Tanzania inatarajiwa kuwa nchi mwenyeji kwenye Makutano wa saba (7) wa kimataifa wa jumuiya ya Mamlaka za usimamizi wa usafiri Majini Barani Afrika utakaofanyika kuanzia Novemba 29,hadi Disemba 1, 2024 jijini Dar es salaam ambapo mkutano huo umeandaliwa na shirika la uwakala wa Meli Tanzania (TASAC).
Tanzania inatarajiwa kuwa nchi mwenyeji kwenye Makutano wa saba (7) wa kimataifa wa jumuiya ya Mamlaka za usimamizi wa usafiri Majini Barani Afrika utakaofanyika kuanzia Novemba 29,hadi Disemba 1, 2024 jijini Dar es salaam ambapo mkutano huo umeandaliwa na shirika la uwakala wa Meli Tanzania (TASAC).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Novemba 25,2024 jijini Dar es salaam na waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa inasema lengo la mkutano huo ni kujadili masuala muhimu ya maendeleao ya udhibiti na usimamizi wa usalama wa usafiri majini barani Afrika.
Ambapo,Kauli mbiu ya mkutano huo ikiwa ni ' Kuimarisha mustakabali wa sekta ya usafiri majini barani Afrika, ushirikianao katika teknolojia na ubunifu ili kupunguza hewa ukaa, kuimarisha usalama wa mazingira, na mazingira ya sekta ya usafiri majini kwa mustakabali endelevu'.
Amesema kipaumbele cha mkutano huo ni kuangalia mustakabali wa usafiri wa majini na kuongeza ushirikiano baina ya nchi wanachama
Ameongeza kuwa mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Dotto Biteko na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu wa shirika la Bahari Duniani, Bw Antonio Dominguez pamoja na wataalam wa usafiri majini, viongozi wa mamlaka za udhibiti wa usafiri kutoka nchi na wanachama wa umoja wa Afrika zipatazo 40 ambazo zina bahari.
Pia mkutano huo utatatumika kama jukwaa muhimu katika kuwezesha wadau kushiriki katika majadiliano yanayogusa masuala ya teknolojia na ubunifu yenye kulenga katika kuimarisha usalama wa usafiri majini.
"Ushiriki wa Bw. Dominguez ni heshima kubwa kwetu kama Tanzania hasa kipindi hiki tunapotekeleza sera ya Taifa ya uchumi wa Buluu ambapo kama nchi tumebainisha masuala ambayo serikali kwa kushirikiana na Wadau" amesema waziri Mbarawa
Aidha amebainisha kuwa Tanzania itaendelea kutangaza fursa za kiuchumi zilizopo katika sekta ya usafiri kwa njia ya maji zinazohusiana na utumiaji wa rasilimali za habari na maziwa zitakazo saidia kuongeza uwezo wa serikali kuwa hudumia wananchi na kuwaletea maendeleo.
Aidha ametoa wito kwa wadau wa sekta ya usafiri wa majini, wakiwemo wasafirishaji, wamiliki wa vyombo vya usafirishaji majini, wawakilishi wa mashirika ya kimataifa, viongozi wa serikali kujitokeza kwa wingi kuhudhuria mkutano huo muhimu.
KOREA KASKAZINI YAWANASA ‘SNIPER’ UKRAINE, YADAI RUSSIA INAWAUA MAJERUHI
MAREKANI HALI TETE, MOTO WAUA 16 LOS ANGELES, UPEPO WATARAJIWA KUONGEZEKA
Ajali ya gari yajeruhi mamia ya watu Ufaransa
Maria Sarungi atekwa Kenya wasiojulikana watajwa
BENKI KUU YAWAGEUKIA WATENGENEZAJI, WAUZAJI ‘PUTTY’