Serikali ya Tanzania kuendelea kushirikiana na Serikali ya Zanzibar | The Dodoma Post
The Dodoma Post Tanzania

Serikali ya Tanzania kuendelea kushirikiana na Serikali ya Zanzibar

Dodoma.SERIKALI kupitia Ofisi ya Taifa ya TAKWIMU,imesema kuwa Takwimu ni suala la Muungano hivyo Serikali ya Tanzaniaa itaendea kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika suala zima la kuleta maendeleo kwa nchi zote mbili kama ilivyoasisiwa na Viongozi wa awali.

Moreen Rojas
By Moreen Rojas
24 Jul 2024
Serikali ya Tanzania kuendelea kushirikiana na Serikali ya Zanzibar

Kauli hiyo imetolewa na Mtakwimu Mkuu wa Serikali,DK.ALBINA CHUWA,wakati akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa  Kamati ya Bajeti pamoja na Watendaji kutoka Ofisi ya Rais  Fedha na Mipango  waliofanya ziara ya Mafunzo kwenye Ofisi ya Taifa ya Takwimu.

"haya yote yanayofanyika ni mashirikiano ambayo yataleta tija pande zote mbili na kwakufanya hivi ni kuunga mkono waasisi wa Taifa hili Mwalimu Julius kambarage Nyerere pamoja na Amani Abeid karume". Amesema Dkt.Chuwa

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Sensa Toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu EMILIAN KALUGENDO akitoa mada amesema  wanatekeleza Mpango wa pili wakuimarisha na kuboreshaTakwimu na mradi huo ulianza 2022/2023 na unatarajiwa kukamilika mwaka 2027 pamoja na kuimarisha Pato la Taifa.

"tutakuwa tukiandaa Kwa pamoja Mifumo ya kizalisha Takwimu za kiutawala kati ya Tanzania bara na Tanzania zanziba pamoja utafiti wa kilimo na mifugo wa kila mwaka utatekelezwa na utafiti wa mapato na matumizi wa kaya binafsi na utafiti wa watu Wenye uwezo wa kufanya KAZI". Amesema

Naye Naibu Waziri wa Fedha Zanzibar,SALUM ALLY SALUM,amesema kuwa ni muhimu  kuwaeleza Watendaji wao  umuhimu wa matumizi ya Takwimu ili Wananchi kupata uelewa.

"changamoto zipo lakini kutokana na mashirikiano haya tutaimarisha maeneo mengi ili tupate Takwimu sahihi Maana ukosefu wa Takwimu huna taarifa na kama huna taarifa ni sawa sawa na kwenda vitani huna silahi lazma utapigwa tu" Amesema

Awali Mwenyekiti wa Kamati hiyo,ya Bajeti ya  Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi MWANAASHA KHAMIS JUMA amesema wataendelee kushirikiana kwa maslahi ya wananchi wa pande zote mbili.

"haya yote tunayofanya ni kutokana na maelekezo ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa serikali ya Mapinduzi zanziba Dkt. Hussein Ally Mwinyi kutaka maeneo haya yaimarishwe ili kupata Takwimu sahihi kwa maslahi ya pande zote mbili". Amesema

JESHI LA POLISI LATOA TAMKO UTATA WA KIFO CHA MSANII MANDOJO.

JESHI LA POLISI LATOA TAMKO UTATA WA KIFO CHA MSANII MANDOJO.

RC CHALAMILA AIPONGEZA TPDC KWA KUTOA ELIMU YA UTUNZAJI MIUNDOMBINU YA SHIRIKA HILO.

RC CHALAMILA AIPONGEZA TPDC KWA KUTOA ELIMU YA UTUNZAJI MIUNDOMBINU YA SHIRIKA HILO.

Asali ya Tanzania Yapata Kibali Kuuzwa China.

Asali ya Tanzania Yapata Kibali Kuuzwa China.

BENKI YA BIASHARA TANZANIA (TCB) KUSHIRIKIANA NA  BUNGE LA TANZANIA KUWAINUA WAJASIRIAMALI NCHINI.

BENKI YA BIASHARA TANZANIA (TCB) KUSHIRIKIANA NA BUNGE LA TANZANIA KUWAINUA WAJASIRIAMALI NCHINI.

REA YAAHIDI KUENDELEA KUWAWEZESHA WAENDELEZAJI BINAFSI WA UMEME NCHINI.

REA YAAHIDI KUENDELEA KUWAWEZESHA WAENDELEZAJI BINAFSI WA UMEME NCHINI.