TANTRADE WATAKA WANANCHI KUJITOKEZA KWENYE MAONESHO YA MIAKA 60 YA MUUNGANO | The Dodoma Post
The Dodoma Post Biashara

TANTRADE WATAKA WANANCHI KUJITOKEZA KWENYE MAONESHO YA MIAKA 60 YA MUUNGANO

Meneja wa ukuzaji biashara TANTRADE Mohamed Tajiri ametoa rai kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika maonesho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ili waweze kujifunza maswala mbalimbali ya Muungano lakini pia kujua namna wanavyoweza kukuza biashara zao na kuzitangaza kimataifa.

Sophia Kingimali
By Sophia Kingimali
19 Apr 2024
TANTRADE WATAKA WANANCHI KUJITOKEZA KWENYE MAONESHO YA MIAKA 60 YA MUUNGANO

Meneja wa ukuzaji biashara TANTRADE Mohamed  Tajiri ametoa rai kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika maonesho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ili waweze kujifunza maswala mbalimbali ya Muungano lakini pia kujua namna wanavyoweza kukuza biashara zao na kuzitangaza kimataifa.

Wito huo ameutoa leo Aprili 19,2024 katika maonyesho hayo yaliyofunguliwa na Makamu wa pili wa Rais wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam.

Amesema uwepo wa TANTRADE katika maonyesho hayo ni kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na mambo wanayofanya hasa katika kukuza biashara na kuzitangaza kimataifa.

"Nitoe rai kwa wananchi kufika katika maonesho haya kwani watapata fursa ya kujifunza maswala mbalimbali ya muungano kwani taasisi zote za muungano zipo na zitatoa elimu kuhusu waliyoyafanya na wanayoendelea kuyafanya katika kukuza na kuimarisha Muungano",Amesema.

Akizungumza awali wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo Naibu Waziri (Muungano na Mazingira)  Khamis Hamza Khamis amesema maonesho hayo yanatoa fursa kwa wananchi kuweza kujifunza kazi mambo mablimbali yaliyoyanyika na yanayoendelea kufanyika katika Muungano.

Aidha amesema muungano huo umeleta mafanikio makubwa katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa pande zote mbili za Muungano kwani huduma mbalimbali za kijamii zimeimarika ikiwemo Afya,maji na miundombinu ya barabara.

"Miongoni mwa mafanikio ya Muungano ni pamoja na kuishi kwa amani na utulivu sehemu yoyote ya Jamuhuri ya Muungano na kufanya shughuli za kiuchumi na kijamii bila bughuza lakini kubwa zaidi tumepata hata fursa ya kuchanganya damu(kuoa)katika pande zote mbili",Amesema.

Maonesho hayo ya biashara yanatarajiwa kufungwa April 25,2024 ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ikisema “Tumeimarika na Tumeshikamana kwa maendeleo ya Taifa letu”

RC SENYAMULE ATAMANI DODOMA KUWA JIJI LA KIBIASHARA.

RC SENYAMULE ATAMANI DODOMA KUWA JIJI LA KIBIASHARA.

WAMILIKI wa viwanda watakiwa kuhakikisha wanalipa madeni ya wakulima.

WAMILIKI wa viwanda watakiwa kuhakikisha wanalipa madeni ya wakulima.

Wananchi 'wafunguka' barabara za TARURA zinavyowaongezea kipato na kukuza uchumi wao - Kilolo

Wananchi 'wafunguka' barabara za TARURA zinavyowaongezea kipato na kukuza uchumi wao - Kilolo

TADB WAINGIA MAKUBALIANO NA BENKI YA EXIM KUTOA DHAMANA YA MIKOPO KWA MINYORORO YA THAMANI KATIKA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI.

TADB WAINGIA MAKUBALIANO NA BENKI YA EXIM KUTOA DHAMANA YA MIKOPO KWA MINYORORO YA THAMANI KATIKA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI.