Kampuni ya PASS Leasing kwa kipindi cha miaka mitatu ya utendaji imefanikiwa kuwafikia wakulima zaidi ya 1000 katika maeneo mbalimbali nchini na kuwawezesha zana zenye thamani ya zaidi ya Tsh. Bilioni 50 nchini kote.
Hayo yameelezwa na Rosebud Kurwijila mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ambaye amezungumza kwa niaba ya Mkurugenzi katika kampuni ya PASS leasing wakati akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya maonyesho 88 Nzuguni jijini Dodoma.
Aidha amesema kuwa Kati ya hao vijana ni 20% wanawake ni takribani 10%Kampuni hii imefanikiwa kutoa vifaa mbalimbali ikiwemo trekta, powertiller (trekta za mikono), mashine za kuvunia, mashine za kuchakata mazao, magari ya usafirishaji wa mazao ya kilimo na vifaa mbalimbali vinavyotumika kwenye mnyororo wa thamani wa kilimo,uvuvi na ufugaji.
Aidha kampuni ya PASS Leasing, leo imekabidhi vifaa vya kulimia, ambavyo ni trekta 9 aina ya SWARAJ 744 na SWARAJ 855 zenye themani ya TZS 401.76 millioni kwa wakulima wa mkoa wa Dodoma; wilaya ya Kongwa na Chemba waliowezeshwa kupitia huduma za PASS Leasing.
"Uwezeshaji huu tunategemea utakwenda kuongeza uzalishaji kwa kulima mashamba zaidi ya ekari 2000; kutengeneza ajira za moja kwa moja zisizopungua 30 na kuwAmeongeza wanufaika takribani 300 kwa kipindi cha msimu mmoja Aidha, katika kanda ya kati, mkoa wa Dodoma na Singida
tumeshawezesha zana zenye jumla ya thamani ya takribani bilioni 13 kwa wajasiliamali zaidi ya 350 kati yao vijana ni 25%" Ameongeza
Aidha amesema kuwa PASS leasing ikishirikiana na AGRICOM AFRICA, PASS Leasing imekuwa na makubaliano ya kibiashara na kampuni ya AGRICOM AFRICA ambao ni wauzaji na wasambazaji wa zana mbali mbali za kilimo ikiwemo trekta, pawatila, machine za kuvunia na zana nyingine.
"Makubaliano haya yanalenga kuhakikisha wakulima wajasiriamali wanapata bidhaa bora, na huduma baada ya mauzo ikiwemo mafunzo na huduma za utengenezaji wa zana.Hadi kufikia sasa kwa kushirikiana na kampuni hii tumeweza kwa pamoja kutoa zana mbalimbali zaidi ya 350, ambazo zipo kwenye ubora wa juu na wakulima wanafurahia huduma zao na Kampuni hii inahudumia wateja nchi nzima kupitia matawi yake yaliyopo Dar es salaam (makao makuu), Melela, Mbeya, Igurusi, Kahama, Mwanza, Sumbawanga, Babati n.kNani anaweza kunufaikaWanufaika wa huduma za PASS Leasing Company Limited, ni mtu binafsi, kampuni, kikundi n.k ambao wamejikita katika shughuli za kibiashara za kilimo, uvuvi, ufugaji wa mifugo na nyuki pamoja na usafirishaji na usindikaji wa mazao ya kilimo"
"Jinsi ya kufanya maombi fika kwenye banda letu la Nane nane, lililopo kwenye tenti la (Agri-financing and Development Partners mkabala na tenti la wizara ya mifugo na uvuvi),makao makuu ya ofisi yetu ni Dar es salaam Tanzania na tuhudumia wateja nchi nzima kupitia ofidi za kanda,mteja atajaza fomu za maombi zipatikanazo pitia matawi yaliyopo Arusha, Morogoro, Mwanza, Kigoma,Tabora, Mbeya, Songea, Kibaigwa na Kahama" Amesisitiza.
"Hivyo kwa wakulima na wajasiliamari waliopo jirani na maeneo hayo wanaweza kuwasiliana na ofisi iliyo karibu ili kupata muongozo namna ya kufaidika na huduma zetu.Lakini pia mteja anaweza kufanya maombi kupitia tovuti yetu ya www.passlease.co.tz ambapo wanaweza kupata huduma zetu zote bila hata kufika katika ofisi zetu"
"Ushirikiano na makampuni mengine Kwa sasa tayari tumeingia makubaliano na makampuni mbalimbali ya utengenezaji na uuzaji wa zana za kilimo na viwanda na hivyo kuwapa wateja wigo mpana wa kuchagua vifaa wanavyovihitaji,tumefanya pia makubaliano na makampuni mbalimbali ya bima ambayo yatatoa huduma za kibima kwa wateja wetu na hivyo kuwafanya wateja waweze kuendelea na shughuli za uzalishaji bila wasiwasi wowote"Amesema
Kwa upande wake Jalia Abdalah Rashid ambaye ni mkulima kutoka wilaya ya Kongwa ameishukuru kampuni hiyo kwa kuweza kuwaletea zana za kilimo za kisasa kwani hapo mwanzoni walikuwa wanalima kilimo cha mkono lakini hivi sasa ataenda kulima kilimo cha kisasa kwa wakati na kupata mazao ya kutosha kwani anaamini kulima kwa kutumia trekta kutampa uwezo wa kulima heka nyingi kwa muda mfupi na kufikia malengo aliyokuwa akiyatamani kwa muda mrefu hivyo anawashauri wakulima wenzake kuacha kulima kizamani na kuhamia kwenye kilimo cha kisasa na chenye tija.
DKT. BITEKO ataka TANESCO kuongeza kasi utekelezaji miradi ya umeme wa gridi
Ndaisaba azidi kumwaga Fedha katika sekta ya Michezo Wilayani Ngara
"Hatutawavumilia wanaochochea Machafuko Nchini" Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan
(LHRC) chatoa maelekezo kwa vyombo vya ulinzi na usalama Kufuatia mauaji ya watoto watatu wa familia moja
TRA yaahidi kuwa na usawa kwa wafanyabiashara Nchini
VIJANA NDIO WALINZI WA NCHI HII: MEJA JENERALI RAJABU MABELE
BRIGEDIA Jenerali Ngata Apongezwa uongozi makini SUMAJKT
VIONGOZI SOKO LA MACHINGA DODOMA WASIMAMISHWA KUPISHA UCHUNGUZI
TRA yaahidi kuwa na usawa kwa wafanyabiashara Nchini
(LHRC) chatoa maelekezo kwa vyombo vya ulinzi na usalama Kufuatia mauaji ya watoto watatu wa familia moja