

Uongozi wa wazee wa Yanga na uongozi wa mkoa wa Dodoma wamemtaka Rais wa shirikisho wa mpira wa miguu Tanzania Wallace Karia kuomba radhi kwa timu yao kufuatia kauli waliyoiita ya kuwafokea
Akizungumza Kwa niaba ya Wazee wengine Abdalah Mtosa amesema hawaoni sababu ya kurudia mchezo ambao tayari ulipangwa kisheria na kuahirishwa bila utaratibu siku ya Machi 8,2025
Mzee Mtosa amesema siku pekee ambayo ilikuwa halali kwa mchezo huo kuchezwa tayari imepita na ilikuwa inatosha kabisa kuwakutanisha watani kwani maandalizi yote yalikuwa yameshakamilika.
"Nimepokea kwa masikitiko makubwa sana Kwa kuahirishwa kwa mchezo wa Machi 8 mwaka huu, kwahiyo na sisi hatuna imani na karia kwani tunajua wazi hana mapenzi ya dhati na yanga
hivyo niwaombe viongozi wa juu kutokuruhusu mechi kufanyika tena Kwa wakati mwingine kama ni faini tuko tayari kulipa lakini sio kurudia mechi na simba". amesema Mtosa
Naye Mzee Bodar Awadhi amesema mechi kuahirishwa imefanya kutokea mkanganyiko na sintofahamu kwa mashabiki wa soka na hivyo kundi kubwa halitaki tena hiyo mechi.
Kauli ya kutokuwa na imani tena na Rais Karia imekuja mara baada ya kuahirishwa Kwa dabi ya karikakoo na Kutokana na kauli aliyoitoa ambayo wameita kauli ya kuwafokea.
"Sisi msimamo wetu ni kutokurudia mechi kwanza RAIS wa TFF ametudhalilisha wanayanga na kama ameshindwa mpira arudi kwenye taaluma yake kwani tunaijua"
Kwa upande wake Mratibu wa yanga Dodoma Elisha Ngwando amesema Karia aombe Radhi kwa Wanachama wa Yanga na wanamichezo kwa alichokifanya na kauli aliyoitoa.
"Watu wametumia gharama kubwa wengine wamelipia matangazo kwa ajili ya mechi hiyo"
CCM Yatangaza Wagombea Nafasi Ya Ubunge Waliopenya Kwenye Mchujo:Mpina,Makamba Waenguliwa.
KATIBU BAWACHA AJIUNGA CHAUMA ATAJA SABABU YA KUONDOKA KWAKE.
MASLAHI MAPANA YA NCHI YANAZINGATIWA UTEKELEZAJI WA MRADI WA EACOP-DKT. MATARAGIO.
VYAMA VYA SIASA VYAHAKIKISHIWA UWANJA SAWA UCHAGUZI MKUU 2025
INEC YATANGAZA RASMI TAREHE YA UCHAGUZI MKUU 2025.
CCM Yatangaza Wagombea Nafasi Ya Ubunge Waliopenya Kwenye Mchujo:Mpina,Makamba Waenguliwa.
SHUJAA ALIYEPIGANA VITA ASISITIZA AMANI.
VITUO VIWILI VYA KUPUNGUZA KASI YA MAFUTA GHAFI EACOP KUJENGWA NCHINI.
TBC KUAZIMISHA MIAKA 26 YA KUMBUKUMBU YA KIFO CHA HAYATI MWALIMU NYERERE KWA KUENDESHA MASHINDANO YA INSHA KWA WANAFUNZI.
SERIKALI YASIKIA KILIO CHA WANANCHI YAINGIZA SEKTA BINAFSI KUENDESHA MRADI WA MWENDOKASI.