SERIKALI KUENDELEA KUSIMAMIA SERA YA UTEKELEZAJI YA TEHAMA. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

SERIKALI KUENDELEA KUSIMAMIA SERA YA UTEKELEZAJI YA TEHAMA.

WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Jerry Silaa amesema Serikali itaendelea kusimamia sera ya utekelezaji ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kukuza utaalamu na uwekezaji ili kuendelea kuboresha na kuimarisha teknolojia nchini.

Sophia Kingimali.
By Sophia Kingimali.
15 Oct 2024
SERIKALI KUENDELEA KUSIMAMIA SERA YA UTEKELEZAJI YA TEHAMA.

Hayo ameyasema leo Oktoba 15, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akifungua Kongamano la nane la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA),  

Amesema Serikali imeendelea kuwekeza kwenye TEHAMA pamoja ya sheria ili kuifanya Tanzania kuwa sehemu ya mabadiliko hayo ya teknolojia Duniani.

Ameongeza kuwa Serikali imeendelea kuwekeza katika TEHAMA ambayo imeonekana kuwa nguzo kuu ya kufikia Uchumi wa Kidijitali katika Nyanja mbalimbali Duniani.

“Hivi sasa dunia ipo katika kipindi cha Mapinduzi ya nne, tano sita ya viwanda ambapo shughuli za kiuchumi, kijamii na uzalishaji inakwenda kuendeshwa kwa kutumia teknolojia " amesema Silaa.

Aidha Silaa amebainisha  kuwa Wizara imepewa jukumu la kusimamia sera ya TEHAMA 2016 ambayo inalenga kukuza matumizi ya TEHAMA nchini.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mohammed  Abdulla, amesema kuwa lengo la Kongamano hilo ni kuwakutanisha wadau wa sekta ya TEHAMA kwa ajili ya kupata fusa ya kujadili masuala yanayohusu teknolijia  ili kuhamasisha matumizi yake nchini.

“Kongamano hili lina sura ya kimataifa ambapo washiriki kutoka ndani ya nchi na nje ya nchi wameshiriki, tutashuhudia utoaji wa tuzo ya Kimataifa na Tanzania imekuwa mwenyeji kwa kuwa nchi ya kwanza kufanyika mashindano haya yaliyoandaliwa na Umoja wa Afrika kuhusu masuala ya Akili Mnemba na Roboti” amesema Abdulla.

Nae,Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA, Prof. Leonard Msele amesema kuwa  Kongamano hilo limekuwa wakijadilia masuala mbalimbali ya uchumi wa digitali lakini kwa mwaka huu wamejikita katika eneo la Akili Mnemba na Roboti kwa sababu ndio eneo linalojadilliwa zaidi Duniani.

Kongamano la nane la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa mwaka huu limebeba kauli mbinu isemayo : 'Kutumia uwezo wa Akili Mnemba na Roboti kwa mapinduzi ya kiuchumi na kijamii'

DCEA YABAINI WAFANYABIASHARA WA SHISHA WANAOCHANGANYA BIDHAA HIYO NA DAWA ZA KULEVYA.

DCEA YABAINI WAFANYABIASHARA WA SHISHA WANAOCHANGANYA BIDHAA HIYO NA DAWA ZA KULEVYA.

AWESO,BASHUNGWA WAJADILI MIKAKATI KUTATUA CHANGAMOTO YA MAJI KATIKA JIJI LA TANGA.

AWESO,BASHUNGWA WAJADILI MIKAKATI KUTATUA CHANGAMOTO YA MAJI KATIKA JIJI LA TANGA.

Vyuo Vikuu Dar vyatambulisha tamasha la UNIFEST 255.

Vyuo Vikuu Dar vyatambulisha tamasha la UNIFEST 255.

TRENI YA MCHONGOKO KUSIMAMA KWA SAA SITA NI HUJUMA:TRC

TRENI YA MCHONGOKO KUSIMAMA KWA SAA SITA NI HUJUMA:TRC

SOKO SWAHILI MARKET KUJA NA FURSA KWA WAJASILIAMALI WADOGO.

SOKO SWAHILI MARKET KUJA NA FURSA KWA WAJASILIAMALI WADOGO.