Naibu waziri Mkuu na Waziri wa Nishati amelipongeza Shirika la maendeleo ya Petroli na gesi TPDC kwa kuendelea kusimamia vyema ujenzi wa vituo vya kujazia Gesi asilia (CNG) nchini huku ambapo bilioni 18.9 zimetumika kujenga vituo hivyo.
Naibu waziri Mkuu na Waziri wa Nishati amelipongeza Shirika la maendeleo ya Petroli na gesi TPDC kwa kuendelea kusimamia vyema ujenzi wa vituo vya kujazia Gesi asilia (CNG) nchini huku ambapo bilioni 18.9 zimetumika kujenga vituo hivyo.
Hayo ameyasema leo Januari 9,2025 Jijini Dar es salaam wakati wa ziara yake ya kutembelea kituo cha ,kujaza gesi asilia kituo kilichopo ubungo Mawasiliano kinachojengwa na TPDC.
"Mitambo yote inayohitajika imeshawasili na Ujenzi utakamilika ndani ya wiki moja umekamilika na maandalizi yamekamilika na Mkandarasi ametuhakikishia itakapofika Februari 03, 2025 kwa mara ya kwanza magari yatakuwa yanakuja kujaza gesi hapa." Amesema Dkt. Biteko
Amesema malengo ni kuondoa foleni ambazo zimekuwa zinajitokeza katika vituo vya kujazia gesi katika magari, Pikipiki na Bajaji..
Amesema mwitikio wa Watanzania kuhama kwenye matumizi ya mafuta kwenda kwenye nishati safi umekuwa mkubwa sana ndio maana watu wanaotumia vyombo vya usafirishaji wanatumia gesi asilia.
"Serikali Rais Samia imeshatoa maelekezo tujenge vituo vingi zaidi katika jiji la Dar es Salaam ambako ndio kuna watumiaji wakubwa wa gesi asilia."
Amesema kutajengwa kituo kingine cha kujazia gesi asilia katika vyombo ya usafiri, lakini wakati huo huo kunavituo vingine saba vinajengwa na sekta binafsi.
Amesema nia ya Serikali ni kuona kwamba vituo hivyo vinaongezeka idadi mpaka kufikia vituo 15, wakati huo huo kuwe na vituo vinavyotembea ambavyo vitakuwa morogoro kimoja na Dodoma vitakuwepo viwili.
"Nataka tuwahamasishe sana wananchi kutoka kwenye matumizi ya nishati siyokuwa safi kwenda kwenye nishati safi ambayo Rais Samia ni Kinara wa Nishati safi Afrika na hasa nishati ya kupikia."Amesema.
Amesema kuwa watahakikisha kuwa vituo hivyo vinajengwa kwa haraka, pia amewapongeza TPDC kwa kazi nzuri wanayoifanya na kuajiri vijana wakitanzania kwaajili ya kusaidia kazi za ujenzi wa kituo hicho.
Akizungumzia matumaini ya ujenzi wa kituo cha gesi asilia kwaajili ya kujaza kwenye vyombo vya usafiri, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba amesema matumaini ni makubwa kwani februari 03,2025 magari yataana kujaza gesi katika kituo hicho.
Amesema kituo hicho ni kituo mojawapo kilichopo katika mipango ya maendeleo kabla ya kuisha mwaka wa fedha wanatagemea kuwe na vituo vingine saba ambavyo vitakuwa Mbezi Beach, Tegeta, Mwenge, Simu 2000, Muhimbili na kibaha ikiwa na nia ya kuwawezesha wananchi wanaotaka kubadilisha magari yao kutumia gesi au wameshabadilisha waweze kuwa na nishati safi ya gesi katika magari yao.
Amesema mipango ya wizara kwenye eneo la gesi asilia linakwenda vizuri hasa kwenye matumizi ya kawaida kwani pia wamekubaliana na Wakala wa Mabasi yaendayo haraka (DART) kwamba magari yatayokuja yatakuwa na uwezo wa kutumia gesi asilia.
Kwa upande wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM), Profesa William Anangisye amesema kuwa ujenzi wa kituo cha CNG katika eneo la UDSM utawanufanisha hasa katika kutoa elimu kwa vitendo kwa wanafunzi wa chuo hicho pamoja na fursa mbalimbali zitakazojitokeza kwa wanafunzi wanaosomea masuala ya gesi.
"TUMEAMUA KUSIMAMA NA LISU MBOWE AKAPUMZIKE"VIONGOZI CHADEMA WANENA
KOREA KASKAZINI YAWANASA ‘SNIPER’ UKRAINE, YADAI RUSSIA INAWAUA MAJERUHI
MAREKANI HALI TETE, MOTO WAUA 16 LOS ANGELES, UPEPO WATARAJIWA KUONGEZEKA
Ajali ya gari yajeruhi mamia ya watu Ufaransa
Maria Sarungi atekwa Kenya wasiojulikana watajwa
"TUMEAMUA KUSIMAMA NA LISU MBOWE AKAPUMZIKE"VIONGOZI CHADEMA WANENA