GAVANA TUTUBA ATAKA VIJANA WAPEWE ELIMU YA FEDHA VYUONI. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Tanzania

GAVANA TUTUBA ATAKA VIJANA WAPEWE ELIMU YA FEDHA VYUONI.

Gavana wa Benki kuu nchini Emmanuel Tutuba ametoa rai kwa Taasisi za Fedha nchini kuwajengea uwezo wanafunzi pindi wanapokuwa vyuoni ili waweze kuwa na mtazamo chanya wa kuendesha mifumo ya kifedha kwani elimu ya maswala hayo bado ipo chini.

Sophia Kingimali.
By Sophia Kingimali.
02 Apr 2024
GAVANA TUTUBA ATAKA VIJANA WAPEWE ELIMU YA FEDHA VYUONI.

Gavana wa Benki kuu nchini Emmanuel Tutuba ametoa rai kwa Taasisi za Fedha nchini kuwajengea uwezo wanafunzi pindi wanapokuwa vyuoni ili waweze kuwa na mtazamo chanya wa kuendesha mifumo ya kifedha kwani elimu ya maswala hayo bado ipo chini.

Hayo ameyasema leo Aprili 2,2024 jijini Dar es salaam wakati akifungua Mashindano ya TIOB( The Tanzania Institute of Bankers) kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu kwa mwaka 2024.

Amesema kufuatia na mifumo imara iliyowekwa na serikali ya awamu ya sita katika sekta ya benki imepelelekea kuwa na mifumo mingi inayowezesha sekta binafsi kuweza kuingia na kufanya kazi vizuri na kupata faida.

"Tuwajengee uwezo vijana kuhusu maswala ya kifedha wakiwa bado wapo shuleni hii itasaidia watakapomaliza chuo waweze kujiajiri lakini pia kuajilika na itasaidia kuendelea kupunguza mikopo chechefu",Amesema  Tutuba.

Amesema kufuatia hali ya uchumi kwa sasa katika sekta ya kibenki kwa asilimia 70 inaendesha na sekta binafsi hii inaamaana kwamba uchumi wa tanzania unaendesha na sekta binafsi 

"Shughuli za uchumi zinaendelea kupanuka hivyo serikali imeweka mazingira huru ya kila mmoja  kufanya shughuli zake kwa sasa ukiangalia product zote zinazingatia mifumo iliyo huru ambapo sekta binafsi zinaweza kuziendesha",Amesema 

Aidha Tutuba ameongeza kwa Kiwango cha mikopo chechefu imepungua kwani lengo lilikuwa kufikia chini ya asilimia tano lakini sasa imefikia asilimi 4 hivyo kama nchi inapaswa kujivunia kwa hili.

Amesema kwanamna ambavyo serikali inavyoshirikiana na mabenk wanaamini hiyo mikopo chechefu inaendelea kushuka zaidi huku tukihamasisha mabenki kwenda vijijini na kuwa na bidhaa ambazo zitawasaidia wote kutumia mabenki.

Akizungumzia kuhusu uhaba  wa Dola nchini amesema Dola zipo na wanaendelea kulipia miradi yote ya serikali na hakuna mradi ambao umewahi kukwama au kuchelewa kwa sababu ya kukosa dola.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa TIOB Patrick Mususa amesema shindano hilo linalengo la kuelimisha vijana jinsi ya kutoa huduma za kifedha kwa kutumia mbinu bora.

Amesema mashindano hayo yamezinduliwa leo na yanatarajiwa kuisha July 7,2024 ambapo washindi watashida zawadi mbalimbali ikiwemo pesa taslim milioni tatu huku gavana akiahidi kuiongeza na kufikia milioni 5 kwa mshindi wa kwanza.

"Wanafunzi wote kutoka Taasisi za elimu ya juu wanaruhusiwa kushiriki wakati wowote popote walipo kwani shindano hili linaendesha kwa njia ya digitali kwa kutumia simu ya mkononi kwa kutumia Whatsapp kwa kutuma neno MENU kwenda namba 0763808776",Amesema Mususa.

Sambamba na hayo Mususa ametoa rai kwa taasisi mbalimbali za fedha kushirikiana na TIOB kuhakikisha wanaendelea kutoa motisha kwa wanafunzi kushiriki shindano hilo.

MAHAKAMA YAMWACHIA HURU ALIYEKUA DED MAFIA KASSIM NDUMBO

MAHAKAMA YAMWACHIA HURU ALIYEKUA DED MAFIA KASSIM NDUMBO

MHANDISI SEFF AMTAKA MKANDARASI UJENZI WA BARABARA YA KASULU-KABANGA-MUYAMA KUMALIZA KAZI KWA WAKATI

MHANDISI SEFF AMTAKA MKANDARASI UJENZI WA BARABARA YA KASULU-KABANGA-MUYAMA KUMALIZA KAZI KWA WAKATI

Serikali ya Tanzania kuendelea kushirikiana na Serikali ya Zanzibar

Serikali ya Tanzania kuendelea kushirikiana na Serikali ya Zanzibar

RC MTWARA AIPONGEZA WIZARA YA FEDHA KWA KUTOA ELIMU YA FEDHA KWA WANANCHI.

RC MTWARA AIPONGEZA WIZARA YA FEDHA KWA KUTOA ELIMU YA FEDHA KWA WANANCHI.