SHIRIKA la BIMA la Taifa (NIC), limezindua msimu wa pili wa kampeni ya NIC Kitaa yenye lengo la kutoa elimu ya bima kwa wananchi wote kwa kuwafuata kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo mitaani na kwenye shughuli zao za kiuchumi.
Hayo ameyabainisha leo Novemba, 12 2024 jijini Dar es Salaam na Mtendaji Mkuu wa NIC Kaimu Mkeyenge amesema wananchi wa Tanzania wana uelewa wa asilimia mbili kuhusu elimu ya bima hivyo wamejipanga kuhakikisha wanatoa elimu hiyo kwa wananchi wote ili kufikia asilimia tano.
Amesema wameingia msimu wa pili wa kampeni wa NIC Kitaa kusogeza huduma kwa wananchi na kuhakikisha elimu ya bima inawafikia wananchi wote ili watambue umuhimu wa bima.
"Uelewa wa bima bado uko chini sisi kama Taasisi kongwe ya serikali tunawajibu wa kusaidia serikali kwa sababu bima ni ukusanyaji wa fedha za wananchi ambao wanahisi wakipata majanga wasaidiwe na faida yake inaweza kusaidia uchumi ambao unawekezwa katika mabenki mbalimbali hivyo tunaongeza mtaji kwenye soko hususan sekta ya bima,"'amesema.
Aidha Mkeyenge amesema kutoa elimu hiyo ni kuendeleza sera ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha bima kwa wote na kuhakikisha watanzania wote wanatumia bima.
Ameongeza kuwa pamoja na kutoa elimu ya kampeni hiyo wataambatisha na kuandikisha bima kwa wateja wapya lakini pia wanapokea malalamiko na kuyapatia ufumbuzi hapohapo lakini pia kulipa madeni sio lazima wafike ofisini kwani wamewasogezea huduma.
Ameeleza kuwa kampeni hiyo inatarajia kufanyika kufayika nchi nzima lakini kwa sasa wameanza na mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma na Singida.
REA KUSHIRIKIANA NA NJOMBE KUSAMBAZA MITUNGI YA GESI ZAIDI YA 13,000
TANZANIA NA UTURUKI KUSHIRIKIANA SEKTA YA MALIASILI NA UTALII
SHEKHE wa mkoa wa Dodoma atunukiwa Udaktari wa Heshima
BALOZI NCHIMBI KUONGOZA WAOMBOLEZAJI MAZISHI YA KIBIKI LEO.
RAIS DK.SAMIA KUFUNGUA MKUTANO WA UWEKEZAJI SEKTA YA MADINI.
SHEKHE wa mkoa wa Dodoma atunukiwa Udaktari wa Heshima
Kuelekea Maadhimisho ya UKIMWI Duniani,Serikali yaeleza ushamiri wa VVU kitaifa kuwa ni asilimia 4.4
BOT YAWATAKA WANANCHI KUKOPA KWENYE TAASISI ZENYE LESENI YA BENKI HIYO.
RAIS DK.SAMIA KUFUNGUA MKUTANO WA UWEKEZAJI SEKTA YA MADINI.
Kuelekea Maadhimisho ya UKIMWI Duniani,Serikali yaeleza ushamiri wa VVU kitaifa kuwa ni asilimia 4.4