi kwenye miradi ya kiuchumi na bidhaa zinazouzwa katika miradi hiyo zinatoka nchini.
Aidha kwenye ajira Baraza la Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi linaangalia ajira za moja kwa moja na ajira ambazo sio za moja kwa moja katika uhaulishaji wa teknolojia kwa kusimamia teknolojia nchini na mipango ya kutoa mafunzo ya kuhaulisha inafanyika
Akizungumzia kuhusu kongamano amesema kongamano hilo la Nne limelenga katika kujenga uelewa wa pamoja kuhusu ushiriki wa watanzania katika miradi ya kimkakati na uwekezaji unaofanyika hapa nchini pamoja na kushirikishana mafanikio na changamoto zilizopo katika ushiriki wa watanzania katika uwekezaji.
DKT. BITEKO AKUTANA NA MTENDAJI MKUU WA CLIMATE INVESTMENT FUNDS
KAMATI ya Bunge ya miundombinu yaridhishwa na kasi ujenzi daraja la pangani
MIKOA 16 kunufaika na Nishati ya Jotoardhi
MASAA YA Upatikanaji wa Huduma ya Maji Yameongezeka Kutoka saa 16 hadi saa 22
MAMLAKA ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imefanikiwa kutoa mafunzo kwa wadau wa kemikali
Hatua Kali Za Kisheria Kuchukuliwa Kwa Watakaoghushi Cheti Cha Kuhitimu Mafunzo ya JKT.
Vituo 94 vimepewa mikopo na NHIF kwa ajili ya kuboresha huduma wanazotoa kwa wananchi.
RAIS SAMIA Aagiza Mamlaka Za Serikali za Mitaa Kujiepusha Kuwa Vyanzo vya Migogoro ya Ardhi Nchini.
NCAA IMEFANIKIWA Kudhibiti Ujangili wa Wanyamapori Ndani na Nje ya Hifadhi ya Ngorongoro.
Mavunde Agawa Kompyuta na Printa kwa shule zote za Sekondari za Jiji la Dodoma.