

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Temeke kupitia Chama cha AAFP Yusuph Rai, ameahidi kufanya mabadiliko makubwa katika sekta za afya, elimu, miundombinu na huduma za kijamii endapo atachaguliwa na wananchi wa jimbo hilo.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Temeke kupitia Chama cha AAFP Yusuph Rai, ameahidi kufanya mabadiliko makubwa katika sekta za afya, elimu, miundombinu na huduma za kijamii endapo atachaguliwa na wananchi wa jimbo hilo.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika Kata ya Mtoni, jijini Dar es Salaam Rai amesema moja ya vipaumbele vyake ni kuhakikisha kila kata inapewa gari la kubebea marehemu (kirukuu) ili kurahisisha huduma za jamii.
"Mkichagua chama hiki na mkanichagua mimi kuwa muwakilishi wenu siyo maiti tu bali hata gari la kubebea maiti tutatoa bure. Kila kata itakuwa na kirukuu kupitia mshahara wangu na fedha za jimbo," amesema Rai.
Kuhusu sekta ya afya, mgombea huyo amesema zahanati ya Mtoni hailingani na idadi kubwa ya wakazi waliopo katika eneo hilo, hivyo ataweka nguvu kubwa kushinikiza kupatikana kwa kituo cha afya kikubwa zaidi chenye majengo na vifaa tiba vya kisasa.
"Niwahakikishie nitafanya kila juhudi kuhakikisha tunapata kituo cha afya cha kisasa na kuongeza majengo ya hospitali pamoja na vifaa tiba vya kutosha," amesisitiza.
Akigusia sekta ya elimu, Rai amesema katika Kata ya Mtoni kuna shule nne za msingi lakini bado shule ya msingi Mtoni inakabiliwa na changamoto ya wanafunzi kukaa chini kwa kukosa madawati.
"Hii hali siyo ya kuridhisha. Tuwatumie wawekezaji na wahisani kupata madawati. Lakini pia nitaondoa michango ya ovyo ambayo imekuwa kero kwa wazazi. Ni ajabu shule zikikusanya pesa nyingi kuliko TRA," amesema.
Ameongeza kuwa shule pekee ya sekondari iliyopo Mtoni haikidhi mahitaji ya wanafunzi, hivyo kuna ulazima wa kujenga shule nyingine ya serikali pamoja na shule ya kidato cha tano na sita (advance).
Kuhusu miundombinu, Rai amesema atahakikisha maboresho ya njia za maji taka na miundombinu ya barabara ili kuepusha mafuriko yanayojitokeza mara kwa mara wakati wa mvua.
Aidha, amegusia mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, ameahidi kushughulikia vikundi hewa ambavyo vimekuwa vikiitumia vibaya mikopo hiyo.
"Kuna vikundi hewa vimekuwa vikifaidika. Nikichaguliwa nitahakikisha mikopo hii inawafikia walengwa halisi," alisema.
Akihitimisha hotuba yake, Rai amewataka wananchi wa Temeke kuchagua viongozi wanaoleta mabadiliko ya kweli,huku akiwahimiza kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura.
"Niwaambie, chagueni viongozi wa kweli. Tukiamua kwa pamoja, mabadiliko Temeke yanawezekana," amesisitiza.
Mfalme wa Mashairi Awasha Moto wa Uzalendo: “Kura Yako Ni Silaha”
MUFTI ATAKA WAISLAMU KUZINGATIA MAFUNDISHO YA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 29.
DOWOSA Yawaokoa Wanawake Dodoma Kutoka Mikononi mwa “Kausha Damu”
VIONGOZI WA DINI WAHIMIZA KUWAKATAA WASIOHESHIMU MISINGI NA TUNU ZA NCHI
Huduma za Uwakala CRDB Zachochea Ukuaji wa Mapato ya Serikali na Ujumuishi wa Kifedha
BADO TUNAMUHITAJI POLEPOLE KWA MKURUGENZI WA UPELELEZI- POLISI
BRIGEDIA JENERALI NDAGALA AFUNGUA KONGAMANO LA WADAU WA USIMAMIZI WA MAAFA JIJINI MBEYA
Mkomi Awasisitiza Wakuu wa Taasisi Kusimamia Mifumo ya Kielektroniki Serikalini.
WAZEE WAASWA KUHAMASISHA JAMII KUJITOKEZA KUPIGA KURA.
JAMII YAHIMIZWA KUWAKATAA WANAOTAFUTA HAKI KWA KUVUNJA SHERIA