

Wadau wa Ununuzi waaswa kuzingatia maadili na elimu katika Ununuzi wa Umma ili kuiwezesha Serikali kupata thamani halisi ya fedha
Wito huo umetolewa mwishoni mwa wiki na Katibu Mtendaji wa Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA), Bw. James Sando alipokuwa akifunga mafunzo ya siku mbili kuhusu matumizi ya Moduli ya kuwasilisha na kushughulikia malalamiko na rufaa kwa njia ya kielektroniki katika mfumo (NeST) kwa wazabuni na wadau wa ununuzi wa Umma kutoka taasisi za Serikali kwa Kanda ya Kaskazini yaliyofanyika jijini Arusha.
Bw. Sando amesema kuwa baadhi ya kesi zinazowasilishwa PPAA kwa asilimia kubwa zinakuwa zimesababishwa na ukiukwaji wa maadili.
“Kama wadau katika sekta ya ununuzi wa umma ni muhimu sana kuzingatia maadili kwa sababu ndiyo itakayoipatia serikali thamani halisi ya fedha na heshima, sote tunajua mifumo ya ununuzi ipo lakini inaongozwa na binadamu kama hawana maadili mifumo haina maana,” alisema Bw. Sando
Bw. Sando aliongeza kuwa unaweza kutengeneza sheria nzuri sana lakini kama watu hawataamua kuwa watiifu wa sheria hiyo kutakuwa na uvuinjifu mkubwa wa sheria katika nchini hiyo.
“……vivyo hivyo hata sisi tukikosa maadili katika sekta ya ununuzi wa umma tutakuwa na kesi nyingi sana……kutakuwa na upotevu wa fedha za umma,” aliongeza Bw. Sando
Kadhalika, Bw. Sando amewataka washiriki walipota fursa ya kuhudhuria mfunzo hayo kwa Kanda ya Kaskazini kuwaelimisha wadau wengine kuhusu matumizi ya moduli ya kuwasilisha na kushughulikia malalamiko na rufaa kwa njia ya kielektroniki (Complaint and Appeal Management Module) katika Mfumo wa Kielektroniki wa Ununuzi wa Umma (NeST).
Naye mmoja wa wadau wa ununuzi wa umma aliyeshiriki mafunzo hayo Bi. Rachel Werema aliipongeza PPAA kwa kuandaa mafunzo hayo ya siku mbili kwani yamewasaidia kufahamu namna ya kuwasilisha malalamiko na rufaa zitokanazo na michakato ya ununuzi kwa wakati kupitia moduli iliyopo katika mfumo wa NeST.
Mafunzo hayo ya siku mbili kwa Kanda ya Kaskazini yelifanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 10 – 11 Aprili, 2025 yalihudhuriwa na washiriki 240 kutoka mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga.
Awamu ya kwanza ya mafunzo kikanda yalifanyika Kanda ya Ziwa kwa siku tatu ambapo yalijumuisha washiriki zaidi ya 580 mkoani Mwanza kuanzia tarehe 4 – 6 Februari, 2025 yakijumuisha mikoa ya Mwanza, Geita, Mara, Kagera, Simiyu na Shinyanga.
Maiko Salali Arejesha Fomu ya Kugombea Ubunge Jimbo la Mpwapwa, Apongeza CCM kwa Ujumuishwaji wa Makundi Maalum
DIB YAHIMIZA WANANCHI KUDAI FIDIA ZAO KUTOKA BENKI ZILIZOFILISIKA
USHIRIKI WA TAWA KATIKA MAONESHO YA 49 YA BIASHARA YA KIMATAIFA
DWIGHT DANDA KIJANA MDOGO NA MHITIMU WA CHUO KIKUU ATIA NIA UBUNGE KIBAMBA
BoT YAWATAKA TAMFI NA TAMIU KUBORESHA UPATIKANAJI WA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA.
Aliyeongoza kura maoni Vunjo 2020, kumkabili tena Dkt. Kimei
Maiko Salali achukua fomu ya ubunge Jimbo la Mpwapwa
Serikali kufanya mageuzi ya kimtazamo katika nafasi za uongozi kwa wanawake
Dkt.Tulia Aweka Jiwe La Msingi Ujenzi wa Shule ya Wavulana Bunge.
Mavunde Akabidhi Jengo la kupumzikia Wananchi Hospitali ya Rufaa ya Dodoma