WIZARA YA VIWANDA WAPOKEA WAWEKEZAJI KUTOKA CHINA. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Tanzania

WIZARA YA VIWANDA WAPOKEA WAWEKEZAJI KUTOKA CHINA.

Wizara ya Viwanda na Biashara imefanya mazungumzo na wawekezaji kutoka nchi ya China waliokuja kuangalia fursa zinazopatikana ili waweze kuwekeza nchini na nchi iweze kunufaika kwa kupata uwekezaji utakaochochea maendeleo ya nchi na kuongeza ajira.

Sophia kingimali
By Sophia kingimali
27 Mar 2024
WIZARA YA VIWANDA WAPOKEA WAWEKEZAJI KUTOKA CHINA.

Wizara  ya Viwanda na Biashara imefanya mazungumzo na wawekezaji  kutoka  nchi ya China waliokuja kuangalia  fursa zinazopatikana ili waweze kuwekeza nchini na nchi iweze kunufaika kwa kupata uwekezaji utakaochochea maendeleo ya nchi na kuongeza ajira.

Akizungumza leo Machi 27 jijini Dar es Salaam baada ya mazungumzo hayo Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Sempeho Manongi amesema  wamepata wageni kutoka nchini China katika  Jimbo la Changzho ambao wamekuja kwaajili  ya kuangalia maeneo ambayo wanaweza kuleta ushirikiano.

Amesema wawekezaji hao wameletwa kwa kushirikiana na kampuni  mbili ambazo ni kampuni  ya Canopus Energy  Solutions na Amec Group katika wangeni hao wameambatana na viongozi wa serikali na wawekezaji na timu ya wataalam.

"Tumewaonyesha fursa zilizopo za viwanda  na maeneo ya uwekezaji katika sekta zote muhimu  kwa nchi yetu ili waweze kuimarisha uchumi wa  nchi.Pia wamewaonyesha maeneo mengine ya viwanda ambayo ni muhimu wanaweza kuzalisha na kutengeneza Kituo  maalumu,"amesema Manongi. 

Ameeleza kuwa katika mazungumzo hayo wamekubaliana na baadhi ya maeneo hayo hivyo wanaelekea Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),kwenda kupata taarifa ya kina kwenye masuala  ya uwekezaji  ili waweze  kuingia makubaliano  kwenye  maeneo ambayo wameona yanahitajika kwaajili ya uwekezaji. 

Manongi amesema wao wameonyesha maeneo  ya sekta ya kilimo katika  kuongeza thamani mazao ya kilimo  maeneo  ya uzalishaji wa madini ya viwanda ambayo  ni muhimu mfano chuma

Ameongeza kuwa Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) wana maeneo  makubwa ambayo wanaweza kuwekeza ikiwemo Kilimanjaro machine tools, Tange lipo Tanga, Kibaha maeneo kwaajili ya uwekezaji.

Amesema wameshauriana kuangalia aina ya  uwekezaji kwani wanaweza kuwekeza moja kwa moja,  au kuwekeza kwa ubia na kubadilisha ujuzi na uzoefu ambao utaletwa nchini.

Aidha amesema  katika Miradi saba ikitekelezwa kuzalisha MEGAWATI 

zaidi ya 1400  wanahitaji umeme kwa wingi hivyo wakipata uwekezaji kikubwa kupata utalaamu wa hiyo sekta ndio wanahitaji kwa wingi na baadae wawekezaji wakijitokeza watapata umeme kwa wingi na uzalishaji utaongezeka ajira na matumizi ya umeme.

Naye Kiongozi wa Ujumbe Kutoka Serikalini  ya Jimbo la Changzho, Shen Don amesema nchi hizo mbili zimekuwa na ushirikiano  mkubwa  katika  nyanja mbalimbali  wanahitaji kuwekeza katika uzalishaji katika  viwanda. 

Kwa upande wake  Mhandisi Anna Nyangasi wa Kampuni  ya Canopus Energy  Solutions kwa kushirikiana na Amec amesema  kampuni hizo zimewaleta wawekezaji hao ili kuja kuwekeza nchini kwenye meeneo tofauti ya kiwemo sekta ya kilimo,Afya na vifaa vya ujenzi

"Watawekeza katika  maeneo  mashine za kilimo watawekeza dola za kimarekani milioni  24.5,  vifaa vya hospitali watawekeza dola za kimarekani milioni 6.

Vifaa vya  umeme watawekeza dola za Kimarekani  milioni mbili vifaa vya ujenzi dola za kimarekani milioni 11.3 vifaa vya uchakataji wa mafuta dola za kimarekani milioni  43,"amesema Mhandisi Anna .

KINANA: SERIKALI YA RAIS DKT.  SAMIA ITACHUKUA HATUA KUKABILI ATHARI ZA MVUA.

KINANA: SERIKALI YA RAIS DKT. SAMIA ITACHUKUA HATUA KUKABILI ATHARI ZA MVUA.

MAKAMU WA PILI WA RAIS SMZ ATAKA WANANCHI KUULINDA MUUNGANO.

MAKAMU WA PILI WA RAIS SMZ ATAKA WANANCHI KUULINDA MUUNGANO.

TANZANIA YAIPATIA ZAMBIA SCANA ILI KUTATUA CHANGAMOTO ZA BIASHARA MPAKANI

TANZANIA YAIPATIA ZAMBIA SCANA ILI KUTATUA CHANGAMOTO ZA BIASHARA MPAKANI

TANZANIA Imeendelea Kunufaika na fursa za mafunzo kutoka nchi mbalimbali.

TANZANIA Imeendelea Kunufaika na fursa za mafunzo kutoka nchi mbalimbali.