

Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania unajukumu la kutoa mafunzo kwa wasanii pamoja na kutangaza huduma zake kwa umma, ambapo mafunzo yanayotolewa yanawawezesha wasanii kugeuza Sanaa kutoka kuwa burudani na kuwa biashara ili iweze kuwazalishia kipato kitakachowasaidia kujikimu na kuchangia katika pato la Taifa.
Hayo yameelezwa na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania, Bi. Nyakaho Mahemba,wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa taasisi hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita leo tarehe 28 Februari, 2025, katika ofisi za Idara ya Habari - MAELEZO, Dodoma.
Aidha amesema kuwa Mafunzo yanayotolewa yanahusisha mada mbalimbali kama vile uwekaji akiba, umuhimu wa urasimishaji, uandishi wa maandiko ya miradi, Sanaa na afya, biashara na familia na uwekaji wa kumbukumbu wa mapato ya kila siku.
Aidha, katika kipindi husika, Mfuko umetoa mafunzo kwa wasanii 11,684 ndani ya mikoa 18 nchini. Washiriki wa mafunzo walikuwa wanawake 6,985 (59.8%) na wanaume 4,699 (40.2 %).
Aidha Mfuko unatoa huduma za mikopo, mafunzo na ruzuku kwa wadau wa Utamaduni na Sanaa kwa Msanii mmoja mmoja (Msanii Binafsi), Kikundi/Bendi pamoja na Makampuni katika maeneo/ makundi ya:-Sanaa za Maonesho - Ushereheshaji, Mapambo, Upishi, ucheshi (Uchekeshaji), Sarakasi n.k,Sanaa za Ufundi – Uchongaji, Uchoraji, Ufumaji, Ushonaji, Urembo, Uchapishaji n.k,Filamu – Uandaaji wa Maudhui, Uzalishaji, Usambazaji, maktaba za video n.kMuziki - Singeli, Injili, Kaswida, Rege, Kizazi Kipya, Dansi, Taarabu, Usambazaji Lugha na Fasihi – Uandishi wa makala, uchapishaji nakadhalika.
"Kiwango cha Mkopo ni kati ya Shilingi Laki Mbili (TZS 200,000) hadi Shilingi Milioni Mia Moja (TZS 100,000,000) kwa mwombaji wa Kikundi, Kampuni au Mtu Mmoja Mmoja;Riba ya mkopo ni asilimia tisa (9) inayotozwa katika salio la mkopo (Reducing Balance Method)"
Ameongeza kuwa Kwa upande wa Takwa la Uwasilishwaji wa Dhamana:Kuanzia Shilingi Laki Mbili (Shilingi 200,000) hadi Shilingi Milioni Tano (Sh. 5,000,0000 (Hakuna takwa la uwasilishaji wa dhamana kutoka kwa waombaji) Kuanzia Shilingi Milioni 5 + hadi Shilingi Milioni Tano
Aidha Mwombaji atatakiwa kuwasilisha dhamana yenye thamani ya asilimia 20 ya kiwango cha Mkopo kitakachoidhinishwa;Kuanzia Shilingi Milioni 15+ hadi Shilingi Milioni 30 - Mwombaji atatakiwa kuwasilisha dhamana yenye thamani ya asilimia 30 ya kiwango cha Mkopo kitakachoidhinishwa;Kuanzia Shilingi Milioni 30+ hadi Shilingi Milioni 50: Mwombaji atatakiwa kuwasilisha dhamana yenye thamani ya asilimia 40 ya Kiwango cha mkopo kitakachoidhinishwa.
"Kuanzia Shilingi Milioni 50+ hadi Shilingi Milioni 100; Mwombaji atatakiwa kuwasilisha dhamana yenye thamani ya asilimia 50 ya kiwango cha mkopo kitakachoidhinishwa ambapo muda wa marejesho ni hadi miezi Ishirini na nne (24); naMuda wa rehema ni hadi miezi mitatu (3) na itategemeana na aina ya mradi"
Sanjari na hayo kwa kuzingatia umuhimu wa Mfuko katika ukuzaji na uendelezaji wa miradi ya Sanaa ili iweze kuzalisha bidhaa bora na shindani kulingana na viwango na mahitaji ya masoko ya ndani na nje ya nchi, Serikali ya Awamu ya Sita ilichukua hatua kadhaa kwa ajili ya kuongeza bajeti ya Mfuko ili uweze kutekeleza majukumu yake ya Msingi hususani katika kuzalisha ajira na kuongeza fedha za kigeni.
"Miongoni mwa hatua hizo ni:-Kuongezeka kwa bajeti ya Mfuko katika kila mwaka wa Fedha ambapo katika mwaka wa fedha 2023/24 bajeti ya Mfuko iliyoidhinishwa ilikuwa ni shilingi bilioni 1.6 ambapo katika mwaka wa fedha 2024/25 bajeti imeongezeka hadi kufikia shilingi bilioni 3."
Aidha, kiasi kilichoongezeka ni Shilingi Bilioni 1.4 ambacho ni sawa na ongezeko la asilimia 87.5 Serikali imeongeza chanzo kipya na endelevu cha mapato ya Mfuko kinachotozwa katika vibebeo tupu vya Kazi za Sanaa (Tozo ya Hakimiliki – Copyright Levy),kupitia chanzo hichi, Mfuko hupata gawio la asilimia 10 ya mapato yote yanayokusanywa. Chanzo hiki kimeanza kutekelezwa Mwezi Septemba, 2023.
MKURUGENZI WA MASOKO TTB AELEZA FURSA INAYOWEZA KUPATA TANZANIA KUTOKA JAPAN KATIKA ELIMU YA UTALII NA UHIFADHI
MENEJIMENTI YA NCAA YAPATA MAFUNZO YA KUBORESHA UTENDAJI KAZI
BALOZI LUVANDA AONGOZA UJUMBE WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAKALA WA UTALII NCHINI JAPAN
BODI YA ITHIBATI YATAMBULISHWA RASMI BUNGENI
Ibraah Afunguka: "Nilifukuzwa Konde Gang na Harmonize"
BEI YA MADINI YA DHAHABU IMEPANDA HADI DOLA ZA MAREKANI 2,655.80
Ibraah Afunguka: "Nilifukuzwa Konde Gang na Harmonize"
Sekta ya Uvuvi imetoa ajira ya Moja Kwa Moja Kwa Wavuvi 201,661
TUME YATAKA WANANCHI KUTAZAMA DAFTARI LA AWALI,KUHAKIKI TAARIFA ZAO
TUTAENDELEA KUINADI TANZANIA KWA NGUVU ZOTE EXPO 2025 JAPAN- MWAMWAJA.