MAKAMU WA PILI WA RAIS SMZ ATAKA WANANCHI KUULINDA MUUNGANO. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Tanzania

MAKAMU WA PILI WA RAIS SMZ ATAKA WANANCHI KUULINDA MUUNGANO.

Makamu wa pili wa Rais wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla ametoa rai kwa wananchi kuendelea kuulinda,kuimarisha na kudumumisha Muungano kwa faida ya vizazi vijavyo.

Sophia Kingimali.
By Sophia Kingimali.
19 Apr 2024
MAKAMU WA PILI WA RAIS SMZ ATAKA WANANCHI KUULINDA MUUNGANO.

Makamu wa pili wa Rais wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla ametoa rai kwa wananchi kuendelea kuulinda,kuimarisha na kudumumisha Muungano kwa faida ya vizazi vijavyo.

Wito huo ameutoa leo Aprili 19,2024 Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Maonesho ya miaka 60 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika viwanjwa vya Mnazi mmoja.

Amesema katika kipindi chote cha miaka 60 serikali zote mbili zimeweza kusimamia na kutekeleza wa maswala ya Muungano lakini pia kuimarika kwa utaifa,umoja,amani,utulivu na ukuaji wa uchumi wapande zote mbili za Muungano.

"Kipekee nimpongeze Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania lakini pia Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Hussein Alli Mwinyi kwa kuliongoza taifa likiwa na amani na mshikamano unaotokana na muungano ambao sasa umetimiza miaka 60",Amesema.

Amesema maonesho hayo yanashirikisha wizara na taasisi za Muungano pamoja na wafanyabiashara wadogo hivyo ametoa rai kwa wananchi kujitokeza ili waweze kujifunza mambo mbalimbali yaliyoyanywa na taasisi hizo katika kipindi cha miaka 60.

"Nitoe rai kwa wananchi kujitokeza kwa wingi na kutumia fursa hiyo kujifunza mambo yanayohusu muungano lakini pia kutoa maoni na ushauri utakaowezesha kuimarisha na kudumisha Muungano wetu",Amesema.

Aidha ameongeza kuwa ustawi wa wananchi umeimarika lakini pia hali hiyo imetoa fursa kwa wafanyabiashara wadogo na wakubwa kuweza kuwekeza katika pande zote za Muungano ikiwemo viwanda,Hoteli na kilimo cha biashara jambo ambalo limechangia kuongeza ajira kwa wananchi.

Kwa upande wake Naibu waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira Khamis Hamza Khamis amesema maonesho hayo yanatoa fursa kwa wananchi kuweza kujifunza kazi mambo mablimbali yaliyoyanyika na yanayoendelea kufanyika katika Muungano.

Aidha amesema muungano huo umeleta mafanikio makubwa katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa pande zote mbili za Muungano kwani huduma mbalimbali za kijamii zimeimarika ikiwemo Afya,maji na miundombinu ya barabara.

"Miongoni mwa mafanikio ya Muungano ni pamoja na kuishi kwa amani na utulivu sehemu yoyote ya Jamuhuri ya Muungano na kufanya shughuli za kiuchumi na kijamii bila bughuza lakini kubwa zaidi tumepata hata fursa ya kuchanganya damu(kuoa)katika pande zote mbili",Amesema.

NAE,Meneja wa ukuzaji biashara TANTRADE Mohamed  Tajiri ametoa rai kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika maonesho hayo kwani watajifunza maswala mbalimbali ya Muungano lakini pia kujua namna wanavyoweza kukuza biashara zao na kuzitangaza kimataifa.

Maonesho hayo ya biashara yanatarajiwa kufungwa April 25,2024 ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ikisema "Tumeimarika na Tumeshikamana kwa maendeleo ya Taifa letu"

MAHAKAMA YAMWACHIA HURU ALIYEKUA DED MAFIA KASSIM NDUMBO

MAHAKAMA YAMWACHIA HURU ALIYEKUA DED MAFIA KASSIM NDUMBO

MHANDISI SEFF AMTAKA MKANDARASI UJENZI WA BARABARA YA KASULU-KABANGA-MUYAMA KUMALIZA KAZI KWA WAKATI

MHANDISI SEFF AMTAKA MKANDARASI UJENZI WA BARABARA YA KASULU-KABANGA-MUYAMA KUMALIZA KAZI KWA WAKATI

Serikali ya Tanzania kuendelea kushirikiana na Serikali ya Zanzibar

Serikali ya Tanzania kuendelea kushirikiana na Serikali ya Zanzibar

RC MTWARA AIPONGEZA WIZARA YA FEDHA KWA KUTOA ELIMU YA FEDHA KWA WANANCHI.

RC MTWARA AIPONGEZA WIZARA YA FEDHA KWA KUTOA ELIMU YA FEDHA KWA WANANCHI.