

Mashindano ya Umoja wa Michezo na Sanaa kwa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) ngazi ya Mkoa wa Dodoma yamehitimishwa rasmi jijini Dodoma, huku timu bora zikiaga kwa matarajio makubwa kuelekea mashindano ya kitaifa yatakayofanyika mkoani Iringa kuanzia Juni 20 hadi 30.
Hafla ya kufunga mashindano hayo imefanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Dodoma, ikihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa elimu kutoka ngazi ya wilaya na mkoa. Akizungumza wakati wa kufunga mashindano hayo, Kaimu Afisa Elimu wa Mkoa wa Dodoma, Bi. Sophia Mbeyu, ameeleza kuridhishwa kwake na kiwango cha mashindano na kuonesha matumaini makubwa kwa timu ya mkoa itakayowakilisha Dodoma kitaifa.
Tumefunga mashindano ya ngazi ya mkoa kwa mafanikio makubwa. Tunayo matumaini kuwa vijana wetu wataipeperusha vyema bendera ya Dodoma kule Iringa,” amesema Mbeyu.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Mchumi wa Mkoa wa Dodoma, Bw. Charles Mduma, aliyemwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa huo, Bw. Kaspar Mmuya. Bw. Mduma amepongeza juhudi za pamoja zilizowezesha kufanikisha mashindano hayo, huku akiwasihi wawakilishi wa mkoa huo kutobweteka bali kujiandaa kikamilifu kwa mashindano ya kitaifa.
Hili ni jambo la kujivunia. Ushirikiano wa walimu, wanafunzi na uongozi wa elimu umeonesha mshikamano wa hali ya juu. Tunawatakia kila la heri Iringa,” amesema.
Kwa upande wake, Afisa Michezo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bw. Evance Sangawe, amebainisha kuwa timu ya mkoa imeundwa na wachezaji 120 walioteuliwa baada ya mchujo wa kina kutoka kwa washiriki wa mashindano ya ngazi ya mkoa. Amesema timu hiyo itaingia kambini kwa siku saba kabla ya kuelekea Iringa.
"Tumejipanga kufanya vizuri zaidi ya mwaka jana. Walimu walioteuliwa wana uzoefu wa kitaifa na tumeandaa programu maalum ya mazoezi na maandalizi ya kisaikolojia kwa vijana wetu,” amesema Sangawe.
Ameongeza kuwa uteuzi wa walimu walioko kambini umezingatia utendaji wao kwenye mashindano ya mkoa na uzoefu wao katika mashindano ya kitaifa, hatua inayolenga kuongeza ufanisi wa timu hiyo ya mkoa.
Nao baadhi ya wanafunzi walioteuliwa kuiwakilisha Dodoma ambao ni Iddi Yusuphu na Ester Robert walielezea furaha yao na kuahidi kufanya kila wawezalo kuhakikisha mkoa wao unarudi na ushindi kutoka Iringa.
"Tunaamini tutafanya vizuri. Tumejifunza mengi kutoka kwa walimu wetu na mashindano ya mkoa yamekuwa chachu ya mafanikio yetu,” amesema mmoja wa wanafunzi hao"
Mashindano ya UMISSETA ni jukwaa muhimu la kukuza vipaji vya michezo na sanaa miongoni mwa wanafunzi wa shule za sekondari nchini. Mkoa wa Dodoma umeonesha dhamira ya dhati ya kuwekeza kwa vijana wake kwa kutoa mazingira rafiki ya maandalizi na usimamizi thabiti wa timu na wawakilishi wake.
Mashindano hayo yamebeba kauli mbiu isemayo"Uongozi Bora ni Msingi wa maendeleo ya taaluma,Sanaa na Michezo,Shiriki Uchaguzi Mkuu 2025 Kwa Amani na Utulivu"
Maiko Salali Arejesha Fomu ya Kugombea Ubunge Jimbo la Mpwapwa, Apongeza CCM kwa Ujumuishwaji wa Makundi Maalum
DIB YAHIMIZA WANANCHI KUDAI FIDIA ZAO KUTOKA BENKI ZILIZOFILISIKA
USHIRIKI WA TAWA KATIKA MAONESHO YA 49 YA BIASHARA YA KIMATAIFA
DWIGHT DANDA KIJANA MDOGO NA MHITIMU WA CHUO KIKUU ATIA NIA UBUNGE KIBAMBA
BoT YAWATAKA TAMFI NA TAMIU KUBORESHA UPATIKANAJI WA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA.
Aliyeongoza kura maoni Vunjo 2020, kumkabili tena Dkt. Kimei
Maiko Salali achukua fomu ya ubunge Jimbo la Mpwapwa
Serikali kufanya mageuzi ya kimtazamo katika nafasi za uongozi kwa wanawake
Dkt.Tulia Aweka Jiwe La Msingi Ujenzi wa Shule ya Wavulana Bunge.
Mavunde Akabidhi Jengo la kupumzikia Wananchi Hospitali ya Rufaa ya Dodoma