Serikali imewahimiza wananchi kutumia msimu wa Sikukuu na likizo kutembelea Vivutio vya Utalii. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Utalii

Serikali imewahimiza wananchi kutumia msimu wa Sikukuu na likizo kutembelea Vivutio vya Utalii.

SERIKALI imewahimiza wananchi kutumia msimu wa sikukuu na likizo kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini ili kujifunza, kuburudika na kuchangia ukuaji wa uchumi wa Taifa.

Moreen Rojas, Dodoma.
By Moreen Rojas, Dodoma.
01 Jan 2025
Serikali imewahimiza wananchi kutumia msimu wa Sikukuu na likizo kutembelea Vivutio vya Utalii.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma jana, Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii you Tanzania (TTB) Ernest Mwamwaja alisema Tanzania imejaliwa kuwa na vivutio vya kipekee ambavyo vinapaswa kuthaminiwa na Watanzania wenyewe.

“Msimu huu wa sikukuu ni fursa muhimu kwa wananchi kutembelea vivutio vilivyopo nchini ili kujivunia urithi wetu wa asili na kiutamaduni,”alisema

Aliongeza kuwa:”Tulizindua kampeni maalumu ya kuhamasisha utalii wa ndani kati msimu huu wa sikukuu ijulikanayo kama “Funga mwaka kijanja talii “ ambayo inalenga kuwahamasisha watanzania wa rika zote kushiriki katika shughuli za utalii ambayo itakoma ifikapo junuari 10 mwaka huu.

Katika hatua nyingine Mwamwaja alisema TTB imejipanga kuendelea  kushirikiana na waandishi wa habari ili kuongeza idadi ya watalii lengo ni kuhakikisha wanatekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020/2025 ya kufikia watalii milioni tano.

Alisema lengo lingine ni kuunga mkono jitihada za Rais Dk.Samia Suluhu Hassan za kuhakikisha sekta ya utalii inakua na kuchangia katika Uchumi wa taifa.

“Tunaamini kupitia waandishi wa habari tunaweza kuwafikia wananchi wengi na kutangaza vivutio vya utalii ili kuunga mkono jitihada za Rais Dk.Samia za kutangaza vivutio vya utalii na kuongeza idadi ya watu wanaotembelea,”alisema

Aliongeza kuwa:”Tunatamani kuona wananchi wanachangamkia fursa ya kutembelea vivutio vya utalii,”alisema

NCAA IMEFANIKIWA Kudhibiti Ujangili wa Wanyamapori Ndani na Nje ya Hifadhi ya Ngorongoro.

NCAA IMEFANIKIWA Kudhibiti Ujangili wa Wanyamapori Ndani na Nje ya Hifadhi ya Ngorongoro.

OPARESHENI YA KUWADHIBITI FISI SIMIYU YAONESHA MAFANIKIO MAKUBWA

OPARESHENI YA KUWADHIBITI FISI SIMIYU YAONESHA MAFANIKIO MAKUBWA

WATANGAZAJI WAASWA KUACHA KUKIFUBAZA KISWAHILI.

WATANGAZAJI WAASWA KUACHA KUKIFUBAZA KISWAHILI.

ZOEZI LA KULIPA FIDIA WANANCHI NGOMBO LINAKWENDA VIZURI : DC MALINYI

ZOEZI LA KULIPA FIDIA WANANCHI NGOMBO LINAKWENDA VIZURI : DC MALINYI

HARUSI YA KIHISTORIA YAFUNGWA KRETA YA NGORONGORO

HARUSI YA KIHISTORIA YAFUNGWA KRETA YA NGORONGORO