

Naibu Waziri wa Nchi,ofisi ya Rais Mipango na uwekezaji Stanslaus Nyongo amiezitaka asasi za Kiraiai(AZAKI) kufanya majadIliano ya pamoja na kujenga uelewa wa pamoja ili kufanikisha upatikanaji wa dira ya Taifa 2050 inayotokana na maoni ya wananchi.
Rai hìyo ameitoa leo Januari 10,2025 wakati akifungua mkutano wa Asasi za Kiraia zilizokutana jijini Dar es salaam ili kufanya mapitio ya Rasimu ya kwanza ya dira ya Maendeleo ya Taifa 2050.
Amesema ni muhimu kuwepo na majadiliano ya pamoja baina ya Serikali na wadau wa maendeleo badala ya ukosoaji ili kufanikisha Dira ya Maendeleo ya Taifa inakua shirikishi.
"Amesema Serikali imejiandaa vya kutosha kusikiliza maoni yote yanayotolewa na wadau na wananchi ili kuhakikisha Dira 2050 inakua halisi na inayotokana na wananchi wenyewe",Amesema Nyongo.
Akizungumzia uzoefu wake akiwa kama Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Maendeleo ya Jamii amesema amekutana mara kwa mara na Kamati hizo za kiraia.
"Usipoelewa dhamira yao ya kukumbusha baadhi ya mambo huenda ukafikiri kuwa wanaikosoa Serikaliì jambo ambalo sio la kweli wanafanya hivyo kwa ajili ya kujenga uelewa mpana wa mambo ambayo wanayajadili.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Foundation for Civil Society(FCS) Justice Rutenge ameipongeza serikali kwa kuwajumuisha wadau wa asasi za kiraia katika hii uandishi wa dira ya maendeleo ya mwaka 2050.
Aidha Rutenge amehimiza umuhimu wa kukuza uchumi na kuwa na uchumi shindani kuelekea miaka 25 ijayo ili kutoa hakikisho la Nchi na ustawi jumuishi na endelevu kwa kizazi cha sasa na vijavyo.
Naye,Mkuu wa programu za Umoja wa mataìfa nchìni (UNA-TANZANIA) Lucas Kifyasi amesema kuwa utekelezaji wa dìra hiyo unahìtajì kipaumbele katika elimu hasa ya teknolojia kwa kuzingatiaii mapinduzi ya viwanda yanayotarajiwa kuimarika miaka 25 ijayo.
WATAALAMU WA UNUNUZI NA UGAVI WAASWA KUZINGATIA MADILI
SERIKALI IMEDHAMIRIA KUHAKIKISHA KILA ENEO LINATAMBULIKA KWA ANWANI YA MAKAZI
WAGOMBEA NAFASI YA NGAZI YA URAIS CCM KUTAMBULISHWA KWENYE MIAKA 48 YA CHAMA HICHO.
SERIKALI KUFANYA SENSA YA UZALISHAJI VIWANDA KWA MWAKA WA REJEA 2023.
AZANIA BENKI BUNGE BONANZA LAWALETA PAMOJA MASHABIKI WA SIMBA NA YANGA.
MASHABIKI WA SIMBA NA YANGA KUKUTANA KATIKA BONANZA LA KUHAMASISHA MICHEZO NA UMUHIMU WA MAZOEZI.
MABADILIKO YA SERA YA ELIMU KUAKISI MABADILIKO YA KITAIFA NA KIMATAIFA.
RASMI UZINDUZI WA SERA YA ELIMU KUFANYIKA TAREHE 1 FEBRUARI 2025.
WASIRA: CHADEMA MSIJE NA AZIMIO LINALOKIUKA SHERIA ZA NCHI YETU.
SERIKALI IMEDHAMIRIA KUHAKIKISHA KILA ENEO LINATAMBULIKA KWA ANWANI YA MAKAZI