KINANA: SERIKALI YA RAIS DKT. SAMIA ITACHUKUA HATUA KUKABILI ATHARI ZA MVUA. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Tanzania

KINANA: SERIKALI YA RAIS DKT. SAMIA ITACHUKUA HATUA KUKABILI ATHARI ZA MVUA.

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na serikali kwa ujumla inafuatilia kwa karibu athari zinazotokana na mvua kubwa ikiwemo kusababisha uharibifu wa miundombinu.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
19 Apr 2024
KINANA: SERIKALI YA RAIS DKT.  SAMIA ITACHUKUA HATUA KUKABILI ATHARI ZA MVUA.

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na serikali kwa ujumla inafuatilia kwa karibu athari zinazotokana na mvua  kubwa ikiwemo kusababisha uharibifu wa miundombinu.

Miongoni mwa hatua zilizochukuliwa ni kupeleka fedha za ukarabati wa miundombinu na misaada mbalimbali kuwasaidia walioathirika. 

Kinana ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wanachama wa CCM Wilaya ya Musoma Mjini ambao walieleza uharibifu wa baadhi ya miundombinu ya barabara katika wilaya hiyo na Mkoa wa Mara kwa ujumla  kutokana na mvua zinazoendelea kunyeesha.

 "Serikali inaendelea kufanya tathmini ya uharibifu huo wa miundombinu ili kutenga fedha za kukarabati maeneo yote ambayo yameathirika.Uharibifu wa miundombinu umefanyika katika nchi mbalimbali duniani hata zile zilizopiga hatua kubwa ya maendeleo na sio Tanzania peke yake. 

"Kwa mara ya kwanza tumeona duniani nchi nyingi zimepatwa na mafuriko, hata zile ambazo katika historia hatukuwahi kuona mvua, hivyo sio sisi peke yetu, haya yote yametokana na mabadiliko ya tabianchi, mahitaji ya kufanya marekebisho ni makubwa na yataendelea.

"Niwaambie Rais Samia anapata taarifa kuhusu haya yanayotokea katika mikoa mingi, sehemu ambapo miundombinu imeharibika sana hadi kukosekana kwa mawasiliano hatua za dhati zimechukuliwa," amesema.

MAHAKAMA YAMWACHIA HURU ALIYEKUA DED MAFIA KASSIM NDUMBO

MAHAKAMA YAMWACHIA HURU ALIYEKUA DED MAFIA KASSIM NDUMBO

MHANDISI SEFF AMTAKA MKANDARASI UJENZI WA BARABARA YA KASULU-KABANGA-MUYAMA KUMALIZA KAZI KWA WAKATI

MHANDISI SEFF AMTAKA MKANDARASI UJENZI WA BARABARA YA KASULU-KABANGA-MUYAMA KUMALIZA KAZI KWA WAKATI

Serikali ya Tanzania kuendelea kushirikiana na Serikali ya Zanzibar

Serikali ya Tanzania kuendelea kushirikiana na Serikali ya Zanzibar

RC MTWARA AIPONGEZA WIZARA YA FEDHA KWA KUTOA ELIMU YA FEDHA KWA WANANCHI.

RC MTWARA AIPONGEZA WIZARA YA FEDHA KWA KUTOA ELIMU YA FEDHA KWA WANANCHI.